WAKATI baadhi ya madiwani wa halmashauri ya manispaa
wanajiandaa kwenda mjini Dodoma kumuona waziri
mkuu Mizengo Pinda kwa lengo la kumshtaki mstahiki meya wa manispaa
hiyo, Anatory Amani nao baadhi ya
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
katika manispaa hiyo wameandaa mpango kurudisha kadi za uanachama wa chama hicho
kufuatia kukerwa na kauli zinazotolewa
na meya huyo mara kwa mara.
Wanachama hao wamedai kuwa meya huyo anatakiwa kujiuzulu kwa
kuwa miradi yote ya maendeleo ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko jipya na
upimaji wa viwanja 5,000 kuwa anaibuni kwa maslahi yake binafsi.
Kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamekasirishwa na kauli
zake alizozitoa wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika siku ya
ijumaa iliyopita ya kutumia lugha ya matusi, na pia kuuelea umma kuwa mgogoro
kati yak e na wananchi na baadhi ya madiwani wanaompinga umeisha.
Katika kikao hicho Amani aliwambia madiwani kuwa
ameishakutana na waziri mkuu hivyo tume iliyoundwa kumchunguza haikubaini
tuhuma yoyote inayomkabili.
Meya huyo alichowashangaza wananchi katika kikao hicho
alisema ujenzi wa soko jipya la Bukoba utaendelea kama kawaida, walisema kauli
aliyoitoa inaingili uhuru wa mahakama kwa kuwa wafanyabiashara ndani ya soko
hilo walishafungua kesi ambayo inaendelea kusikilizwa na Mahakama kuu.
No comments:
Post a Comment