Wednesday, February 27, 2013

KIKAO CHA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA NA WADAU

 Baadhi ya maofisa wa tume ya mahakama, kutoka kulia ni Jaji Kiongozi, Fikir Jandu, Jaji wa mahakama ya rufaa Edward Rutakangwa, mkuu wa mkoa wa Kagera, kanali mstaafu Fabian Massawe na Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Bukoba, Gadi Mjemas.


 Baadhi ya washiriki wa kikao kilichoandaliwa na tume ya mahakama, aliyesimama ni mkuu wa wilaya ya Ngara, Bw. Costa Kanyasu.
 Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Bi. Ziporah Pangani alikuwa mmoja wa walioudhuria kikao hicho.
 Kulia ni mkuu wa wilaya ya Bukoba, kanali mstaafu Issa Njiku.

 Bw.Richard Kwitega aliyevaa tai nyekundu alikuwa miongoni mwa maofisa wa ofisi ya mkuu wa mkoa walioudhuria kikao hicho.
 Baadhi ya mahakimu walioudhuria kikao hicho.

Jaji wa mahakama ya rufaa akiwasilisha hoja zake wakati wa kikao.

RAIS KIKWETE ATEMBELEA JKT

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia walihudhuria.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jijini Dar es salaam alipotembelea leo February 27, 2013. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange pia wapo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya saa toka kwa  Mkuu  wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga huku  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Vuai Shamsi Nahodha, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange wakishuhudia. Saa hiyo imeandaliwa na makamanda wa JKT kumpongeza Rais Kikwete kwa kurejesha mafunzo ya jeshi la ulinzi kwa mujibu wa sheria kuanzia mwaka huu.


UZINDUZI WA MPANGO GSI

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi  wa Mpango  Mkakati  wa Miaka Mitano  wa Taasisi  ya  GSI Tanzania  kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl  jijini Dar es salaam Februari 27, 2013. Wapili kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dr.Abdallha Kigoda. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Joyce Mapunjo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mikoba katika maonyesho yaliyoambatana na Uzinduzi wa  Mpandgo Mkakati wa Miaka  Mitano wa Taasisi  ya GSI Tanzania kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es slaam Februari  27, 2013. Kushoto ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Masoko, Abdallah Kigoda na kulia ni  Katibu  Mkuu wa Wizara hiyo, Joyce Mapunjo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, February 26, 2013

MANDHALI YA CHAMA CHA MSINGI MWEYANJALE KINACHOUNDA KCU 1990 LTD

 Jengo la chama cha msingi cha Mweyanjale kinachojihusisha na kilimo cha kahawa hai 'organic coffee' kinachounda chama cha ushirika Kagera (KCU 1990 LTD).
 Mwenyekiti wa chama hicho, Leopord Mtalemwa akiwa nje ya jengo la chama hicho.
 Maeneo yanayozunguka chama hicho.
Mtalemwa akiongea na waandishi wa habari.

Monday, February 25, 2013

NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA KWAWAKA MOTO

MANISPAA ya Bukoba hapakaliki, hii inafuatia hatua ya madiwani wa manispaa hiyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kususia kikao chama hicho ambacho hufanyika kabla ya kikao cha baraza la madiwani.


Baadhi ya madiwani wa CCM wamesusia kikao hicho baada ya watu wasiofahamika kusambaza waraka unaowakashfu.


Waraka huo unawakashfu madiwani kumi ambao ni pamoja na madiwani wa CCM 8 na wa vyama vya vya upinzani vinavyowaunga mkono 2.


Mwandishi wa waraka huo anatoa kashfa nzito kwa madiwani waliosaini waraka wa kutaka Mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani apigiwe kura za kutokuwa na imani naye kufuatia tuhuma mbalimbali zinazomkabili.


Baadhi ya madiwani waliiongea walidai mgogoro ulioko kati ya Meya huyo na madiwani kuwa umeishaigawa CCM, kwa anyakati tofauti walisema kuwa hawana imani na meya huyo na ndio maana wanataka kumng'oa.


Walisema kuwa hata kama nyaraka zikisambazwa na kuwakasfu kamwe hawatarudi nyuma, "tunajua waraka huu aliyeuandaa hivyo hatuna wasiwasi nao, moto wetu uko palepale wa kumuondoa Amani madarakani" walisema bila kutaka majina yao yatakjwe.

Walisema kuwa hawataki kuongozwa na kiongozi yoyote mwenye huruka ya ufisadi ambaye anabuni miradi mingi kwa maslahi yake binafsi," Kiongozi yoyote atakayekuwa na mlengo wa kutaka kuifilisi manispaa tutakula naye sahani moja" walimaliza.


Manispaa ya Bukoba sasa kumewaka moto, pande zote zinazopingana kila mmoja anijiona ni mbabe, pande zinazopingana moja unaundwa na kundi la waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki na upande nyingine inaongozwa ana Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani.

Kambi ya Kagasheki inamtaka Meya wa manispaa ya Bukoba Amani anga'atuke na kambi ya Amani inapinga mapendekezo hayo.WAZIRI PINDA AKUTANA NA BALOZI WA CANADA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Balozi wa Canada nchini, Mhe.Alexandre Leveque kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 25, 2013. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

VIONGOZI WASAINI MPANGO WA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini  Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA IKULU


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  leo Februari 24, 2013 ameungana na Wakuu wenzake wa Nchi za  Ukanda wa Maziwa Makuu  kutia  saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe. Rais Kikwete alisema mara baada ya utiwaji saini wa Mpango huo kwamba: “Hii ni siku kubwa na ya kihistoria kwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jirani zake na Ukanda wote wa Maziwa Makuu. Ni siku ya kukumbukwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Afrika, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Jumuiya yote ya Kimataifa.
“Watu wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu sana. Wanastahili kupumua sasa. Wanastahili kuishi maisha bora; maisha ambayo usalama wao umehakikishiwa na kuthibitishwa; maisha ambayo yatawafanya waendeshe maisha yao kwa kufanya mambo ya maana zaidi katika kuboresha  maisha yao ya kila siku.
“Saini tulizotia kwa Mpango huo leo ni kielelezo cha  dhati na ahadi ya utekelezwaji wa  yale yanayotarajiwa na watu wa Kongo na Ukanda wa Maziwa Makuu kwa ajili ya Amani, Usalama na Ushirikiano.
“Kwa niaba ya Serikali na Watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naahidi kwamba sisi tutatekeleza kwa dhati yale yote yanayotarajiwa kwa upande wetu”, alisema.
Mpango huo umetiwa saini na viongozi kutoka   Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jamhuri ya Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Angola, Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kongo (Brazaville), Jamhuri ya Zambia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jamhuri ya Afrika Kusini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki-moon, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa, Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma, pamoja na wenyeviti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) wametia  saini Mpango huo kama mashahidi na wadhamini.
Mpango huo una nia ya kuchangia juhudi ambazo zimefanywa na ICGLR na SADC katika kutafuta amani Mashariki ya Kongo na ukanda wote wa Maziwa Makuu kwa ujumla.
Mpango huo pia umetilia maanani mapendekezo muhimu yaliyokubalika baada ya mashauriano kati ya wakuu wa nchi za ICGLR  na SADCna Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mapendekezo ya mpango huo ni pamoja na kuboresha sekta ya Ulinzi na usalama, hususan jeshi la polisi, Kuimarisha mamlaka ya nchi hasa mashariki ya Kongo; na kuendeleza ajenda kuhusu maelewano, kuvumiliana na kudumisha demokrasia nchini humo.
Vile vile, nchi za Kanda zimetakiwa kutoingilia mambo ya ndani ya nchi jirani, kututoa msaada wowote wa vikundi vya waasi, kuheshimu utawala na maeneo ya nchi jirani na kuimarisha mahusiano ya Kanda.
Hali kadhalika, Jumuiya ya Kimataifa imetakiwa kuisaidia DRC na Kanda yote ya Maziwa Makuu kwa ujumla katika utekelezaji wa miradi muhimu pamoja na mkataba wa Amani, Usalama na Maendeleo katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Aidha, Mpango huo unapendekeza kuwepo kwa chombo cha usimamizi (Oversight Mechanism) ambacho kitaundwa na viongozi wote wa nchi 11 pamoja na Umoja wa Mataifa, SADC na ICGLR.

Imetolewa na:
Muhidin Issa Michuzi,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Addis Ababa,
ETHIOPIA.
24 Februari, 2013

Saturday, February 23, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA IKULU


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 23, 2013 kuhudhuria utiwaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mpango huo unatarajiwa kutiwa saini kesho Februari 24, 2013 na Wakuu wa Nchi kutoka Ukanda wa Maziwa Makuu, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jamhuri ya Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Angola, Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kongo (Brazaville), Jamhuri ya Zambia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Jamhuri ya Afrika Kusini.
Aidha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe. Ban Ki Moon, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa, Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma, pamoja na wenyeviti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) watatia saini Mpango huo kama mashahidi na wadhamini.
Mpango huo una nia ya kuchangia juhudi ambazo zimefanywa na Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) katika kutafuta amani Mashariki ya Kongo na ukanda wote wa Maziwa Makuu kwa ujumla.
Mpango huo pia umetilia maanani mapendekezo muhimu yaliyokubalika baada ya mashauriano kati ya wakuu wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Imetolewa na:

Ikulu,
DAR ES SALAAM.
23 Februari, 2013

RAIS KIKWETE AWASILI NCHINI ETHIOPIA


Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 23, 2013 kuhudhuria utiwaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

PICHA NA IKULU

KATIBU MKUU KIONGOZI NA UGENI WAKE

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na Dkt Idris Jala wa kitengo cha usimamizi na utekelezaji kiitwacho PEMANDU (Performance Management and Delivery Unit) cha Malaysia na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es salaam leo Februari 21, 2013. Katikati ni Dkt Philip Mpango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.

PICHA NA IKULU

MAHAFALI YA KWANZA YA SHULE YA SEKONDARI YA JOSIAH ILIYOKO MKOANI KAGERA

 Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Josiah.
 Baadhi ya wageni walioudhuria mahafali ya kwanza ya shule ya sekondari ya Josiah, kutoka kushoto ni Bw. Mashasi anayefuata Bw. Rutabingwa.


 Wahitimu wa kidato cha sita wakiwasilisha mawazo yao kwa njia ya risala iliyosomwa na Mwanafunzi Mary Kazimoto.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera,Kanali mstaafu Fabian Massawe akiteta jambo na askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini.
 Mkuu wa shule ya Josiah sekondari,Adella Kashushula akielezea historia ya shule wakati wa mahafali.
 Padre Mrosso  na Bw.Sendwa kulia.
 Mwenyekiti wa bodi ya shule, Johansen Rutabingwa akiongea wakati wa mahafali.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, kanali mstaafu Fabian Massawe akihutubia wakati wa mahafali.

BAKWATA BUKOBA YATOA TAMKO LA MASUALA YA UDINI

 Sheikh wa wilaya ya Bukoba, Haruna Kichwabuta akielezea msimamo wa waislamu juu ya matukio ya masuala ya utofauti wa masuala ya dini nchini.
Baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wakiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISENYI

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya misenyi, William Katunzi akiwahutubia madiwani.

 Baadhi ya wakuu idara.
 Mtunza hazina wa halmashauri ya wilaya ya misenyi, Alapha Baraza na afisa habari wa wilaya hiyo, Laizer.
 Adeodatus Rugaibula, diwani wa kata ya Bukwali.

KAMANDA WAJESHI LA POLISI KAGERA AWATAHADHALISHA WANANCHI

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani kagera,Philip Kalangi akiongea na waandishji wa habari amewatahadhalisha wananchi kuwa makini na matapeli wanaouza madini feki aina ya dhahabu na almasi
 Baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi.
Dhahabu feki hizi hapa.

Wednesday, February 20, 2013

WAZIRI PINDA AKUTANA NA MWAKILISHI WA USAID

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akisalimiana na Msimamizi Mwendeshaji wa Shirika la  la Maendeleo la Marekani USAID, Dr. Rajiv Shah kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri 
 Mkuu jijini Dar es salaam Februari 20, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA AKALIA KUTI KAVU ABURUZWA MAHAKAMANI

BAADHI ya madiwani  wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wamemburuza mahakamani Mstahiki Meya wa manispaa hiyo Anatory Amani kwa kile kinachodaiwa kuwa alipeleka mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14 Dodoma bila madiwani kuijadili.

Madiwani wa manispaa hiyo waliomburuza mahakamani bila kutaja majina yao wamesema meya huyo amekiuka kanuni zinazowaongoza madiwani, wamesema hatua ya meya huyo ya kupeleka bajeti hiyo bila kujadiliwa inaonyesha jinsi gani anavyowaburuza.

Wakiongea kwa nyakati tofauti walisema sababu kubwa iliyomfanya meya huyo asiitishe kikao cha kujadili bajeti kuwa inatokana na msimamo wa madiwani wa kutaka kumng'oa, walisema alifikiri kuwa kama angeitisha kikao wadiwani wangeshikilia msimamo wao wa kumpigia kura za kutokuwa na imani naye.


Walisema alifanya hivyo kukwepa maswali ambayo angeulizwa na madiwani wanaotaka kumng'oa, waendelea kusema kuwa meya huyo atakiwi japokuwa anataka kungan'gania madaraka,"madiwani hatumtaki kabisa ndio maana anatukwepa, tutamg'oa lazima" alitamba mmoja wa madiwani wanaompinga.

"Sisi hatuna imani naye kabisa tumeishamstukia hata miradi yote anayotaka kutekeleza ndani ya manispaa ya Bukoba anaibuni kwa maslahi yake aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa soko, standi kuu ya mabasi Kyakailabwa, ujenzi wa jengo la kitega uchumi, tumeishamshtukia takuibii tena" alisema mmoja wa madiwani.

By. Furgence Ishenda

Tuesday, February 19, 2013

WAZIRI MKUU PINDA AZINDUA KIWANDA CHA KUSINDIKA PAMBA

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitama mbegu za pamba wakati alipofungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18l 2013. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti. (Picha na OFisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua kiwanda cha kusindika mbegu za pamba za kisasa  cha Quton kilichopo Bariadi Februari 18, 2013. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti  na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho, Morgan Nzwele. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS KIKWETE ATEMBELEWA NA UJUMBW TOKA SIMIYU

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 19, 2013 kumwelezea mipango ya kufungua benki hiyo itayoshirikisha jamii katika mkoa huo mpya na ya jirani katika azma ya kumkomboa mjasiriamali na mkulima
mdogo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana  na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam.

PICHA NA IKULU