Friday, May 10, 2013

POLISI KAGERA YANASA VINARA WA UTEKAJI

 
Jeshi la POLISI mkoani KAGERA limekamata jumla ya watuhumiwa wa ujambazi  SABA  kati yao akiwemo mwanamke ambaye anadaiwa kuwa  ni kinara wa kupanga mipango unyanganyi wa kutumia silaha na utekaji wa magari kwenye maeneo ya mapori mbalimbali yaliyoko mkoani humo.
 
Akizungumza leo kaimu kamanda wa jeshi la POLISI mkoani KAGERA,  HENRY MWAIBAMBA  ambaye ni  kamishina msaidizi  jeshi hilo amemtaja kinara huyo wa ujambazi kwa jina la LEONCIA LOVATUS.


MWAIBAMBE amesema jeshi limefanikiwa kuwanasa watuhumiwa hao kufuatia mpango wa  muda mrefu wa jeshi  hilo wa kufuatilia mtandao wa majambazi  wanaojificha katika mapori kuteka magari na kupora mali pamoja na fedha.
 

 
MWAIBAMBE amesema   jeshi hilo limefanikiwa kukamata BUNDUKI moja aina ya SMG iliyokuwa inamilikiwa na watuhumiwa hao wa ujambazi, amesema watuhumiwa hao wa UJAMBAZI walikuwa wameifadhi bunduki hiyo kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la SABUHOLO DAUD,ilikuwa na magazini moja na risasi KUMI NA SITA.
 
 
MWAIBAMBE amesema watuhumiwa walipoojiwa walikiri kutekeleza matukioa makubwa ya uharifu ambayo ni pamoja na wizi wa utekaji wa magari na wizi wa kutumia silaha.
 
Watuhumiwa walikamatwa ni pamoja na mwanamke kinara wa kupanga mipango ya unyanganyi LEONCIA LOVAST ,SLAMBUKI ABEL, AMOS AMON, KABICHI SYLIVESTER, HANANA FRANCIS, NDANDA ILIOFU na IMAN EZEKIEL.
 

No comments:

Post a Comment