Thursday, September 12, 2013

JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA BINTI MDOGO .......AIBU HIYO.........


MAHAKAMA ya wilaya ya Bukoba imemhukumu Mathayo Bagaichwaki (40) mkazi wa mtaa wa Nyamkazi ulioko katika manispaa ya Bukoba kwenda jela miaka kutumikia kifungo cha miaka 30 baada kupatikana na kosa la kumbaka binti mwenye umri wa miaka 15.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu mfawidhi wa mahakama ya Bukoba, Charles Uisso baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa katika mahakama hiyo na mashahidi upande wa mashitaka uliiongozwa na wakili wa serikali Chema Mbena.

Pia hakimu huyo aliridhika na ushahidi ulitolewa na binti aliyefanyiwa unyama huo baada ya kuielezea  mahakama jinsi alivyobakwa na Bagaichwaki kabla ya kuokolewa na wazazi wake walioshirikiana na majirani. 

Katika hukumu hiyo mahakama hiyo haikuridhika na  ombi la utetezi lililokuwa limetolewa na Baigaichwaki aliyedai mashtaka yaliyokuwa yanamkabili ya ubakaji kuwa yalikuwa yakubambikizwa.

Alikuwa ameielezea mahakama kuwa alibambikizwa kesi hiyo kwa kuwa alikuwa akimdai baba mzazi wa binti aliyembaka kiasi cha shilingi 50,000.

Wakati wa hukumu hiyo ikitolewa mwendesha mashtaka wa serikali aliielezea mahakama kuwa mstakiwa hakuwa kumbukumbu zozote za uharifu ila aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mstakiwa.

Alisema adhabu kali ikitolewa dhidi ya mshtakiwa itakuwa fundisho kwa  watu wazima wenye tabia ya kujihusisha na vitendo vya ubakaji hasa kwa watoto wenye umri mdogo.

Awali mwendesha mashtaka aliielezea mahakama kuwa April 18,mwaka huu, Gabaichwaki katik maeneo ya nyamkazi alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 15 nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment