Monday, December 31, 2012

MAMBO YA MKESHA WA MWAKA MPYA

 Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian Massawewa tatu toka kushoto akicheza nyimbo za dini sambamba na baadhi ya viongozi wa dini wakati wa mkesha wa sherehe ya mkesha wa mwaka mpya wa mwaka 2013.
 Baadhi ya walioudhuria mkesha wa mwaka mpya.
 Msanii akitumbuiza wakati wa sherehe ya mkesha wa mwaka mpya iliyoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Kagera iliyofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Kaitaba.


MAMBO YA WASANII

Wasanii wa muziki wakiwa na mmiliki wa mtandao huu, Audax Mutiganzi.

MAREHEMU ABOOD MOHAMED ABOOD AZIKWA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib  Bilali, Makamu wa Pili wa Rais Wa Znzibar Balozi Seif Iddi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 29, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam leo Desemba 29, 2012.

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI PADRE MKENDA

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali  Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii  wakati akisubiri kufunguliwa geti  la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.

PICHA NA IKULU

WAZIRI WA UTAMADUNI, VIJANA NA MICHEZO Bi. MKANGARA MKOANI KAGERA

 Waziri Akikagua Shamba la Migomba.
Waziri Akiwa Kemondo Katika Kukagua Kikundi cha Vijana Wajasiliamali Wanaofuga Samaki na Wanawezeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

Sunday, December 30, 2012

Utajiri wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Tusipuuze

Maandamano ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya alhamis wiki hii yameibua hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi, vyombo vya habari na mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook, twitter na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji wapuuzi na Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba udhaifu wa utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.
Lakini kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo katika sekta hii tu bali pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake katika maisha ya watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera za CCM. Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM wanaanza kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa Watanzania wamefungua macho yao na wanaona.
Wanaona katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona katia elimu (kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya, wanaona katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea kushindwa.
Mtwara na Lindi wanataka nini?
Watu wa Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake viwanda na mitambo ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe kupelekwa sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara usambazwe nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima. Wanataka Bandari ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la hasha.
Sio dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala haya. Watu wa Mtwara wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali na kutoa maoni yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa nini tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa Afrika kiasi cha kuwa katika hatari kabisa? Tumesahau ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara na Lindi dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa Korosho imekuwa zao kubwa la biashara na linaloingiza mapato mengi sana ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo anasema Mtwara warudishe Fedha za Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za Korosho? Mwaka 2011 Korosho ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni baada ya Tumbaku.
Lakini tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za Mkonge? Walifaidi fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau hata Reli iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali huru ya Tanzania?
Tujiulize zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na Mgodi wa Resolute pale Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu ya thamani ya dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu Serikali Kuu imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana Haki kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye Gesi asilia.
Mtwara na Lindi wanakosea wapi?
Madai yao halali na mimi binafsi na chama changu tunayaunga mkono. Lakini kuna mahala lazima waelimishwe.
Watu wa Mtwara pia wanapaswa kuelewa kuwa juhudi zao zisiwatenganishe na Watanzania wengine kwani bado utajiri wa Taifa unafadisha kikundi cha Watanzania wachache sana. Watu wa Mtwara wanahitaji kuungana na watu wa Mara, watu wa Mwanza, watu wa Shinyanga na watu wa Kagera kudai utajiri wa nchi utumike kwa maendeleo ya watu badala ya kunufaisha kundi dogo la watu. Watu wa Mtwara wanapaswa kuunganisha nguvu na Watanzania wengine kuzuia uporaji wa rasilimali ya nchi dhidi ya kizazi kijacho. Watu wa Mtwara wasijitenge wakawa peke yao na Gesi yao. Nguvu ya mnyonge ni umoja.
Serikali isiyosikia
Serikali ina hoja kuhusu kujenga Bomba la Gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa gharama nafuu. Umeme unaotumiwa na asilimia 14 tu ya Watanzania. Kwa kuwa hii asilimia 14 ndio wenye sauti basi watu wa Mtwara wataonekana hawana hoja kabisa. Lakini Serikali imejiuliza mara mbilimbili kuhusu mradi huu wa Bomba? Tunaambiwa na Wataalamu kwamba kuna uwezekano mkubwa mwakani gesi asilia ya kiasi cha futi za ujazo trillioni 20 itakuwa imegunduliwa katika Kitalu namba 7( block 7) ambacho kipo mkoani Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke. Iwapo gesi nyingi hivi itakuwa hapa Dar karibu kabisa na mitambo ya kuzalisha umeme, mradi huu wa Bomba unaojengwa kwa trillioni za shilingi utakuwa na maana tena? Huu mkopo utakuwa na tija?
Serikali imewaambia watu wa Mtwara gharama za kuleta bomba Dar dhidi ya gharama za kujenga mtambo wa kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha umeme kwenda maeneo mengine ya Tanzania? Serikali imeangalia faida ya kujenga gridi nyingine badala ya kuwa na gridi moja tu yenye kushikwa na bwawa la Mtera? Leo bwawa la Mtera lisipozalisha hata megawati moja hata Dar es Salaam izalishe megawati alfu kumi umeme hautakuwapo maana uti wa mgongo wa gridi ni Mtera! Kwa nini tusiwe na gridi nyingine yenye uti wa mgongo Lindi au Mtwara?
Tuwasikilize watu wa Mtwara
Watanzania sio mabwege tena. Kuwaita watu wa Mtwara ni wahaini, wapuuzi au watu hatari haisaidii kujenga Taifa moja lenye watu huru. Serikali na wadau wote wa sekta ya Gesi likiwemo Bunge washirikiane na watu wa Mtwara kuhusu miradi ya gesi asilia. Tuwe na Azimio la Mtwara, tamko la kuelekeza namna bora ya kutumia utajiri wetu wa Gesi bila kuathiri umoja wa Taifa letu.
Ujio wa Sera, Maono na Uongozi Mbadala
Sasa hivi wananchi wa Mtwara kama wananchi wa sehemu nyingine wanahitaji maono mbadala, uongozi mbadala, sera mbadala na mwelekeo mbadala wa kitaifa ambao utaangalia mahitaji yao, utazingatia raslimali zilizopo na utaunganisha utendaji wa sekta mbalimbali katika kutengeneza mfumo wa kiutawala na kiuchumi ambao utaliinua taifa zima.
Ni kwa sababu hiyo naamini chama changu ni jibu sahihi kwa matamanio na kiu ya wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine nchini. Ikumbukwe kuwa katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya 2010 tulielewa haja ya kuangalia mikoa hii ya Kusini kwa namna ya pekee na kuipa mwelekeo wa kipekee katika sera.  Bado tuna makusudio hayo tunapoelekea 2015 na tukishika Dola wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine zote zilizoachwa pembezoni mwa mafanikio wajue kuwa wamepata rafiki na mshirika wa karibu wa kushirikiana nao kuleta maendeleo.
Siyo katika suala la gesi tu bali katika nishati, maji, elimu, miundombinu, kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii. Mtwara kama ilivyo mikoa mingine ina raslimali za kutosha kuweza kuwainua wananchi wake kimaisha, na zaidi ya yote kutoa mchango mkubwa wa kiuchumi. Hili ambalo ni kweli kwa Mtwara ni kweli kwa mikoa mingine kama Kigoma, Manyara, Katavi, Lindi n.k.
 
zittokabwe | December 29, 2012 at 10:57 AM

Friday, December 28, 2012

RAIS KIKWETE ASHEREKEA SIKUKUU YA KRISMAS ARUSHA

 Nahodha wa hoteli ya Seronera Jamali Kitonga akifurahia baada ya kukabidhiwa kombe la Ujirani mwema na Rais Jakaya Kikwetebaada ya timu yake kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara leo Hasdi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiikagua  timu ya hoteli ya  Serena  kabla ya kucheza na hoteli ya Four Seasons Safari Lodge katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara. leo hadi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.

PICHA NA IKULU

Thursday, December 27, 2012

ZIARA YA WAZIRI MUKANGARA MKOANI KAGERA

 Baadhi ya maofisa wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na waziri wa elimu, vijana, utamaduni na michezo Fenella Mukangara  alipokuwa kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera, kanali mstaafu Fabian Massawe.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera Fabian Massawe akisikiliza maelezo toka kwa waziri Mukangara.
 Afisa elimu wa mkoa wa Kagera Florian Kimolo akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na waziri Mukangara.

Tuesday, December 25, 2012

MAMBO YA USIKU WA CHRISMAS KATIKA MANISPAA YA BUKOBA

 Msanii anayeimba mwenyewe na kupiga gitaa moja Nimrod Mwamezi akitumbuiza kwenye ukumbi wa hoteli ya Coffee tree iliyoko katika manispaa ya Bukoba.
Baadhi wakisakata mziki uliokuwa ukitumbizwa na msanii Mwamwezi.

MAMBO YA SHAMLASHMLA ZA KUSHEREKEA SIKUKUU YA KRISMAS MKOANI KAGERA

 Wakazi wa manispaa ya Bukoba wakisherekea sikukuu ya krismas kwenye ufukwe wa ziwa victioria uliko maeneo ya hoteli ya Spice.
 Hapa wanaonekana wakila na kunywa.
 Watoto wakiogelea kwenye ufukwe wa ziwa victoria, eneo hili huwa maarufu sana wakati wa sherehe za sikukuu za kidini na mwaka mpya.
 Wadau wa mtandao huu, kulia ni Ayesiga Rugalabamu, na kushoto ni Ivan Kalumuna Rugalabamu.
Mmoja wa wabia wa mtandao huu wa kijamii, Margareth Rugalabamu, naye alikuwa miongoni mwa waliosherekea sikukuu ya krismas  kwenye maeneo ya ufukwe wa ziwa Victoria.

Monday, December 24, 2012

KIKWETE ATOA MILIONI 30 KWA AJILI YA KUWALINDA NA KUWAHIFADHI MBWA MWITU

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  wakielekea kwenye sehemu ya boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu muda mfupi kabla ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  akikata utepe katika boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu  kuashiria rasmi kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. 
Mbwa mwitu wakirejea mbugani baada ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

MKUU WA MKOA KAGERA ATOA MISAADA KWA MAKUNDI YASIYOJIWEZA


 Massawe akitoa zawadi kwa kikundi cha kulea watoto yatima cha Nusuru yatima.

 Bi. Saada Suleimani wa kikundi cha uyacho akipokea msaada wa mbuzi toka kwa mkuu wa mkoa, hiyo ilikuwa nki zawadi ya Kristmas.

JESHI LA POLISI KAGERA LATHIHIRISHA LINAVYOTEKELEZA WAJIBU

 Baadhi ya vitu vilivyokamatwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kufuatia operation mbalimbali lililoziendesha kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani humo, vitu hivyo ni pamoja na viungo vya wanyama mbalimbali vikiwemo meno, pembe na ngozi, bunduki aina ya SMG na risasi zake, pesa bandia na kamba zinazotumiwa na waharifu kutekeleza uharifu, pia kufuatia msako huo zaidi ya bunduki 15 zilizokuwa zinamilikiwa kinyume na sheria zilisalimishwa.
 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi, akionyesha bunduki aina ya SMG iliyokamatwa kufuatia operation iliyoendeshwa na jeshi la polisi mkoani Kagera iliyopendeshwa na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Kagera (kukia) Mwaibambe.


 Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, Mwaibambe akionyesha pembe za wanyama mbalimbali zilikamatwa na jeshi la polisi kufuatia msako lililouendesha.

Silaha mbalimbali zilizosalimishwa kwa hiari kufuatia operation ya jeshi la polisi.

Sunday, December 23, 2012

MAMBO YA UZINDUZI WA ALBAMU YA YESU MWEMA ULIOFANYWA NA KAPOTIVE STAR SINGERS UKUMBI WA LINA'S

 Familia ya Dr. Kalumuna ilikuwa miongoni mwa walioudhuria uzinduzi wa albamu ya yesu mwema uliofanywa na kundi la Kapotive star singers uliofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya Linas ulioko mkoani Kagera katika manispaa ya Bukoba.
 Askofu msaidi wa jimbo la Bukoba akibadilishana mawazo na baadhi ya watu kabla ya uzinduzi wa albamu ya yesu mwema.
 Kwaya ya kanisa katoriki ya kikango cha Rwamishenye ikitumbuiza kabla ya  uzinduzi wa albamu ya yesu mwema.
 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya utalii ya Kiroyera, Mary Kalikawe alikuwa miongoni mwa walioudhuria uzinduzi wa albamu ya yesu mwema, anaonekana akijadiliana jambo na mmoja wa marafiki zake.
 Kwaya ya vijana ya kanisa la kiinjili la kirutheri la diosisi ya kaskazini magharibi ikitumbuiza.


 Kikundi cha kwaya cha kanisa la SDA nacho hakikubaki nyuma wakati w uzinduzi wa albamu hiyo.
 Kikundi cha nyimbo za injili cha The Groover toka nchini Uganda kinachoongozwa na Padre Antony Musaala kikifanya vitu kabla ya uzinduzi wa albam, padre Musaala aliwakuna watu alipoimba wimbo unaotamba wa injili wa ampeche a mgongo.
 Padre Musaala akiimba sambamba na walioudhuria uzinduzi wa albamu.
 Akiimba sambamba na kundi zima la Kapotive star singers.
 Kundi la Kapotive star singers likifanya vitu wakati likitambulisha albamu kiliyoizindua rasmi ya yesu Mwema, uzinduzi wa albamu hiyo ulifanyika jana, kwenye ukumbi wa klabu ya linas na kuhudhuliwa na maelfu ya watu.
 Mambo ya kundi la Kapotive star Singer, kundi hili linaitaji zaidi ya shilingi zaidi ya milioni 32 kwa ajili ya kufanikisha shughuli yake ya kurekodi albamu mbalimbali kinachotaka kusisambaza, usiku wa uzinduzi wa albamu jumla ya shilingi zaidi ya milioni 15 zilipatikana.