Askari wakimsindikiza mtuhumiwa.
Mfanyakazi kampuni ya
mafuta ya ABOOS iliyoko mjini BUKOBA, HAMADI ALI MOHAMED anayetuhumiwa kumuibia
mwajili wake RAZA FAZAL zaidi ya milioni MIA TANO ISHIRINI na SITA hatimaye
amepata dhamana baada ya wadhamini wake kutimiza masharti ya dhamana.
Mahakama ya hakimu
mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bukoba awali ilitoa masharti ya dhamana kwa
kumtaka mtuhumiwa awe na wadhamini WAWILI ambapo mmoja wa wadhamini awe
mtumishi wa serikali na mali isiyoamishika yenye thamani zaidi ya shilingi
milioni MIA MBILI NA SITINI NA MBILI na mdhamini wa PILI alitakiwa kuwasilisha
mahakamani hati ya nyumba yenye thamani ya kiasi hicho.
Mtuhumiwa huyo mwenye
asili ya kiasia aliyepata dhamana baada ya kusota rumande kwa zaidi ya mwezi
mmoja alifika kwa mara nyingine kwenye mahakama
ya wilaya ya BUKOBA majira ya saa TATU na NUSU chini ya ulinzi mkali wa askari
polisi waliokuwa wamevaa sare za kipolisi na wengine wakiwa wamevaa nguo za kiraia.
Mshitakiwa huyo
kufikishwa mahakamani mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya BUKOBA,SYLIVIA
LUSHASI, mtuhumiwa hakutakiwa kujibu lolote kufuatia uzito wa kesi inayomkabili,
hakimu huyo amesema kesi hiyo itatajwa tena tarehe SITA mwezi JUNI mwaka huu.
Pamoja na mtuhumiwa huyo
kupata dhamana mahakama imemtaka kuwasilisha pasi ya kusafiria pia imemtaka
mtuhumiwa huyo kuipa polisi taarifa anapotaka kusafiri toka sehemu moja kwenda
nyingine na anatakiwa pia kutosafiri nje ya mkoa wa Kagera.
Mwendesha
mashitaka
ambaye pia ni wakili wa serikali PAUL KADUSHI akisoma mashitaka
yanayomkabili
mbele ya hakimu huyo amesema mtuhumiwa anadaiwa kumuibia mwajili zaidi
ya shilingi milioni MIA TANO ISHIRINI NA SITA kwa nyakati tofauti kati
ya mwezi JANUARI hadi DESEMBA mwaka
2010.
No comments:
Post a Comment