Ndege ya shirika la Precision Air aina ya ATR ambayo hutua kwenye viwanja mbalimbali vilivyoko hapa nchini imekwama kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kufuatia uwanja huo kujaa matope kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Kagera hali iliyosababisha hofu kwa abiria.
Hali ya kukwama kwa ndege hiyo kwenye matope iliwatia hofu abiria walikuwa ndani ya ndege hiyo jambo ambalo liliwalazimu kila abiria aanze kusali kulingana na dhehebu lake mmoja wa waliounusurika na ajali hiyo alisema.
Habari zinadai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni rubani ambaye kuiendesha ndege hiyo kwa mwendo kasi wakati akijua sehemu ya uwanja huo inafanyuiwa ukarabati.
Kufuatia hali hiyo abiria walikuwa ndani ya ndege hiyo walilazimika kuvua viatu kwa ajili ya kushika ndani ya ndege hiyo ambayo ilikuwa tayari imekwama kwenye matope.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo blog hii imezipata ni kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es salaam, ambapo kufuatia ajali hiyo ilisitisha safari kwa muda na baadae kuondoka kwenye uwanja wa Bukoba majira ya usiku.
Ndege hiyo ilikwamuliwa katika tope hilo baada ya kuvutwa.
No comments:
Post a Comment