Wednesday, July 31, 2013

UN yaamrisha M23 kusalimisha silaha



Waasi wa M23
Umoja wa Mataifa umewapa wapiganaji wa M23 walioko Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia
saa 48 kusalimisha silaha, la sivyo watakabiliwa kijeshi. 

Kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 3000 kitasaidiana na jeshi la Congo kuweka eneo la usalama mjini Goma.Kikosi hicho kimekubaliwa kutumia nguvu dhidi ya waasi wanaolaumiwa kwa kuwaua raia katika maeneo karibu na mji wa Goma.

Mapema mwezi huu mapigano kati ya M23 na jeshi la Congo yalizuka mashariki mwa nchi ambapo Umoja wa Mataifa ulilaumu waasi wa M23 kwa kuwaua kiholela raia katika eneo la Mutaho viungani mwa Goma.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa umewataka waasi wote na raia walioko Mashariki mwa Congo kusalimisha silaha walizonazo katika kambi ya jeshi la Umoja wa Mataifa ifikapo Alhamisi jioni.Onyo hilo limeongeza yeyote atakayepatikana na silaha atachukuliwa kuwa mpiganaji.

Hali ya usalama imeendelea kudorora Mashariki mwa nchi na onyo la sasa linanuia kuzuia waasi dhidi ya kukaribia mji wa Goma. Takriban watu 70,000 wamekimbia makwao, kufuatia mapigano kati ya jeshi na waasi. Umoja wa Mataifa unasema Wengi wamekimbilia nchi jirani ya Uganda.

Tsvangirai apingana na Mugabe kuhusu uchaguzi



Waziri mkuu Morgan Tsvangirai
Waziri mkuu nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ametoa wito kwa mahakama ya kikatiba nchini humo kufutilia mbali agizo la rais wa taifa hilo Robert Mugabe kuandaa uchaguzi mwishoni mwa mwezi Julai.
Tsvangirai ameonya kuwa huenda taifa hilo likakumbwa na hali ya switofahamu iwapo uchaguzi huo utafanyika.
Katika ombi lake waziri huyo anasema kuwa mda uliotolewa kuandaa shughuli ya usajili wa wapiga kura na uteuzi wa wagombea ni mchache mno.
Hata hivyo Tsvangirai hakusema ni lini angependa uchaguzi huo ufanyike.
Tayari uamuzi huo wa Mugabe kuitisha uchaguzi mapema kuliko ilivyotarajiwa, umekashifiwa na viongozi wengine wa mataifa ya Afrika Kusini.
Rais Mugabe alikwenda mahakamani mwezi jana kufuatia shinikizo kutoka kwa muungano wa nchi za Afrika Kusini (SADC) kubana hatua ya kuakhirisha shughuli nzima ya uchaguzi.
Ikiwa Tsvangirai atashinda kesi hii, anasema mahakamana itakuwa imezuia jambo lisilo la kisheria kuweza kutumbukiza nchi katika hali ya switofahamu.
Tsvangirai anataka uchaguzi ufanyike tu baada ya mageuzi ya sheria za uchaguzi ambayo yametokana na katiba mpy

Wanyarwanda wapiganaji wa M23


Wapiganaji wa M23
Raia wanne wa Rwanda wameambia BBC kwamba walilazimishwa na jeshi la nchi hiyo kujiunga na waasi wa M23 Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wanne hao wamesema walitoroka mapigano na kwamba wanajaribu kuomba hifadhi katika nchi jirani ya Uganda.
Mmoja wa Wanyarwanda hao wamesema asili mia 90 ya wapiganaji wa M23 ni wanajeshi wa Rwanda.
Mwenzake ambaye ni mwanafunzi wa utabibu amesema amewahudumia wapiganaji 300 waliojeruhiwa kwa risasi.
Serikali ya Rwanda imekanusha kuunga mkono waasi wa M23. Msemaji wa jeshi la Rwanda Joseph Nzabamwita amesema wanne hao wanatumia kisingizio cha kulazimishwa jeshini ili kupata hifadhi.

Tuesday, July 30, 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND AWASILI NCHINI


 Waziri mkuu wa THAILAND akikagua gwalide.
 Jakaya Mrisho Kikwete akimuonesha mandhari ya bandari ya salama Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  alipowasili jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra  akisalimiana na baadhi ya raia wa Thailkand wanaoishi nchini alipowasili katika hoteli ya Kilimanjaro Regency Hyatt jijini Dar es salaam.

KIKWETE AUPA WAKATI MGUMU UONGOZI WA MANISPAA YA BUKOBA


RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,  Dkt.Jakaya Kikwete ameuagiza uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba kuhakikisha unagawa viwanja kwa wananchi zaidi ya 800  waliokuwa wanadai viwanja walivyoviomba katika manispaa hiyo mwaka 2003.
 
Rais Kikwete alitoa agizo hilo wakati akiwahutubia wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba katika  mkutano wa hadhara kwenyeuwanja wa michezo wa Kaitaba baada ya kupokea taarifa toka mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki juu ya malalamiko ya wananchi walioomba viwanja katika manispaa hiyo.
 
Aliuambia uongozi huo pia kuhakikisha unawarejeshea wananchi hao fedha walizozitoa wakati wa mchakato wa kuomba viwanja hivyo, ameutaka uongozi huo kutekeleza haraka mchakato wa kuwapatia viwanja hivyo kwa wananchi hao.

Aliuambia uongozi huo utenge viwanja 800 kutoka  kwenye viwanja vya mradi vya upimaji wa viwanja 5,000 ambavyo halmashauri ya manispaa ya Bukoba imeanza kuviuza kwa wananchi.

 
Alisema atauelewa uongozi wa manispaa hiyo ikiwa utashidwa kutekeleza agizo alilolitoa, “lazima haki ya wananchi itendeke, haki itatendekeka ikiwa manispaa itawapatia wananchi viwanja walivyoviomba ambavyo hawajapatiwa kwa muda mrefu” aliagiza.
 
Pia katika mkutano huo aliwaeleza wananchi  mradi  wa ujenzi wa soko kuu la Bukoba  kuwa lazima utekelezwe, Rais huyo aliuagiza uongozi manispaa kuhakikisha unaandaa maeneo mbadala yatakayotumiwa na wafanyabiashara watakaohamishwa katika soko hilo la sasa baada ya kuvunjwa kupisha ujenzi wa soko jipya.
Rais huyo alitoa angalizo kwa  uongozi wa manispaa kuhakikisha unatekeleza ujenzi wa soko jipya kwa kufuata taratibu zote zinazokubalika, aliauagiza pia kuwashirikisha wananchi katika mchakato mzima wa ujenzi wa soko hilo jipya.
 
Alisema mradi wa ujenzi wa soko jipya la kisasa unaweza kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo katika manispaa ya Bukoba, “wananchi wanapenda maendeleo ni lazima wakubali mradi wa ujenzi wa soko jipya la Bukoba” alisisitiza.
 
Rais Kikwete aliwaambia wananchi waachane na malumbano ya kisiasa kwa kuwa yanakwamisha mambo ya maendeleo, alisema kuwa maendeleo hayaji mara moja yanataka mchakato, alimaliza kwa kuiwaomba wananchi kuwa kitu kimoja hasa katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayobuniwa.

Kwa sasa uongozi wa manispaa hiyo unatekeleza mradi wa upimaji na wa viwanja 5,000 ambavyo tayari imeishaanza kuviuza kwa wananchi, pamoja na mradi wa upimaji na ugawaji wa viwanja wale walioomba viwanja mwaka 2013 uongozi wa manispaa umewaweka pembeni.
 

Monday, July 29, 2013

KIKAO CHA MAJUMUISHO YA ZIARA YA RAIS KIKWETE MKOANI KAGERA nv

 Charles Mwebeya, Mwandishi ya shirika la utangazaji nchini (TBC) akimsikiliza Mh.Kikwete kwa makini.



 Baadhi ya watumishi wa serikali.






ZIARA YA RAIS KIKWETE MKOANI KAGERA

 Kivuko kilichozinduliwa na rais Kikwete, ni cha Rusumo.
 Waziri wa maji,Jumanne Magembe akiongea na waziri wa miundo mbinu, Dkt John Magifuli.
 Magufuli na mmiliki wa mtandao huu.


SERIKALI imetoa kipindi cha wiki mbili kwa wale wanaomiliki silaha kinyume na sheria katika mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma kuhakikisha wanazisalimisha mara moja kwa hiari ili wajiepushe na mkono wa sheria.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiongea na wananchi wa wilaya ya Biharamulo baada ua kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 154 toka Kagoma hadi Rusaunga.


Kikwete amesema baada ya kipindi alichokitoa cha kumalizika serikali itaanzisha operation maalumu kusaka silaha hizo kwa kupita nyumba hadi nyumba.

Amesema operation hiyo maalumu itaendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo alivitaja kuwa ni pamoja na jeshi la polisi, jeshi la ulinzi na usalama na idara ya usalama wa taifa.
 Vikundi vya burudani.

 Mpiga picha maarufu, Issa Michuzi na mmiliki wa mtandao huu, Audax Mutiganzi.

 Mkuu wa mkoa wa Kagera, kanali mstaafu Fabian Massawe,akicheza ngoma.
Jumanne Magembe akiwatunza wasanii.

Friday, July 26, 2013

RAIS KIKWETE WILAYANI BIHARAMULO

VIONGOZI wa vyama vingine vya ushirika vilivyoko hapa nchini wametakiwa kuja mkoani Kagera kujifunza namma chama cha ushirika cha Kagera (KCU)kinavyoendesha  shughuli zake ili waweze kupata elimu ya itakayowasaidi kuimarisha vyama vyao vya ushirika.
 
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete mara kuzindua jesho la kitega uchumi lililojengwa na chama cha ushirika cha Kagera (KCU) liliko mtaa wa one way jana.
 
Rais Kikwete alisema chama cha ushirika Kagera ni moja ya vyama vya ushirika nchini ambavyo vimeimarika zaidi na vyenye uwezo mkubwa ukilinanisha na vyama vingine vya ushirika vilivyoko hapa nchini.

Alisema kuimarisha kwa chama hicho kunatokana na mikakati mizuri inayopangwa na viongozi wa chama hicho yenye lengo la kuiimarisha hasa kwa kikijengea uwezo zaidi.

"KCU ni chama cha ushirika ambacho ni imara kisichoteteleka na chenye mafanikio mazuri viongozi wa vyama vya ushirika ni lazima waje kupata elimu ya namna ya kuendesha vyama vyao" alisema Rais huyo.
 
Alisema vyama vya ushirika vinapoimarika vinawanufaisha zaidi wakulima kwa kuwa vinakuwa na uwezo mkuba wa kukusanya mazao toka kwa wakulima na kuwalipa kwa wakati, aliendelea kusema kwa vyama vya ushirika kamwe haviwezi kuimarika bila kuwa na nguzo.
 
Rais huyo alisema nguzo kuu ya inayiviimarisha vyama vya ushirika ni vitega uchumi, alisema vitega uchumi vinaviwezesha vyama vya ushirika kupata mikopo toka kwenye taasisi za kifedha.
 
"Nimefurahia taarifa niliyopokea toka KCU inapendeza,nimefurahishwa na idadi ya vitega uchumi vikubwa inavyovimiliki  ambavyo vinaweza kuipa dhamana popote duniani, naomba uongozi wa KCU uendelee kubuni mambo makuba zaidi" alisema.
 
Alisema serikali kila mara imekuwa ikipata mzigo mkubwa wa kuvinasua vyama vya ushirika kwa kuvilipa madeni, amesema hali hiyo ni mbaya sana kwa kuwa inaitia serikali hasara kubwa.
 
Rais Kikwete alisema sasa ni wakati wa vyama vya ushirika kijiendesha bila kutegemea ruzuku toka serikalini, utegemezi huo unawadidimiza wakulima kwa kuwa vinakuwa havina uhakika wa kukusanya mazao toka kwao na kuwalipa kwa wakati.
 
 
 





ZIARA YA RAIS KIKWETE MKOANI KAGERA







RAIS KIKWETE AUDHURIA SIKU YA MASHUJAA KABOYA






Wednesday, July 24, 2013

MAMBO YA MAREKENI HAYO

Mahojiano na wadau wa GENN Radio (Kansas U.S.A)


Bwn. Robert Otto ambae ni Mkurugenzi wa kituo cha Global Entertainment and News Network (GENN) kiliyopo Kansas City nchini Marekani.
Dada D ni mtangazaji wa kituo cha Global Entertainment and News Network (GENN) kiliyopo Kansas City nchini Marekani.

Vile vile Dada D Show ni kipindi kinachokwenda hewani kila Jumamosi Mida ya Saa 8:00 PM Est Time kwenye vionjo na vibwagizo Mchanganyiko wa mahusiano ya Mapenzi ndani ndoa, Mahaba, maelewano na malezi ya watoto kwa familia na kufunzani zaidi ndani ya Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Jijini Kansas City.

Mtangaziji AJ wa kipindi cha kuamshana na asubuhi njeema ndani ya  Global Entertainment and News Network (GENN) kiliyopo Kansas City nchini Marekani.

Katika beti hii tunawakaribisha sana katika Mahojiano haya baina ya Jamii Production na wadau wakuu wa Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Kansas City nchini Marekani.

Katika mahojiano haya, utasikia Mkurugenzi wa kituo Bwn. Robert Otto na watangazaji AJ na Dada D wakizungumzia harakati zao kwenye kituo hiki kipya cha Radio


ZIARA YA RAIS KIKWETE MKOANI KAGERA

 Waziri wa ardhi, nyumba na makazi, Profesa  Anna Tibaijuka akiwa na mmiliki wa mtandao huu wa kijamii, Audax Mutiganzi.

 Mkuu wa mkoa waKagera, kanali mstaafu Fabian Massawe, akiongea na Profesa Tibaijuka.