Wednesday, May 29, 2013

MUHANDIKI AUMBULIWA

WAJUMBE  wa mkutano mkuu wa  Chama Cha Ushirika KAGERA (KCU) kwa pamoja wamepitisha hoja ya kumfukuza uanachama wa chama hicho ALKAD FELICIAN  MUHANDIKI ambaye  ni mwenyekiti wa chama cha msingi cha KAMACHUMU moja ya vyama vinavyounda ushirika huo kufuatia tuhuma zinazomkabili ya kupanga mikakati ya kutaka kukisambaratisha na kuwagawa wanachama.
 
Uamzi wa kumfukuza MUHANDIKI ulifikiwa na wajumbe hao wwakati  wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya BUKOBA COOP inayomilikiwa na chama hicho cha ushirika  iliyoko katika manispaa ya BUKOBA.
 
Katika kikao hicho wajumbe wa mkutano huo mkuu walipiga kura za kutokuwa na imani MUHANDIKI, baada ya wajumbe kupiga kura hizo walimuomba  mwenyekiti wa KCU, JOHN BINUNSHU amuondoe ndani ya ukumbi wa mkutano kwa madai kuwa anakisaliti chama hicho cha ushirika.
 
 
Katika kikao hicho mkuu wa wilaya ya BUKOBA, Bi. ZIPORAH LION PANGANI pamoja na kusikitishwa na tabia ya baadhi ya wanachama wa chama hicho ya kutaka kukisambaratisha, alikemea pia tabia ya watu wanaojihusisha na biashara ya kuuza kahawa nje ya nchi kwa njia ya  magendo.
 
 
Kwa upande wake meneja mkuu wa  Chama cha Ushirika cha Mkoa wa KAGERA(KCU) ,VEDASTO NGAIZA katika kikao hicho amesema chama hicho kimekusanya asilimia THEMANINI ya MALENGO ya zao la KAHAWA kwa msimu uliopita wa mwaka 2012/2013 .
 
Amesema KCU ilikuwa  ilijiwekea malengo ya kukusanya jumla ya tani ELFU KUMI NA TANO, lakini chama kimekusanya  jumla ya tani ELFU KUMI NA MOJA ikiwa ni asilimia THEMANINI kutokana na baadhi ya changamoto ambazo anazibainisha kuwa ni pamoja  ushindani uliopo wa ununuzi wa kahawa kati ya chama hicho na wanunuzi binafsi wenye mitaji mikubwa.
 
Taarifa ambazo zimepatikana zinadai kuwa mhandiki alikuwa anawania nafasi ya uenyekiti wa KCU akaenguliwa kwa kukosa sifa.
 

No comments:

Post a Comment