Sunday, March 15, 2015

MAKANISA YA KIKIRISTO YAENDELEA KUCHOMWA MOTO KAGERA



NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA +255 784 939 586/ 753 844 995

Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya uchomaji moto  makanisa unaofanywa na watu wasiojulukana katika maeneo mbalimbali yaliyoko mkoa wa kagera, jeshi la polisi mkoani kagera  limeanzisha  operation maalumu kwa lengo la kuwabaini wanaojihusisha na vitendo hivyo.
Jeshi hilo limelazmika kuanzisha  operation hiyo maalumu kufuatia matukio mawili yliyofuatana ya  uchomaji wa moto makanisa  katika manispaa ya BUKOBA, akizungumza na waandishi wa habari leo ofisi kwake,HENRY MWAIBAMBE, kamanda wa jeshi hilo mkoani humo , ameyataja makanisa yaliyochomwa  moto kuwa ni pamoja na kanisa la wakatoriki Lililoko katika kata ya KAGONDO na lile la dhehebu la PENTEKOSTE lililoko eneo la KYABITEMBE lililochomwa usiku wa kuamkia leo.


Katika hatua nyingine  kamanda huyo amesema jeshi hilo linawashikilia watu KUMI na SABA kwa tuhuma ya kujihusisha na vitendo vilivyokithiri katika manispaa ya BUKOBA vya kuwaua watu kwa kuwakata na  mapanga kichwani na kuondoka na baadhi ya viungo vyao ni pamoja na MAKOROMEO, pia amesema kwamba jeshi hilo linawashikilia waganga ya jadi KUMI na NANE kwa tuhuma ya kujihusiha na vitendo vya upigaji wa LAMLI chonganishi.



Katika hali isiyo ya kawaida mmoja wa  waganga  jadi wanaoshikiliwa na jeshi hilo amepandisha MASHETANI  huku akitoa ishara mbalimbali za kiganga baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi kama anavyoonyesha hapa. huku mmoja wa waganga akikana  kuhusika na tuhuma zilizoelekezwa kwao za upigaji wa LAMLI.


Vitendo vya uchomaji wa makanisa vimeendelea kukithiri katika manispaa ya BUKOBA tangu mwaka jana hadi sasa jumla ya makanisa MATANO katika manispaa hiyo yameishachomwa na watu wasiojulikana, pia katika manispaa hiyo zaidi ya watu KUMI wameishauawa kufuatia wimbi la mauaji linalofanywa na watu wasiojulikana ambao utekeleza  mauaji kwa kuwakata kata watu mapanga na wakati mwingine kuondoka na sehemu za viungo vya vya mili hususani makoromeo.


No comments:

Post a Comment