·
Mradi kabambe wa umeme
kujengwa
· Rais Kikwete apokea ripoti ya maandalizi
· Utagharimu mabilioni ya fedha
·
Utaunganisha mikoa yote kwenye
Gridi ya Taifa
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba 12, 2011, amepokea ripoti kutoka makampuni
mawili ya kimataifa kuhusu Mpango Kabambe ya mradi mkubwa
wa umeme ambao utaunganisha kwenye Gridi ya
Taifa mikoa yote sita ambayo
kwa sasa haiko kwenye gridi
hiyo.
Rais
Kikwete amepokea ripoti hiyo kutoka
makampuni ya China National
Machinery&Equipment Import&Export
Corporation (CMEC) ya China na
Siemens ya Ujerumani ambayo kwa pamoja
yanatarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi
katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia
kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita
1,100 kutoka Mtwara hadi Singida.
Mradi
huo mkubwa wa umeme wa
megawati 300 utakaogharimu karibu dola za
Marekani milioni 684 na utakaozalisha umeme wa moja
kwa moja na wenye nguvu
kubwa ya 300 kV (300 kV
High Voltage Direct Current – HVDC) utagharimiwa kwa pamoja na
mkopo kutoka Benki ya Exim ya
China na Serikali ya Tanzania.
Umeme
kutokana na mradi huo utaunganishwa
kwenye gridi ya taifa na
kutoka Singida hatimaye utavutwa kupelekwa katika mikoa ya Kaskazini
Magharibi mwa Tanzania ya Kagera, Kigoma
na Rukwa ambako pia utaongeza
upatikanaji wa umeme katika machimbo
ya madini yaliyoko katika mikoa hiyo.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo, mbali
na mikoa hiyo mitatu, pia
mikoa ya Lindi na Mtwara
ambayo nayo haiko katika Gridi
ya Taifa nayo itaunganishwa katika Gridi hiyo
kupitia umeme huo.
Kuunganishwa
kwa mikoa hiyo sita katika
Gridi ya Taifa kupitia umeme
wa mradi huo pamoja na
Mkoa wa Ruvuma ambao utaunganishwa katika Gridi hiyo
kwa mradi unaogharimiwa na Serikali ya Sweden kutakamilisha mpango wa Serikali ya
Awamu ya Nne kuunganisha mikoa yote ya
Tanzania kwenye umeme wa Gridi ya
Taifa.
Kwa
sasa Mkoa wa Kagera unahudumiwa
na umeme kutoka Uganda, wakati Mikoa ya Kigoma
na Rukwa inahudumiwa na umeme wa mafuta
ya dizeli. Mikoa ya Mtwara
na Lindi inapata
umeme wake kutoka kampuni ya Wentworth ambao haujaunganishwa kwenye gridi ya
taifa.
Kuunganisha
mikoa yote ya Tanzania kwenye Gridi ya Taifa
ilikuwa moja ya ahadi kubwa
zilizotolewa na Serikali ya Rais
Kikwete wakati anaingia maradakani na kwa kuuunganisha
mikoa hiyo sita kwenye Gridi
hiyo, Serikali hiyo itakuwa imetimimiza
ahadi hiyo.
Akipokea
ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru
Wizara ya Fedha, Wizara ya
Nishati na Madini pamoja na
Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kwa juhudi zao zilizofanikisha makubaliano ya kujengwa kwa mradi
huo mkubwa wa umeme ambao
utachangia kuongeza wingi wa umeme
nchini katika kipindi ambacho kwa miezi kadhaa
Tanzania imekabiliwa na mgawo wa umeme
kutokana na ukame uliokausha maji kwenye mabwawa
makubwa ya uzalishaji umeme nchini.
Rais
Kikwete pia ameitaka Wizara ya Fedha kwa
kushirikiana na Benki ya EXIM ya
China kuhakikisha kuwa fedha za kutekeleza
mradi huo zinapatikana haraka iwezekanavyo na pia ameitaka TANESCO na makampuni ya
CMEC na Siemens baada ya kupatikana kwa
fedha kuanza ujenzi wa mradi
huo kwa kasi
na kuukamilisha katika muda na
ubora unaotarajiwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
12
Oktoba, 2011
No comments:
Post a Comment