Thursday, January 31, 2013

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KABILA WA JAMHURI YA DEMKORASIA YA KONGO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii ya Januari 30. 2013

Wednesday, January 30, 2013

Dr. DIODURUS KAMALA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MBOLEA.

 Dr. Diodorus  Kamala (Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Daniel RICHIR Chief Executive Officer wa kampuni ya Rosier na Raphael De RIJCKE General Sales Manager wa kampuni ya Rosier.  Kampuni ya Rosier ni kampuni kubwa inayozalisha mbolea hapa Ubelgiji na na sehemu ya mbolea inayozalishwa na kiwanda hicho inauzwa nchini Tanzania.

 Dr Kamala ameushukuru uongozi wa kiwanda hicho kwa kazi nzuri wanayofanya na pia ameuomba uongozi wa kiwanda hicho kuwatuma watalaamu wake nchini Tanzania ili waweze kuyafanyia utafiti  mazao mbalimbali, udongo na hali ya hewa ya maeneo mbalimbali ya Tanzania.

 Kampuni hiyo imekubali kutuma wataalam Tanzania ili kufanya utafiti utakaosaidia kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula. Balozi huyo alitembelea  kiwanda hicho jana. Kwa sasa kiwanda hicho kinauzia mbolea Wazalishaji wa Tumbaku . Kiwanda hicho kilianza uzalishaji wa mbolea mwaka 1830, Kinazalisha mbolea za aina mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya mteja.

Tuesday, January 29, 2013

PINDA AKUTANA NA WAFANYBIASHARA KUJADILI MGOGORO WA GESI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wafanyabiashara wa Mtwara kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara, Januari 28, 2013. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAHADHALI YA MVUA KUBW KWENYE MAENEOMENGI TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Simu pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 29 Januari, 2013
Taarifa kwa umma: Uwezekano wa matukio ya mvua kubwa
Taarifa Na. 20130129-02
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 12:00 Jioni
Daraja la Taarifa:
1:Taarifa 2:Ushauri
3:Tahadhari
4:Tahadhari Kubwa:
Ushauri
Kuanzia:
Tarehe
30 Januari, 2013
Mpaka:
Tarehe
01 Februari, 2013
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila
siku)
Kiwango cha uhakika: Wastani
Maeneo yatakayoathirika
Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe,
Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara na maeneo jirani na
mikoa hiyo.
Maelezo:
Kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa
Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu
kutoka Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo:
Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu
wanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika
na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho
na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

PICHA YA SATELITE INAYOONYESHA JINSI MVUA ITAKAYOSABABASHWA NA KIMBUNGA


Ndugu zangu wananchi jiandaeni kuna dalili za mvua kubwa, picha hii imetolewa na idara ya hali ya hewa.

Monday, January 28, 2013

WAZIRI MKUU PINDA AANZA MKAKATI WA KUMALIZA MGOGORO MTWARA

  Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Mkoani Mtwara, Askofu, Chilumba akiomba  kabla ya kuanza kwa kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wa madhehebu ya dini  ya Kikristo mkoani Mtwara kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukmbi wa VETA mjini Mtwara Januari 18, 2013. Jana Mheshimiwa Pinda alikutana na Viongozi wa dini ya Kiislam mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  viongozi wa madhehebu  ya Kikristo kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA  mjini Mtwara, Januari 28, 2012.Jana Mheshimiwa Pinda  alikutana viongozi wa dini ya Kiislam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NDEGE YA PRECISION AIR YAKWAMA KAGERA

Ndege ya shirika la Precision Air aina ya ATR ambayo hutua kwenye viwanja mbalimbali vilivyoko hapa nchini imekwama kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kufuatia uwanja huo kujaa matope kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Kagera hali iliyosababisha hofu kwa abiria.

Hali ya kukwama kwa ndege hiyo kwenye matope  iliwatia hofu abiria walikuwa ndani ya ndege hiyo jambo ambalo liliwalazimu kila abiria aanze kusali kulingana na dhehebu lake mmoja wa waliounusurika na ajali hiyo alisema.

Habari zinadai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni rubani ambaye kuiendesha  ndege hiyo kwa mwendo kasi  wakati akijua sehemu ya uwanja huo inafanyuiwa  ukarabati.

Kufuatia hali hiyo abiria walikuwa ndani ya ndege hiyo walilazimika kuvua viatu kwa ajili ya kushika ndani ya ndege hiyo ambayo ilikuwa tayari imekwama kwenye matope.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo blog hii imezipata ni kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es salaam, ambapo kufuatia ajali hiyo ilisitisha safari kwa muda na baadae  kuondoka kwenye uwanja wa Bukoba majira ya usiku.


Ndege hiyo ilikwamuliwa katika tope hilo baada ya kuvutwa.

Sunday, January 27, 2013

WAZIRI MKUU PINDA MKONI MTWARA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunguma na Maimamu wa mkoa wa Mtwara kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa veta mjini Mtwara Januari 27, 2013. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

TAARIFA YA NDUGU ZITTO KABWE (MB) KUHUSU YANAYOENDELEA MTWARA NA MRADI WA BOMBA LA GESI ASILIA


Serikali iache kutafuta mchawi, iende Mtwara

Katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamamo, malumbano na vurugu kuhusu mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa kilometa 542 ni mkubwa sana hapa nchini, na una thamani kubwa zaidi kuliko miradi mingine yote  ya miundombinu iliyopata kutokea hapa nchini. Mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola za Kimarekani 1.2 bilioni kutoka Benki ya Exim ya China.

Wananchi wa Mtwara kupitia maandamano ya tarehe 27 Desemba 2012 wametaka kujua hatma ya maendeleo ya mikoa wa kusini kutokana na mradi huu wa bomba la gesi. Serikali imewajibu wananchi hawa kwa kuwaita wahaini, watu hatari na wasio elewa. Imefika mahali inapotosha madai yao kwamba hawataki gesi itoke Mtwara.

Kimsingi Serikali haijajibu hoja yeyote ya msingi ya wananchi wa Mtwara kuhusu mradi wa kusafirisha gesi. Badala yake imekuwa ikijaribu kupotosha madai ya watu wa Mtwara kupitia mikutano na vyombo vya habari.

Tangu maandamano haya yatokee, na baadaye mikutano ya hadhara na
hatimaye matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji ya
watu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara yenye dhamana ya
mradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya
kwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona
namna ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo,
kusikiliza na kuzungumza na wananchi wa Mtwara, vurugu mbaya sana zimeendelea mkoani humo.

Mwezi uliopita, Desemba 2012, tatizo lilionekana kuwa ndogo na lenye kuhusiana zaidi na ukosefu wa kushirikishwa kwa wananchi. Badala ya kushughulikia
tatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro
huu.

Leo hali iliyopo mkoani Mtwara inasikitisha sana, maana mali za wananchi zinaharibiwa, nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha. Tunalaani matukio haya kwa nguvu zetu zote, maana kinachotokea Mtwara si Utanzania. Tusipowasikiliza wananchi na kutatua mgogoro huu kwa kuwashirikisha, hali itazidi kuzorota wakati tukitupiana lawama.

Hivi sasa serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisema kuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro huu.

Kwanza, Serikali imekuwa ikiaminisha umma kwanza suala hili limechukuliwa kisiasa. Pili, Serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa baadhi ya makampuni ya uwekezaji nchini na mataifa ya Magharibi yamekuwa yakichochea wananchi wa Mtwara.

Katika mwendelezo wa mtindo wa Serikali wa ‘management by press conferences’ jana Jumamosi Naibu Waziri wa Nishati na Madini ndugu George Simbachawene aliwaambia wahariri kwamba mimi Zitto Kabwe ninachochea wananchi wa Mtwara, ninatumiwa, na si mzalendo. Vile vile alitoa vielelezo kadhaa kuonyesha kuwa mradi wa kujenga bomba la gesi ni gharama sawasawa. Akasisitiza kwamba mimi ni mwongo.

Katika kipindi chote cha mgogoro wa Gesi Mtwara, sijafika Mtwara. Sijafanya mkutano wowote na waandishi zaidi ya kuandika mawazo yangu, kama Mtanzania kuhusu suala hili.

Nimeandika makala nne na zimechapishwa katika magazeti kadhaa hapa nchini na kwenye blogu yangu (http://zittokabwe.wordpress.com/).


Sitaki kubishana na Naibu Waziri ama Kiongozi yeyote ya Serikali kwa sasa. Hatuwezi kuendelea kulumbana, kuzozana, kuzodoana na kurushiana maneno wakati nchi yetu inaungua. Huu sio wakati wa kutafuta mchawi bali kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo mbele yetu.

Yanayotokea Mtwara ni fundisho kwetu kwa Taifa namna ya kukabili changamoto za utajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati, mambo haya yanayotokea Mtwara yasitokee tena Tanzania. Tutaweza kuzuia maafa haya iwapo tutaweka uwazi katika mikataba, tutashirikisha wananchi kwenye unyonyaji wa maliasili za nchi, na iwapo tutaweka uwajibikaji.


Rais Kikwete Kikwete ana majibu; ayatoe sasa kwa wana Mtwara

Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power System Master Plan), kulikuwa na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais Jakaya Kikwete aliagiza utekelezwe mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi huo wa kujenga kituo cha kufua umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga msongo wa umeme wa 300KV mpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 12 Oktoba 2012, Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya ujenzi wa mradi huu kutoka makampuni ya China National Machinery & Equipment Import & Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola za kimarekani milioni 684 na Rais aliagiza utekelezwe haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini Serikali ipo kimya kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa Mtwara? Taarifa ya Ikulu kuhusu mradi huu imeambatanishwa hapa.

Tufanyeje?

Hapa tulipofikia ni lazima kwanza kabisa kusikia kilio cha wananchi wa Mtwara ikiwemo kuelewa madai yao. Swali kubwa kubwa la watu wa Mtwara na Kusini kwa ujumla ni ‘tunanufaikaje’? Jibu la swali hili si ahadi za miradi bali ni vitendo. Hapa ndipo serikali inaposhindwa kushughulikia suala hili, kutoelewa madai ya wananchi na kuyapotosha.Viongozi wa kisiasa wenye ushawishi kutoka pande zote, chama tawala na vyama vya upinzani, waende Mtwara kuzungumza na wananchi, lakini wawasikilize kwanza.

  1. Lazima viongozi tujenge utamaduni wa kusikiliza wananchi na si kuwahutubia tu. Wananchi wa Mtwara wana madai ambayo lazima viongozi tukae kitako kuwasikiliza kisha kufanya nao majadiliano ambayo yatatoa mwafaka. Rais mstaafu, Ndugu Benjamin Mkapa ameshatoa kauli kuhusu suala hili. Ni wakati mwafaka sasa kwa viogozi wengine kumuunga mkono kwa kwenda Mtwara na kukaa na wananchi wa Wilaya zote za Mtwara, kusikiliza hoja zao na kuona namna ya kupata ufumbuzi wa suala hili. Wakati hatua hii inachukuliwa, wananchi waombwe kutulia na kuacha vurugu za aina yeyote ile, na Serikali isimamishe mradi mpaka hapo suluhu na wananchi itakapopatikana.

  1. Wakati juhudi hizo zinaendelea Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa bomba, kwani ni dhahiri gharama za mradi huu ni kubwa mno kulingana na uhalisia wa miradi ya namna hii duniani kote. Katika taarifa zote kwa umma Serikali imekuwa ikisema kwamba mradi utagharimu jumla ya dola za kimarekani 1.2 bilioni, lakini katika taarifa ambayo Wizara ya Nishati na Madini imesambaza jana kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini imesema mradi utagharimu dola za kimarekani milioni 875. Usiri katika mkataba huu unaashiria kwamba Serikali inaficha kitu. Hivyo njia pekee ni kutaka mkataba uwe wazi kwa wananchi.

  1. Wakati tunawataka wananchi wa Mtwara kuruhusu utulivu, ni vema Serikali ijiandae kutoa majawabu ya madai ya wananchi hao. Majawabu ya Serikali yajikite kueleza wananchi wa Mtwara wanafaidikaje na rasilimali ya gesi asilia kwa maendeleo yao. Wananchi wa Mtwara wanataka uwajibikaji wa Serikali kwenye utajiri wa nchi, na wamechoka na porojo za orodha ya miradi isiyotekelezwa.

Viongozi twendeni Mtwara kusikiliza wananchi wetu. Nchi inaungua na hatuwezi kuendelea kuzozana badala ya kuzima moto huu hatari kama vita vya MajiMaji. Mimi nakwenda Mtwara haraka na mara baada ya viongozi wangu wa chama kutoa ridhaa.


ZITTO KABWE
Mbunge, Kigoma Mjini (Chadema)
Waziri Kivuli wa Fedha
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


·        Mradi kabambe wa umeme kujengwa
·        Rais Kikwete apokea ripoti ya maandalizi
·        Utagharimu mabilioni ya fedha
·        Utaunganisha mikoa yote kwenye Gridi ya Taifa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba 12, 2011, amepokea ripoti kutoka makampuni mawili ya kimataifa kuhusu Mpango Kabambe ya mradi mkubwa wa umeme ambao utaunganisha kwenye Gridi ya Taifa mikoa yote sita ambayo kwa sasa haiko kwenye gridi hiyo.

Rais Kikwete amepokea ripoti hiyo kutoka makampuni ya China National Machinery&Equipment Import&Export Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani ambayo kwa pamoja yanatarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100 kutoka Mtwara hadi Singida.

Mradi huo mkubwa wa umeme wa megawati 300 utakaogharimu karibu dola za Marekani milioni 684 na utakaozalisha umeme wa moja kwa moja na wenye nguvu kubwa ya 300 kV (300 kV High Voltage Direct Current – HVDC) utagharimiwa kwa pamoja na mkopo kutoka Benki ya Exim ya China na Serikali ya Tanzania.
Umeme kutokana na mradi huo utaunganishwa kwenye gridi ya taifa na kutoka Singida hatimaye utavutwa kupelekwa katika mikoa ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ya Kagera, Kigoma na Rukwa ambako pia utaongeza upatikanaji wa umeme katika machimbo ya madini yaliyoko katika mikoa hiyo
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mbali na mikoa hiyo mitatu, pia mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo nayo haiko katika Gridi ya Taifa nayo itaunganishwa katika Gridi hiyo kupitia umeme huo
Kuunganishwa kwa mikoa hiyo sita katika Gridi ya Taifa kupitia umeme wa mradi huo pamoja na Mkoa wa Ruvuma ambao utaunganishwa katika Gridi hiyo kwa mradi unaogharimiwa na Serikali ya Sweden kutakamilisha mpango wa Serikali ya Awamu ya Nne kuunganisha mikoa yote ya Tanzania kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.
Kwa sasa Mkoa wa Kagera unahudumiwa na umeme kutoka Uganda, wakati Mikoa ya Kigoma na Rukwa inahudumiwa na umeme wa mafuta ya dizeli. Mikoa ya Mtwara na Lindi inapata umeme wake kutoka kampuni ya Wentworth ambao haujaunganishwa kwenye gridi ya taifa.
 Kuunganisha mikoa yote ya Tanzania kwenye Gridi ya Taifa ilikuwa moja ya ahadi kubwa zilizotolewa na Serikali ya Rais Kikwete wakati anaingia maradakani na kwa kuuunganisha mikoa hiyo sita kwenye Gridi hiyo, Serikali hiyo itakuwa imetimimiza ahadi hiyo
Akipokea ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa juhudi zao zilizofanikisha makubaliano ya kujengwa kwa mradi huo mkubwa wa umeme ambao utachangia kuongeza wingi wa umeme nchini katika kipindi ambacho kwa miezi kadhaa Tanzania imekabiliwa na mgawo wa umeme kutokana na ukame uliokausha maji kwenye mabwawa makubwa ya uzalishaji umeme nchini.
Rais Kikwete pia ameitaka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki ya EXIM ya China kuhakikisha kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zinapatikana haraka iwezekanavyo na pia ameitaka TANESCO na makampuni ya CMEC na Siemens baada ya kupatikana kwa fedha kuanza ujenzi wa mradi huo kwa kasi na kuukamilisha katika muda na ubora unaotarajiwa.

Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM. 
12 Oktoba, 2011


PINDA USO KWA USO NA WANAHABARI

 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Habari, Wamiliki na Wahariri wa Vyombo vya Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza nao, kwenye makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam, Januari 25, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Prince Bagenda wakati alipokutana na Wajumbe wa Baraza la Habari, Wamiliki na Wahariri  wa Vyombo vya Babari kwenye makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam, Januari 25, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Saturday, January 26, 2013

MAMBO YA NDONDI HAYO

 Francis Cheka, mmoja wa mashuhuda wa ngumi za ridhaa ya kuwapata wanandondi wa kuuwakilisha mkoa wa Kagera kwenye mashindano ya taifa, yalifanyika kwenye ukumbi wa klabu wa Lina's uliko katika manispaa ya Bukoba.
 Wanandondi wakijinadi.
 Mwenyekiti wa chama cha ndondi Kagera, Leoperd Kayunga, na afisa utamaduni wa mkoa wa Kagera Rugeiyamu.
 Msanii  Afisa Kazinja akifanya vitu vyake.

Kundi la BK Sunday aliyepiga wimbo wa SEKDO.

BONANZA KWA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI LILILOANDALIWA NA JAMBO TANZANIA

 Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Kagera, Fikir Kisimba na mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali mstaafu Issa Njiku (kushoto) waliokuwa miongoni mwa walioudhuria bonanza.
 Muasisi wa jambo Tanzania toka Ujerumani akitoa historia ya Jambo Tanzania.
 Wanafunzi walioshiriki kwenye bonanza hilo.