Mfanyakazi mwenye asilia ya kiasia wa kampuni inayojihusisha
na uuzaji wa mafuta ya ABOOS iliyoko mjini BUKOBA, HAMADI ALI MOHAMED amefikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kumuibia mwajili wake RAZA FAZAL
zaidi ya shilingi milioni 526.9.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa leo mahakamini kusomewa tuhuma zinazomkabili mbele ya hakimu
mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya BUKOBA , Mheshimiwa CHARLES UISO.
Mwendesha mashitaka ambaye pia ni wakili wa serikali PAUL
KADUSHI akisoma mashitaka yanayomkabili mbele ya hakimu huyo amesema mtuhumiwa
anadaiwa kumuibia kiasi hicho cha fedha mwajili wake kwa nyakati tofauti kati
ya mwezi JANUARI hadi DESEMBA mwaka
2010.
Mtuhumiwa huyo alikana mashataka yote aliyosomewa, pamoja na
dhamana kuwa wazi mtuhumiwa huyo alikosa
watu wa kumdhamini hivyo alipelekwa gerezani,
kesi ya mtuhumiwa huyo itatajwa tena juni 23, mwaka huu.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana na jeshi la polisi mkoani
KAGERA lililokuwa likimsaka wakati akiwa
kwenye harakati za kutoroka kuelekea nchi jirani ambayo haikubainishwa.
No comments:
Post a Comment