Tuesday, January 22, 2013

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TAIFA MKOANI KAGERA

 Baadhi ya viongozi wa chama na serikali waliojitokeza kumlaki makamu mwenyekiti wa CCM taifa, Philip Mangula alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kufanya ziara ya siku mbili mkoani Kagera, mbele ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kagera Bi. Costancia Buhiye, mwenye tai ya njano ni mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe.

 Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Bi. Ziporah Lion Pangani alikuwa miongoni mwa walijitokeza kumlaki Mangula.
 Mangula alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki na mjumbe wa NEC, Nazir Kalamagi walikuwa miongoni mwa waliojitokeza kumlaki Mangula.
 Kagasheki akifurahia jambo na mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Mstaafu, Issa Njiku.

 Waziri Kagasheki akiteta jambo na Meya wa zamani wa manispaa ya Bukoba, Samwel Ruangisa nje ya ofisi ya kuu ya mkoa wa Kagera ya CCM.
 Mbunge wa zamani wa jimbo la Bukoba mjini Joseph Mujuni Kataraiya akisalimiana na Bw. Ruangisa ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitendagulo.
Ruangisa akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Bukoba, Bi. Ziporah Pangani.

No comments:

Post a Comment