Thursday, September 18, 2014

KIKWETE AWASILI WASHINGTON

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa La Guardia jijini Washington DC tayari kwa kushiriki katika mikutano mbalimbali na pia katika hafla ya "USIKU WA JAKAYA"  leo jioni
 Rais Kikwete akilakiwa na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kuwasili hoteli aliyofikia
 Karibu Washington DC Mheshimiwa
 Rais akiendelea kusalimia na na wafanyakazi wa ubalozini
 Mapokezi yakiendelea
 Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Lucas Mkama wa Vijimambo Blog
Karibu sana Mzee...
PICHA NA IKULU

Wednesday, September 17, 2014

RAIS KITWETE AELEKEA NCHINI MAREKANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York. Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
Rais Kikwete akisindikizwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakati alipokuwa anaondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuelekea Marekani Septemba 15, 2014. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili New York, Marekani. Kulia Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifuatiwa na Mama  Upendo Manongi Septemba 16, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Tanzania  baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.  PICHA NA IKULU


WAZIRI MKUU PINDA NA WAHISANI

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Bw. Lord Hollick ambaye ni  Mjumbe wa Masuala ya Biashara wa Waziri Mkuu wa Uingereza nchini  Tanzania katika majadiliano  kuhusu  ushirikiano baina ya serikali na Sekta Binafsi  (PPP Dialogue) kwenye hoteli ya Hyatt Regency- Kilimanjaro jijini Dar es salaam.

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa  wa Kampuni ya Japani ya  SUMITOMO baada ya kuzungumza nao ofisini kwake jijini Dar es salaam Kulia kwake ni Rais wa kampuni hiyo, Nakamura Kumharu.

Tuesday, September 09, 2014

RAIS KIKWETE NA WAJUMBE WA KITUO CHA DEMOKRASIA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya kumalizika kwa  awamu ya pili ya mazungumzo nao Ikulu Ndogo mjini Dodoma.

PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU PINDA JIJINI ARUSHA

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kibosho wakati alipokutana nao kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro wakiwa katika ziara ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga. Mheshimiwa Pinda alikuwa akienda Dar es salaam akitoka Arusha.