Dr. Diodorus Kamala (Balozi wa Tanzania
Ubelgiji, Daniel RICHIR Chief Executive Officer wa kampuni ya Rosier na
Raphael De RIJCKE General Sales Manager wa kampuni ya Rosier. Kampuni
ya Rosier ni kampuni kubwa inayozalisha mbolea hapa Ubelgiji na na sehemu ya mbolea inayozalishwa na kiwanda hicho inauzwa nchini
Tanzania.
Dr Kamala ameushukuru uongozi wa kiwanda hicho kwa kazi nzuri wanayofanya na pia ameuomba uongozi wa kiwanda hicho kuwatuma watalaamu wake nchini Tanzania ili waweze kuyafanyia utafiti mazao mbalimbali, udongo na
hali ya hewa ya maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Kampuni hiyo
imekubali kutuma wataalam Tanzania ili kufanya utafiti utakaosaidia
kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya biashara na
chakula. Balozi huyo alitembelea kiwanda hicho jana. Kwa sasa kiwanda hicho
kinauzia mbolea Wazalishaji wa Tumbaku . Kiwanda hicho kilianza
uzalishaji wa mbolea mwaka 1830, Kinazalisha mbolea za aina mbalimbali kwa
kuzingatia mahitaji ya mteja.
No comments:
Post a Comment