Mhe. Dkt. Diodorus Buberwa Kamala, Balozi wa
Tanzania Ubelgiji, Uholanzi, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya anayo furaha
kuwaalika Watanzania wote wanaoishi katika nchi za Ubelgiji, Uholanzi na Luxembourg
kushiriki Tamasha la Filamu za Afrika ambalo litakuwa na siku mbili maalum za kuonyesha
Filamu za Kitanzania. Filamu ya Kitanzania inayojulikana kwa jina la “A
Teachers Country” itaonyeshwa tarehe
29/03/2013 katika ukumbi wa sinema wa KINEPOLIS, Bondgenotenlaan 145, Leuven kuanzia saa mbili usiku. Aidha, tarehe 30/03/2013
Filamu za Kitanzania zinazojulikana kwa majina ya “ The Road to Sainthood na Mwalimu: The
Legacy of Julius Kambarage Nyerere” zitaonyeshwa
katika ukumbi wa Museum M, Leuven, Ubelgiji
kuanzia saa 5.30 Asubuhi. Mhe. Madaraka Nyerere atakuwa mgeni rasmi.
Wote mnakaribishwa kuja kushiriki katika
Tamasha la Filamu za Kitanzania.
Imetolewa na Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Balozi wa Tanzania
– BENELUX
21/03/2013
No comments:
Post a Comment