Kampuni ya Simu ya Vodacom
Tanzania yajipanga kuzindua wiki ya Maadhimisho
ya Siku ya FISTULA duniani Mkoani Kagera kesho Ijumaa tarehe 17/05/2013 katika
Manispaa ya Bukoba maeneo ya Soko Kuu.
Siku ya FISTULA
huadhimishwa duniani Mei, 23 kila mwaka na kuhamasisha wahanga wa
ugonjwa huo unaotibika kujitokeza kutibiwa bure na kuutokomeza ugonjwa huo.
Uzinduzi wa wiki ya
Maadhimisho ya Siku ya FISTULA duniani mkoani Kagera umeratibiwa na Vodacom
Tanzania chini ya Meneja Uhusiano wa Nje Bwana Salum Mwalimu.
AKiongea na Katibu Tawala
Mkoa Bw. Nassor Mnambila ofisini kwake, Salum
Mwalimu alisema, uzinduzi huo unalenga kuwahamasisha wanawake wenye tatizo la
FISTULA kujitokeza ili watibiwe na matibabu ni bure.
Ugonjwa wa FISTULA
unatibiwa katika Haspitali ya CCBRT iliyopo Jijini Dar es Salaam na matibabu
hayo hutolewa bure.
Aidha kwa wanawake wenye
matatizo hayo walioko mikoani wanatakiwa kujitokeza na kuijiandikisha ambapo
watasafirishwa bure na kutibiwa bure katika hospitali hiyo.
Katika uzinduzi huo
watakuwepo wasanii mbalimbali, Mabalozi wa FISTULA (waliotibiwa tatizo hilo na
kupona) Madaktari mbalimbali na wawakilishi wa Vodacom Tanzania pamoja na
wananchi wanakaribishwa.
Vodacom Tanzania wanasaidia
na kuchangia katika matibabu ya FISTULA yanayotolewa bure katika Hospitali ya
CCBRT Dar es Salaam. Aidha, wachangia gharama za matibabu ili kumaliza tatizo
la FISTULA katika jamii kama mojawapo ya huduma zao kwa jamii ya Watanzania.
Uzinduzi huo baada ya
kufanyika rasmi mkoani Kagera kesho tarehe 17/05/2013 pia utapitia mikoa ya
Geita, Mwanza, Singida, Dodoma, Pwani na Dar es Salaam.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013
No comments:
Post a Comment