MKOA wa Kagera umezindua wimbo maalumu utakaokuwa ukiimbwa
wakati wa shughuli mbalimbali za kuhamasisha masuala ya maendeleo na amani mkoani humo ambao umetungwa na msanii maarufu
hapa nchini mwalimu John Mgango.
Wimbo huo umezinduliwa rasmi jana na mkuu wa mkoa wa Kagera
Kanali Mstaafu Fabiani Massawe wakati wa kikao cha ushauri cha mkoa wa Kagera
(RCC) kilichokuwa na lengo la kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha
2013/14 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa huyo uliko katika manispaa
ya Bukoba.
Akizundua wimbo huo awaagiza viongozi wahakikishe wimbo
unahubiliwa kwa kuwa utasaidia kuwaelimisha
wanachi kuelewa mambo yanayokwamisha maendele
mkoani humo na yanayochangia uvunjifu wa
amani.
Mkuu huyo wa mkoa ameendelea kusema kuwa wimbo huo
ulitafutiwa maneno mazuri yanayolenga dhana halisi ya amani na maendeleo ya mkoa
wa Kagera, amesema mkoa wa Kagera una mkakati mkubwa wa kutokomeza vitendo vinavyokwamisha
maendeleo na uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake mtunzi wa wimbo huo John Mgango wakati wa
uzinduzi huo amewaomba Watanzania wajiepushe na mkifarakano ili waweze
kudumisha amani hapa nchini .
Massawe ni mmoja wa wanaharakati wa masuala ya maendeleo
hapa nchini, mkoani Kagera amefanikiwa kubadili ya mkitazamo ya wananchi mkoani humo hali ambayo
imewawezesha kuondokana na masuala ya uvivu, majungu na masuala mengine
yaliyokuwa yanakwamisha maendeleo mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment