Sunday, September 30, 2012

WAMACHINGA WAENDELEA KUYAVAMIA MAENEO YA MANISPAA

 Wamachinga wakiwa wakiuza bidhaa zao kwenye maeneo waliyoyavamia ya manispaa ya Bukoba.
 Eneo lililovamiwa na wamachinga lililo karibu na msikiti wa ijumaa.
Wamachinga wakiuza bidhaa zao kando ya barabara ielekeayo hospitali kuu ya mkoa.

KALDINARI RUGAMBWA ENZI ZA UHAI WAKE

Mwili wa kaldinari Rugambwa utazikwa rasmi Octoba 6, Mwaka kwenye eneo la kanisa kuu la jimbo la Bukoba ambapo zaidi ya watu 40,000 wanatarajia kuhudhuria mazishi hayo.

HALI YA SASA YA KANISA KATORIKI LA JIMBO LA BUKOBA

Kanisa ambalo mwili wa marehemu kardinari Laurean Rugabwa utapumzishwa milele.

UCHAGUZI WA CCM KATAVI

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda ambaye ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM akifungua mkutano mkuu wa Uchaguzi wa  CCM  wilaya za Mlele na Mpanda mkoani Katavi kwenye Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Milala wilayani Mpanda, Septemba 30,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

RAIS KIKWETE AONANA NA UJUMBE WA MWAPORC IKULU, DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea leo Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiuonesha njia za reli katika  ramani ya Tanzania ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea leo Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli.

PICHA NA IKULU
Mgomba ulikubukwa ugonjwa wa mnyauko, ugonjwa wa mnyauko unaendelea kuhatarisha usalama wa ndizi mkoani Kagera.

Friday, September 28, 2012

Fw RAIS KIKWETE AAGANA NA MABALOZI WA CUBA NA IRAN

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Cuba  nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Ernesto Gomes Dias leo Septemba 28,  2012 Ikulu jijini DAr es salaam Dar es salaam.

Thursday, September 27, 2012

CHUO KIKUU cha St. AUGUSTINO CHAZINDUA MWAKA WA MASOMO


 Askofu Nestory Timanywa akiendesha ibada ya uzinduzi wa mwaka wa masoko wa chuo cha Mtakatifu Francis Tawi la Bukoba liliko Nkindo.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Francis.
 Askofu Nestory Timanywa askofu mkuu wa jimbo la Bukoba akisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na wahadhiri wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino wakati wa uzinduzi wa mwaka wa masomo.
Askofu Kilaini asikiliza mada, kulia ni Profesa Babyegeya na katikati ni padre Mrosso.

RAIS JAKAYA KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA KIFO CHA MEJA GENERALI KAMAZIMA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Majeshi  Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha Meja Jenerali Anatory Ruta Kamazima (Mstaafu) aliyefariki jana tarehe 25 Septemba, 2012 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Nimepokea kwa mshituko na huzuni nyingi habari za kifo cha Meja Jenerali Kamazima, ni pigo kubwa sana kwa Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Taifa kwa ujumla” Rais amesema katika salamu hizo.
Mchana wa leo Rais ameitembelea familia ya marehemu nyumbani kwao Tegeta kuwafariji wafiwa.
Marehemu alizaliwa mwaka 1946 katika kijiji cha Maruku, Mkoani Kagera. Alijiunga na Jeshi mwaka 1967, mara baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 1966.
Marehemu Kamazima amesoma kozi mbalimbali za kijeshi hapa nchini na nchi za China, India, Uingereza na Misri na kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989, aliteuliwa kuwa  Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia Rushwa Tanzania, hadi alipostaafu Juni 2003.
Rais amemuelezea marehemu Kamazima kama mzalendo na mtu aliyeipenda na kuitumikia nchi yake kwa weledi mkubwa, uaminifu na moyo mmoja.
“Nimemfahamu Marehemu kwa miaka yote ya utumishi wake jeshini na serikalini kama mzalendo, muaminifu na mwenye moyo wa kulinda nchi yake wakati wote” amesema “Marehemu Kamazima alikua mtu wa kutumainiwa sana katika nchi yetu na kamwe hatutamsahau kwa utumishi wake uliotukuka”.
“Tutamkumbuka na kumuenzi siku zote, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na tunamuombea mapumziko mema Marehemu Kamazima. Amina”.  Rais ameongeza.
Marehemu ameacha mjane, watoto na wajukuu.

Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu.
DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MKURUGENZI MKUU WA KWANZA WA TAKUKURU, MEJA JENERALI (mstaafu) ANATOLI KAMAZIMA


Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa  pole kwa mjane na ndugu wa wa Meja Jenerali Mstaafu  Anatoli Kamazima leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia  leo Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 utokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU

PINDA AAGANA NA BALOZI WA CUBA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Cuba  nchini, Ernesto Gomez Diaz ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijiniDar es salaam kuaga , Septemba 26, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UZINDUZI WA TIGO MAMA AFRIKA SARAKASI WAFANA JIJINI DAR...!!!


Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo akizungumza machache katika ufunguzi wa maonyesho ya Tigo Mama AfriKa sarakasi yanayoendelea katika ukumbi wa ukumbi wa Mancom ndani ya Centre New World Cinema Mwenge. Maonyesho hayo yanaendelea mpaka ifikapo Oktoba 4, 2012.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez akieleza machache kwa wageni waliokuwa wamefika katika maonyesho hayo.

Mkurugenzi wa Mancom Centre, Constantine Magavilla akiwakaribisha na kuwashukuru wageni waliokuwa wamefika katika uzinduzi wa Tigo Mama Afrika Sarakari.

Moja ya michezo iliyovutia katika Tigo Mama Africa Circus inayoendelea katika ukumbi wa Mancom ndani ya Centre New World Cinema Mwenge.

Huyu kijana anauwezo wa kuendesha baiskeli ya tairi moja.

... ilikuwa ni maajabu na kweli.

Kijana mwingine alionyesha umahili wake ni huyu kama vile unavyomuona.

Michezo ya kamba nayo ilikuwa ya kuvutia.

Mchezo mwingine ulikuwa niwa kurushiana vikapu ya kutimia miguu.

Vijana wakionyesha uhodari wao wa kupaa juu.

Vijana wakiaga mara baada ya onyesho kumalizika.

Wanamuziki wa Bendi ya Inafrika nao wakiaga, kazi yao kubwa ilikuwa ni kusherehesha wakati vijana wakiendelea na onyesho.

Umati mkubwa wa watu uliojitokeza katika maonyesho hayo.

watu walipata fulsa ya kubadilisha mawili matatu. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa www.kajunason.blogspot.com

Tuesday, September 25, 2012

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiteta katika kikao chao kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Septemba 24, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM kwenye  ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Septemba  24, 2012. Kushoto ni Rais wa Zamnzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Kulia ni Makamu mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, September 24, 2012

Morning Jogging In Mbeya City!

Nimekimbia mchakamchaka ( Jogging) asubuhi hii kutoka Mwanjelwa hadi katikati ya Jiji la Mbeya. Ni umbali wa kilomita saba hivi. Niliporudi nimepita barabara mpya ya Mkapa mpaka Soko Kuu Mwanjelwa. Mbeya inapendeza na kila ninapokuja naiona inakua. Kuna ya kuandika zaidi. Nitafanya hivyo baadae. Kwa sasa najiandaa kwenda kutoa mafunzo ya Online Journalism kwa wanahabari wa Mkoa wa Mbeya na wilaya zake. Siku njema.
 Maggid,