Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kufanya naye mazungumzo
Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii ya Januari 30. 2013
Thursday, January 31, 2013
Wednesday, January 30, 2013
Dr. DIODURUS KAMALA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MBOLEA.
Dr. Diodorus Kamala (Balozi wa Tanzania
Ubelgiji, Daniel RICHIR Chief Executive Officer wa kampuni ya Rosier na
Raphael De RIJCKE General Sales Manager wa kampuni ya Rosier. Kampuni
ya Rosier ni kampuni kubwa inayozalisha mbolea hapa Ubelgiji na na sehemu ya mbolea inayozalishwa na kiwanda hicho inauzwa nchini
Tanzania.
Dr Kamala ameushukuru uongozi wa kiwanda hicho kwa kazi nzuri wanayofanya na pia ameuomba uongozi wa kiwanda hicho kuwatuma watalaamu wake nchini Tanzania ili waweze kuyafanyia utafiti mazao mbalimbali, udongo na hali ya hewa ya maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Kampuni hiyo imekubali kutuma wataalam Tanzania ili kufanya utafiti utakaosaidia kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula. Balozi huyo alitembelea kiwanda hicho jana. Kwa sasa kiwanda hicho kinauzia mbolea Wazalishaji wa Tumbaku . Kiwanda hicho kilianza uzalishaji wa mbolea mwaka 1830, Kinazalisha mbolea za aina mbalimbali kwa kuzingatia mahitaji ya mteja.

Tuesday, January 29, 2013
PINDA AKUTANA NA WAFANYBIASHARA KUJADILI MGOGORO WA GESI
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wafanyabiashara wa Mtwara
kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara, Januari 28,
2013. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
TAHADHALI YA MVUA KUBW KWENYE MAENEOMENGI TANZANIA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Simu pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 29 Januari, 2013
Taarifa kwa umma: Uwezekano wa matukio ya mvua kubwa
Taarifa Na. 20130129-02
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 12:00 Jioni
Daraja la Taarifa:
1:Taarifa 2:Ushauri
3:Tahadhari
4:Tahadhari Kubwa:
Ushauri
Kuanzia:
Tarehe
30 Januari, 2013
Mpaka:
Tarehe
01 Februari, 2013
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila
siku)
Kiwango cha uhakika: Wastani
Maeneo yatakayoathirika
Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe,
Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara na maeneo jirani na
mikoa hiyo.
Maelezo:
Kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa
Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu
kutoka Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo:
Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu
wanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika
na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho
na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

PICHA YA SATELITE INAYOONYESHA JINSI MVUA ITAKAYOSABABASHWA NA KIMBUNGA
Monday, January 28, 2013
WAZIRI MKUU PINDA AANZA MKAKATI WA KUMALIZA MGOGORO MTWARA
Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Mkoani Mtwara, Askofu,
Chilumba akiomba kabla ya kuanza kwa kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo
Pinda na viongozi wa madhehebu ya dini ya Kikristo mkoani Mtwara kuhusu
mgogoro wa gesi kwenye ukmbi wa VETA mjini Mtwara Januari 18, 2013.
Jana Mheshimiwa Pinda alikutana na Viongozi wa dini ya Kiislam mkoani
humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa madhehebu ya Kikristo kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara, Januari 28, 2012.Jana Mheshimiwa Pinda alikutana viongozi wa dini ya Kiislam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NDEGE YA PRECISION AIR YAKWAMA KAGERA
Ndege ya shirika la Precision Air aina ya ATR ambayo hutua kwenye viwanja mbalimbali vilivyoko hapa nchini imekwama kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kufuatia uwanja huo kujaa matope kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Kagera hali iliyosababisha hofu kwa abiria.
Hali ya kukwama kwa ndege hiyo kwenye matope iliwatia hofu abiria walikuwa ndani ya ndege hiyo jambo ambalo liliwalazimu kila abiria aanze kusali kulingana na dhehebu lake mmoja wa waliounusurika na ajali hiyo alisema.
Habari zinadai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni rubani ambaye kuiendesha ndege hiyo kwa mwendo kasi wakati akijua sehemu ya uwanja huo inafanyuiwa ukarabati.
Kufuatia hali hiyo abiria walikuwa ndani ya ndege hiyo walilazimika kuvua viatu kwa ajili ya kushika ndani ya ndege hiyo ambayo ilikuwa tayari imekwama kwenye matope.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo blog hii imezipata ni kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es salaam, ambapo kufuatia ajali hiyo ilisitisha safari kwa muda na baadae kuondoka kwenye uwanja wa Bukoba majira ya usiku.
Ndege hiyo ilikwamuliwa katika tope hilo baada ya kuvutwa.

Sunday, January 27, 2013
WAZIRI MKUU PINDA MKONI MTWARA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunguma na Maimamu wa mkoa wa Mtwara
kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa veta mjini Mtwara Januari 27,
2013. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
TAARIFA YA NDUGU ZITTO KABWE (MB) KUHUSU YANAYOENDELEA MTWARA NA MRADI WA BOMBA LA GESI ASILIA
Serikali
iache kutafuta mchawi, iende Mtwara
Katika kipindi cha wiki nne sasa kumekuwa na maandamamo,
malumbano na vurugu kuhusu mradi wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia
kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Mradi huu wa kutandaza bomba la urefu wa
kilometa 542 ni mkubwa sana hapa nchini, na una thamani kubwa zaidi kuliko
miradi mingine yote ya miundombinu
iliyopata kutokea hapa nchini. Mradi huu utajengwa kwa mkopo wa dola za Kimarekani
1.2 bilioni kutoka Benki ya Exim ya China.
Wananchi wa Mtwara kupitia maandamano ya tarehe 27
Desemba 2012 wametaka kujua hatma ya maendeleo ya mikoa wa kusini kutokana na
mradi huu wa bomba la gesi. Serikali imewajibu wananchi hawa kwa kuwaita
wahaini, watu hatari na wasio elewa. Imefika mahali inapotosha madai yao kwamba
hawataki gesi itoke Mtwara.
Kimsingi Serikali haijajibu hoja yeyote ya msingi ya
wananchi wa Mtwara kuhusu mradi wa kusafirisha gesi. Badala yake imekuwa
ikijaribu kupotosha madai ya watu wa Mtwara kupitia mikutano na vyombo vya
habari.
Tangu maandamano haya yatokee, na baadaye mikutano ya
hadhara na
hatimaye matukio ya kusikitisha ya kuharibu mali za watu, mauaji ya
watu na majeruhi mbalimbli, Serikali na hasa Wizara yenye dhamana ya
mradi huu, imekuwa ikitoa matamko kwenye vyombo vya habari badala ya
kwenda Mtwara kuzungumza na wananchi, kusikiliza madai yao na kuona
namna ya kutekeleza madai hayo. Kutokana na Serikali kutofanya hivyo,
kusikiliza na kuzungumza na wananchi wa Mtwara, vurugu mbaya sana zimeendelea mkoani humo.

Mwezi uliopita, Desemba 2012, tatizo lilionekana kuwa ndogo na lenye kuhusiana zaidi na ukosefu wa kushirikishwa kwa wananchi. Badala ya kushughulikia
tatizo likiwa bado ndogo, Serikali imeona njia pekee ya kushughulikia suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisemakuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje yanachochea mgogoro
huu.
Leo hali iliyopo mkoani Mtwara inasikitisha sana, maana mali
za wananchi zinaharibiwa, nyumba zinachomwa moto na watu wanapoteza maisha. Tunalaani
matukio haya kwa nguvu zetu zote, maana kinachotokea Mtwara si Utanzania.
Tusipowasikiliza wananchi na kutatua mgogoro huu kwa kuwashirikisha, hali
itazidi kuzorota wakati tukitupiana lawama.
Hivi sasa serikali imeona njia pekee ya kushughulikia
suala hili ni kutafuta mchawi na kwa wiki zote hizi imekuwa ikisema kuwa wanasiasa na makampuni ya uwekezaji ya nje
yanachochea mgogoro huu.
Kwanza, Serikali imekuwa ikiaminisha umma kwanza suala
hili limechukuliwa kisiasa. Pili, Serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa baadhi
ya makampuni ya uwekezaji nchini na mataifa ya Magharibi yamekuwa yakichochea
wananchi wa Mtwara.
Katika mwendelezo wa mtindo wa Serikali wa ‘management by press conferences’ jana
Jumamosi Naibu Waziri wa Nishati na Madini ndugu George Simbachawene aliwaambia
wahariri kwamba mimi Zitto Kabwe ninachochea wananchi wa Mtwara, ninatumiwa, na
si mzalendo. Vile vile alitoa vielelezo kadhaa kuonyesha kuwa mradi wa kujenga
bomba la gesi ni gharama sawasawa. Akasisitiza kwamba mimi ni mwongo.
Katika kipindi chote cha mgogoro wa Gesi Mtwara, sijafika
Mtwara. Sijafanya mkutano wowote na waandishi zaidi ya kuandika mawazo yangu,
kama Mtanzania kuhusu suala hili.
Nimeandika makala nne na zimechapishwa katika magazeti
kadhaa hapa nchini na kwenye blogu yangu (http://zittokabwe.wordpress.com/).
Niliandika: Utajiri
wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania wa Mtwara na Lindi. Nikaandika
tena: Tusipuuze mandamano
dhidi ya Bomba la Gesi: Kilio cha Uwajibikaji; Nikaandika tena:
Mtwara
: Serikali inavunja nchi kwa kutosikiliza Wananchi; ni baadhi
ya makala nilizoandika kuhusiana na suala la Mtwara.
Sitaki kubishana na Naibu Waziri ama Kiongozi yeyote ya
Serikali kwa sasa. Hatuwezi kuendelea kulumbana, kuzozana, kuzodoana na
kurushiana maneno wakati nchi yetu inaungua. Huu sio wakati wa kutafuta mchawi
bali kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo mbele yetu.
Yanayotokea Mtwara ni fundisho kwetu kwa Taifa namna ya
kukabili changamoto za utajiri wa rasilimali, ili kuweka mkakati, mambo haya
yanayotokea Mtwara yasitokee tena Tanzania. Tutaweza kuzuia maafa haya iwapo
tutaweka uwazi katika mikataba, tutashirikisha wananchi kwenye unyonyaji wa
maliasili za nchi, na iwapo tutaweka uwajibikaji.
Rais Kikwete
Kikwete ana majibu; ayatoe sasa kwa wana Mtwara
Kwa mujibu wa Mpango Kabambe wa Umeme nchini (Power
System Master Plan), kulikuwa na mradi wa kufua umeme MnaziBay, ambao Rais
Jakaya Kikwete aliagiza utekelezwe mara moja. Serikali ieleze umma kuhusu mradi
huo wa kujenga kituo cha kufua umeme 300MW MnaziBay Mtwara na kujenga msongo wa
umeme wa 300KV mpaka Singida. Umeishia wapi? Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 12
Oktoba 2012, Rais Jakaya Kikwete alipokea ripoti ya ujenzi wa mradi huu kutoka
makampuni ya China National Machinery & Equipment Import & Export
Corporation (CMEC) ya China na Siemens ya Ujerumani, ambayo kwa pamoja yalitarajia
kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi katika eneo la Mnazi
Bay, mjini Mtwara na pia kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita 1,100
kutoka Mtwara hadi Singida. Mradi huu ungegarimu dola za kimarekani milioni 684
na Rais aliagiza utekelezwe haraka sana. Huu mradi uliishia wapi? Kwa nini
Serikali ipo kimya kuhusu mradi huu ambao ungejibu kabisa maswali ya watu wa
Mtwara? Taarifa ya Ikulu kuhusu mradi huu
imeambatanishwa hapa.
Tufanyeje?
Hapa tulipofikia ni lazima kwanza kabisa kusikia kilio
cha wananchi wa Mtwara ikiwemo kuelewa madai yao. Swali kubwa kubwa la watu wa
Mtwara na Kusini kwa ujumla ni ‘tunanufaikaje’? Jibu la swali hili si ahadi za
miradi bali ni vitendo. Hapa ndipo serikali inaposhindwa kushughulikia suala
hili, kutoelewa madai ya wananchi na kuyapotosha.Viongozi wa kisiasa wenye
ushawishi kutoka pande zote, chama tawala na vyama vya upinzani, waende Mtwara
kuzungumza na wananchi, lakini wawasikilize kwanza.
- Lazima viongozi tujenge utamaduni wa kusikiliza wananchi na si kuwahutubia tu. Wananchi wa Mtwara wana madai ambayo lazima viongozi tukae kitako kuwasikiliza kisha kufanya nao majadiliano ambayo yatatoa mwafaka. Rais mstaafu, Ndugu Benjamin Mkapa ameshatoa kauli kuhusu suala hili. Ni wakati mwafaka sasa kwa viogozi wengine kumuunga mkono kwa kwenda Mtwara na kukaa na wananchi wa Wilaya zote za Mtwara, kusikiliza hoja zao na kuona namna ya kupata ufumbuzi wa suala hili. Wakati hatua hii inachukuliwa, wananchi waombwe kutulia na kuacha vurugu za aina yeyote ile, na Serikali isimamishe mradi mpaka hapo suluhu na wananchi itakapopatikana.
- Wakati juhudi hizo zinaendelea Serikali iweke wazi mkataba wa ujenzi wa bomba, kwani ni dhahiri gharama za mradi huu ni kubwa mno kulingana na uhalisia wa miradi ya namna hii duniani kote. Katika taarifa zote kwa umma Serikali imekuwa ikisema kwamba mradi utagharimu jumla ya dola za kimarekani 1.2 bilioni, lakini katika taarifa ambayo Wizara ya Nishati na Madini imesambaza jana kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini imesema mradi utagharimu dola za kimarekani milioni 875. Usiri katika mkataba huu unaashiria kwamba Serikali inaficha kitu. Hivyo njia pekee ni kutaka mkataba uwe wazi kwa wananchi.
- Wakati tunawataka wananchi wa Mtwara kuruhusu utulivu, ni vema Serikali ijiandae kutoa majawabu ya madai ya wananchi hao. Majawabu ya Serikali yajikite kueleza wananchi wa Mtwara wanafaidikaje na rasilimali ya gesi asilia kwa maendeleo yao. Wananchi wa Mtwara wanataka uwajibikaji wa Serikali kwenye utajiri wa nchi, na wamechoka na porojo za orodha ya miradi isiyotekelezwa.
Viongozi twendeni Mtwara kusikiliza wananchi wetu. Nchi
inaungua na hatuwezi kuendelea kuzozana badala ya kuzima moto huu hatari kama
vita vya MajiMaji. Mimi nakwenda Mtwara haraka na mara baada ya viongozi wangu
wa chama kutoa ridhaa.
ZITTO KABWE
Mbunge, Kigoma Mjini (Chadema)
Waziri Kivuli wa Fedha
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
·
Mradi kabambe wa umeme
kujengwa
· Rais Kikwete apokea ripoti ya maandalizi
· Utagharimu mabilioni ya fedha
·
Utaunganisha mikoa yote kwenye
Gridi ya Taifa
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba 12, 2011, amepokea ripoti kutoka makampuni
mawili ya kimataifa kuhusu Mpango Kabambe ya mradi mkubwa
wa umeme ambao utaunganisha kwenye Gridi ya
Taifa mikoa yote sita ambayo
kwa sasa haiko kwenye gridi
hiyo.
Rais
Kikwete amepokea ripoti hiyo kutoka
makampuni ya China National
Machinery&Equipment Import&Export
Corporation (CMEC) ya China na
Siemens ya Ujerumani ambayo kwa pamoja
yanatarajia kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kutokana na gesi
katika eneo la Mnazi Bay, mjini Mtwara na pia
kujenga njia ya kusafirisha umeme ya kilomita
1,100 kutoka Mtwara hadi Singida.
Mradi
huo mkubwa wa umeme wa
megawati 300 utakaogharimu karibu dola za
Marekani milioni 684 na utakaozalisha umeme wa moja
kwa moja na wenye nguvu
kubwa ya 300 kV (300 kV
High Voltage Direct Current – HVDC) utagharimiwa kwa pamoja na
mkopo kutoka Benki ya Exim ya
China na Serikali ya Tanzania.
Umeme
kutokana na mradi huo utaunganishwa
kwenye gridi ya taifa na
kutoka Singida hatimaye utavutwa kupelekwa katika mikoa ya Kaskazini
Magharibi mwa Tanzania ya Kagera, Kigoma
na Rukwa ambako pia utaongeza
upatikanaji wa umeme katika machimbo
ya madini yaliyoko katika mikoa hiyo.
Kwa
mujibu wa ripoti hiyo, mbali
na mikoa hiyo mitatu, pia
mikoa ya Lindi na Mtwara
ambayo nayo haiko katika Gridi
ya Taifa nayo itaunganishwa katika Gridi hiyo
kupitia umeme huo.
Kuunganishwa
kwa mikoa hiyo sita katika
Gridi ya Taifa kupitia umeme
wa mradi huo pamoja na
Mkoa wa Ruvuma ambao utaunganishwa katika Gridi hiyo
kwa mradi unaogharimiwa na Serikali ya Sweden kutakamilisha mpango wa Serikali ya
Awamu ya Nne kuunganisha mikoa yote ya
Tanzania kwenye umeme wa Gridi ya
Taifa.
Kwa
sasa Mkoa wa Kagera unahudumiwa
na umeme kutoka Uganda, wakati Mikoa ya Kigoma
na Rukwa inahudumiwa na umeme wa mafuta
ya dizeli. Mikoa ya Mtwara
na Lindi inapata
umeme wake kutoka kampuni ya Wentworth ambao haujaunganishwa kwenye gridi ya
taifa.
Kuunganisha
mikoa yote ya Tanzania kwenye Gridi ya Taifa
ilikuwa moja ya ahadi kubwa
zilizotolewa na Serikali ya Rais
Kikwete wakati anaingia maradakani na kwa kuuunganisha
mikoa hiyo sita kwenye Gridi
hiyo, Serikali hiyo itakuwa imetimimiza
ahadi hiyo.
Akipokea
ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru
Wizara ya Fedha, Wizara ya
Nishati na Madini pamoja na
Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) kwa juhudi zao zilizofanikisha makubaliano ya kujengwa kwa mradi
huo mkubwa wa umeme ambao
utachangia kuongeza wingi wa umeme
nchini katika kipindi ambacho kwa miezi kadhaa
Tanzania imekabiliwa na mgawo wa umeme
kutokana na ukame uliokausha maji kwenye mabwawa
makubwa ya uzalishaji umeme nchini.
Rais
Kikwete pia ameitaka Wizara ya Fedha kwa
kushirikiana na Benki ya EXIM ya
China kuhakikisha kuwa fedha za kutekeleza
mradi huo zinapatikana haraka iwezekanavyo na pia ameitaka TANESCO na makampuni ya
CMEC na Siemens baada ya kupatikana kwa
fedha kuanza ujenzi wa mradi
huo kwa kasi
na kuukamilisha katika muda na
ubora unaotarajiwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
12
Oktoba, 2011
PINDA USO KWA USO NA WANAHABARI
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Habari, Wamiliki na Wahariri wa Vyombo
vya Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza
nao, kwenye makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam, Januari 25,
2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Prince Bagenda wakati alipokutana na Wajumbe wa Baraza la Habari, Wamiliki na Wahariri wa Vyombo vya Babari kwenye makazi yake, Oysterbay jijini Dar es salaam, Januari 25, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Saturday, January 26, 2013
MAMBO YA NDONDI HAYO
Francis Cheka, mmoja wa mashuhuda wa ngumi za ridhaa ya kuwapata wanandondi wa kuuwakilisha mkoa wa Kagera kwenye mashindano ya taifa, yalifanyika kwenye ukumbi wa klabu wa Lina's uliko katika manispaa ya Bukoba.
Wanandondi wakijinadi.
Mwenyekiti wa chama cha ndondi Kagera, Leoperd Kayunga, na afisa utamaduni wa mkoa wa Kagera Rugeiyamu.
Msanii Afisa Kazinja akifanya vitu vyake.
Kundi la BK Sunday aliyepiga wimbo wa SEKDO.

BONANZA KWA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI LILILOANDALIWA NA JAMBO TANZANIA
Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Kagera, Fikir Kisimba na mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali mstaafu Issa Njiku (kushoto) waliokuwa miongoni mwa walioudhuria bonanza.
Muasisi wa jambo Tanzania toka Ujerumani akitoa historia ya Jambo Tanzania.
Wanafunzi walioshiriki kwenye bonanza hilo.
Muasisi wa jambo Tanzania toka Ujerumani akitoa historia ya Jambo Tanzania.
Wanafunzi walioshiriki kwenye bonanza hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)