MAKAMU Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula ameshindwa kumunusuru Meya wa
manispaa ya Bukoba, Anatory Amani asienguliwe na madiwani wanaotaka kumpigia
kura za kutokuwa na imani naye kulingana na utendaji wake wa kazi.
Pamoja na ushawishi mkubwa alioufanyaMangula wa kutaka
kumnusuru Meya huyo madiwani hao
wameonekana kushirikia msimamo wao wa kutaka Meya huyo aachie ngazi.
Madiwani hao walionyesha msimamo wao wakati wa kikao cha
dharula cha halmashauri ya kuu ya Bukoba kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mtakakatifu Francis uliko katika manispaa ya Bukoba.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka ndani ya kikao hicho
kilichomalizika majira ya saa 9.00 leo baadhi ya madiwani na wajumbe wa halmashauri kuu ya Bukoba walimkataa waziwazi Mstahiki meya Amani kwa kuonyesha vielelezo
mbele ya Philip Mangula.
Wajumbe wa halmashauri hiyo kuu walikataa uamzi wa Philip
Mangula aliyetaka tume maalumu iundwe ya kuchunguza tuhuma zinazomkabili
mstahiki Meya huyo.
Walimweleza Mangula kuwa kama anataka kuunda tume ya
kuchinguza tuhuma zinazomkabili Amani kuwa ni lazima ahakikishe Meya huyo
anaachia ofisi ili apishe uchunguzi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walimweleza Mangula kuwa
mambo anayoyafanya yanalenga kuifilisi Halmashauri ya manispaa ya Bukoba, kwa
nyakati tofauti wameonyesha kutoridhishwa na matumizi ya mamilioni ya pesa
yanayofanywa na meya huyo na mikataba ya
miradi anayoibuni katika manispaa hiyo.
Wamemweleza Mangula kuwa hawamtakio Meya huyo na ndio maana
wanataka kumpigia kura za kutokuwa na imani naye, katika hali isiyo ya kawaida
madiwani hao walikataa kutii maelekezo yaliyotolewa Mangula.
Mangula aliwataka madiwani wote 8 wa CCM waliosaini waraka wa kutaka Meya apigiwe kura
za kutokuwa na imani naye waondoe saini zao kwenye waraka huo la sivyo
wangenyanganywa uanachama, madiwani hao walikataa maelekezo hayo.
Mangula aliwatishia madiwani hao kuwa madiwani ambao
walisaini waraka huo ambao wangekataa kuondoa saini zao kuwa chama hicho
kingewanyanganya kadi za uanachama.
Habari ambazo gazetib hili limezipata ni kwamba mchakato wa
kikao cha baraza la madiwani kitakachojadili hatima ya Mstahiki Meya Amani kitafanyika januari, 28 mwaka huu.
Meya huyo anakabiliwa na tuhuma ya kuingia mikataba mibovu
wa miradi ya ujenzi wa soko kuu la Bukoba, upimaji wa viwanja, ujenzi wa jengo
la kitega uchumi, Meya huyo amekuwa akituhumiwa kwa kufanya mambo kwa usiri
mkubwa.
amani si uachie ngazi mbona unagangania madaraka kama amin
ReplyDelete