Wanafunzi Wakiwa Kwenye Maandamano Kuelekea Kwenye Uzinduzi wa Michezo ya UMISSETA Mkoani Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Mhe. Kanali Mstaafu Fabiani I. Massawe amezindua rasmi mashindano ya UMISSETA
(Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania) mkoani Kagera katika Chuo cha
Ualimu Katoke Wilayani Muleba.
Uzinduzi
wa mashindano ya UMISSETA mkoani Kagera ni maandalizi ya kushindanisha na
kubaini vipaji mbalimbali katika michezo
na kuunda timu ya mkoa wa Kagera itakayokwenda kushriki katika ngazi ya Kanda
mpaka taifa.
Mhe.
Massawe akizindua michezo hiyo alisistiza wanafunzi hao kuwa na nidhamu wakati
wote wa mashindano hayo pia na kucheza kwa mshikamano ili kuonesha vipaji vyao na kupitia huko waweze kupata ajira kama
wanamichezo maarufu wengi walivyo duniani.
Pia
Mhe. Massawe aliagiza viongozi wote mkoani Kagera kuipa kipaumbele michezo na
aliwaagiza viongozi wote wa kisiasa kuipa sana msukumo mkubwa michezo ili mkoa
wa Kagera uweze kutoa vipaji kwa wingi na kutengeneza nafasi za ajira kwa
vijana.
Aidha,
Mkuu wa Mkoa alitoa rai ya michezo mingine kuangaliwa na kupewa kipaumbele
kuliko kuendelea kusistiza aina fulani ya michezo. “Mwaka kesho ningependa
kuona michezo ya maigizo, nyimbo na ngoma za kitamaduni , michezo hiyo nayo ipewe
kipaumbele.” Alisitiza Mhe. Massawe.
Mashindano
ya UMISSETA mkoani Kagera yanashirikisha wanafunzi wa shule za Sekondari kutoka
katika Halmashauri za Wilaya za Missenyi, Karagwe, Ngara, Biharamulo, Muleba,
Bukoba na Manispaa ya Bukoba.
Jumla
ya wanafunzi wa shule za sekondari wanaoshiriki katika mashindano ya UMISSETA
mkoani Kagera ni 568, wanafunzi wa kiume 301 na wanafunzi wa kike 267.
Wananfunzi hao wanashiriki michezo ya
mpira Wa miguu, mpira wa mikono, riadha, mpira wa wavu, kuruka na kurusha tufe.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013
No comments:
Post a Comment