Thursday, March 07, 2013

MKUU WA WILAYA AMNUSURU MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA ANATORY AMANI

 Meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani ambaye sasa anakumbana na misukosuko toka kwa madiwani akiongea wakati wa kikao cha bajeti baada ya mkuu wa wilaya kumnusuru, madiwani walitaka asiendeshe kikao hicho badala yake achaguliwe meya wa muda wa kuendesha kikao hicho.


 Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Bukoba.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Bi. Ziporah Pangani akitoa maelezo ya kumnusuru meya wa manispaa ya Bukoba, baadhi ya madiwani wa manispaa hiyo walitaka asiendeshe kikao cha kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14 kwa kile walichodai kuwa anakabiliwa na tuhuma na tayari serikali imeishaagizwa kuundwa tume ya kumchunguza, mkuu huyo wa wilaya aliwataka madiwani wawe na subira wamuache aendeshe kikao hicho wakati tuhuma za ubadhilifu zinazomkabili zinachunguzwa, hali hiyo iliwafanya madiwani wakatuliza munkali wao.

No comments:

Post a Comment