Mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali Mstaafu FABIAN MASSAWE
amewataka waendesha PIKIPIKI kuachana na
tabia ya kuendesha PIKIPIKI kwa mazoea badala yake wajiunge na vyuo vinavyotoa
mafunzo ya udereva ili waweze kuelewa vyema kanuni na sheria zinazohusiana na
masuala ya usalama barabarani hali ambayo itakayopunguza ongezeko la ajali mkoani
humo.
Kanali MASSAWE ametoa kauli hiyo wakati akiitimisha mafunzo
wa mwezi mmoja yaliyoandaliwa na chuo cha udereva cha LAKE ZONE kilichoko mjini
BUKOBA yaliyotolewa kwa waendesha vyombo vya moto wa kijiji cha BUGANGO kilichoko wilayani
MISSENYI.
MASSAWE amewaambia madereva
wanaoendesha PIKIPIKI zinazofanya
biashara ya kubeba abiria maarufu kwa jina la BODA BODA wazingatie sheria
iliyowekewa ya kuvaa kofia ngumu , amesema anayeendesha pikipiki bila kuvaa
kofia ni sawa na mtu anayedhamilia kujinyonga.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani KAGERA ambaye
pia ni Mkurugenzi wa chuo cha udereva cha LAKE ZONE, WINSTON KABANTEGA,
amemweleza mkuu wa mkoa kuwa mwamko wa waendesha pikipiki wa kuhudhuria mafunzo
ya udereva imewajengea uwezo mkubwa na hivyo wanaendesha pikipiki kwa kujiamini
na bila woga.
Nao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo kwa nyakati tofauti
wameahidi kuzingatia mafunzo waliyoyapata ili waweze kujiepusha na ajali,
wamesema kuwa mafunzo hayo yamewawezesha kuelewa vizuri kanuni na sheria za
usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment