Askari wa kike nao walizawadiwa.
Baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi waliopata zawadi, kulia ni Shadrack Agumisa na kushoto ni Bw. Rweyongeza maarufu kwa jina la Mamba.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera akiongea wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti na zawadi askari waliotekeleza wajibu wao vizuri.
MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe ameushauri
uongozi wa jeshi la polisi mkoani humo kuwawajibisha askari wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi yao ili uweze kulinda heshima ya jeshi hilo.
Massawe alitoa ushauri huo wakati wa hafla fupi ya
kuwazawadia maofisa 42 wa jeshi hilo waliotekekeleza wajibu wajibu wao vizuri
kwa mwaka 2012 iliandaliwa na jeshi hilo jana na kufanyika kwenye viwanja vya
kikosi cha kutuliza ghasia vilivyoko eneo la Nshambya katika manispaa ya
Bukoba.
Alisema jeshi la polisi litakapowakumbatia askari
wanafachafua sifa ya jeshi la polisi litakuwa linakaribisha uhasama kati ya jeshi
hilo na wananchi ambao mara nyingi ndio huwa vyanzo vya taarifa zinazolisaidia
jeshi la polisi kukabiliana na vitendo vya uharifu.
Mkuu huyo wa mkoa alisema jeshi la polisi linapochafuliwa na
askari wachache wanaofanya kazi kwa maslahi yao binafsi linaonekana halina
dhamana ndani ya jamii, “ndugu zangu
askari pamoja na kufanya kazi nzuri nawaomba kitu kimoja, jueni dhamana yenu
ili kila mtu awaheshimu msipofanya hivyo mtakuwa mnakaribisha uadui kati yenu
na wananchi” alisema.
“Ndugu zangu maaskari tekelezeni wajibu wenu vizuri hata
vyeo haviji kwa njia ya matambiko, vyeo vinatolewa kwa mtu anayetekeleza wajibu
wake vizuri, matambiko ya kupata cheo sio kuchinja kuku na mbuzi bali ni
kufanya kazi kwa bidii” aliendelea kusema.
Massawe alilipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri
liliyoifanya kwa mwaka 2012 ya kuthibiti matukio ya uharifu yaliyokuwa
yamekithiri kwenye mapori ya kimisi na Kasindaga ambayo ni pamoja na unyanganyi
wa kutumia silaha, utekaji wa magari na ubakaji.
Aliwataka askari wasibweteke na mafanikio walioyapata badala
yake waongeze juhudi katika kutekeleze wajibu wao ili waweze kukomesha kabisa
matukio ya uharifu mkoani Kagera, “ninawapongeza sana ndugu zangu maaskari
mmefanya kazi nzuri sana nafikiri anayepinga hilo naweza nimlinganisha na bundi
ambao huwa wanaona usiku tu” alimaliza.
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera
Philip Kalangi alimweleza mkuu wa mkoa kuwa waliozawadiwa ni askari 42 waliofanya
kazi vizuri kuanzia mwezi januari hadi Desemba mwaka jana.
Kalangi alisema lengo la jeshi la polisi kuwazadia askari ni
kuongeza molali ya kazi, alisema jeshi hili limejiwekea utaratibu wa kutoa
zawadi kwa askari wanaofanya vizuri kila mwaka, askari hao kila mmoja alizawadiwa
pesa taslimu shilingi 50,000 na cheti cha shukrani.
Mkuu wa mkoa wa Kagera katika picha ya pamoja na askari waliotunukiwa zawadi na maofisa wengine wa jeshi la polisi.
Maofisa wa jeshi la polisi Kagera wakiwa katika picha ya pamoja.
askari muendelee kufanya kazi kwa bidii mzingatie maelekezo ya massawe
ReplyDelete