Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.
Hapa
Afrika kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa
ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi
ya kupigiwa mfano. Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande.
Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni
ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana.
Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini
kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast
wanaotokea Kusini.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa
wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani. Lakini
leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu
ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Naomba
nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na
hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya
Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4
Novemba, 1998. Alisema:
“Mr.
Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the
words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is
a good country, let one who wishes to come do so. God has showered
blessings on our country. It is a country of unity, peace, love,
rejoicing and exciding generosity. It is a country of people who love
equality and justice. Our national unity brings from our firm believe
in equality of human beings before God and before the Law. A Unity
reinforced by correct policies of national building. Policies based on
the principles of social justice, peace, harmony and development for
all. A unity which is extra
sensitive to policies, statements behavior and actions which may sore
seeds discard hatred and suspicious among Tanzanians”
Mheshimiwa
Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo
Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia
maneno haya tena? Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu leo
kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa
ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi
na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka pamoja tumejikuta
tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni
“irresponsible” vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni
matumizi ya nyufa hizo.
NDUGU KABWE Z. ZITTO
Asubuhi
hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo
wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya
vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini. Wametoa mfano
kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano
kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-“point fingers” kwa
wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha
waislam ambao walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam hawakunyoosha
mkono kupinga. Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi
hivyo hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu kubwa
sana katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili tuseme
kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni
rahisi kamba kukatika. Tumeji-“expose”, tumejiweka wazi. Leo mtu
anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu
anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana
limetokea tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja
watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu
wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo
tumeifikia; na ndio anachokitaka adui. Ni hicho. Atakuja, wanaitwa
“Agent Provacateur”, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu
NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja
tusimame imara.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu
wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano
waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma
makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo
ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye
magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila
kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na
wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi
viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni “very irresponsible” tunawagawa watu
wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?
Mheshimiwa
Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge
utamaduni wa kufuatilia “grievances” zote ambazo wananchi wanazo bila
kujali dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema. Nimesikia hapa
watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si
tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya
nini? Atatoka na bomu. Turuhusu “honest discussions” miongoni mwetu
kama wananchi.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa na
kauli za chuki “hate speeches”. Kama hatuna vipengele vya kisheria
tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na “hate speeches” nyingi sana katika
hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za
uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama
ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka
mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii
Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita
BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya
waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni
chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye
uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha
kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi
hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au
ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya
Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania. Lazima wote tusimame kuhakikisha
tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante.
No comments:
Post a Comment