BAADHI ya madiwani wa
halmashauri ya manispaa ya Bukoba wamegomea kikao cha baraza hilo na kutoka nje
ya ukumbi wa mkutano baada ya kutokea malumbano makali kati yao na mstahiki Meya wa manispaa hiyo Anatory Amani.
Hicho
kilikuwa kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo cha
kujadili masuala ya mbalimbali yakiwemo ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo na kupokea taarifa za kamati, kilifanyika kwenye ukumbi wa
halmashauri ya manispaa hiyo.
Mgogoro ulianza baada ya madiwani kuanza kuhoji baadhi
ya vipengele vya muhtasari wa kikao cha baraza la madiwani kilichopita kabla ya
kuuthibitisha, wamedai kwamba katika kikao hicho kilichopita kuwa
hawakukubaliana kurasimisha madaraka kwa kamati ya fedha na uchumi ili ifanye
mchakato wa kukopa fedha zaidi ya
shilingi milioni 450 kwa ajili ya kuwalipa wadeni.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti madiwani hao wamesema
katika kikao kilichopita hawakutoa Baraka kwa kamati ya fedha na uchumi kufanya
mchakato kukopa fedha zaidi ya shjlingi milioni 200 toka benki ya rasilimali nchini (TIB) kwa ajili ya kuilipa
kampuni ya OGM itakayosimamia ujenzi wa soko jipya la Bukoba na shilingi zaidi ya milioni 250 kwa ajili ya
ajili ya kuandaa maeneo mbadala yatakayotumiwa wafanyabiashara watakaopisha ujenzi wa soko jipya la Bukoba. .
Madiwani wa
halmashauri ya manispaa ya Bukoba kila mara wamekuwa wakidai kuwa hawana imani
na Meya Amani, kila mara wamekuwa wakimtaka aachachie ngazi kufuatia tuhuma
mbalimbali wanazozielekeza kwake, madiwani wanamtuhumu diwani kuwa anaingia
mikataba ya miradi mbalimbali ya maendeleo kinyemela, miradi anayodai meya
ameiingia kinyemela kuwa ni pamoja na ujenzi wa soko jipya la Bukoba, upimaji wa viwanja 5,000
na ujenzi wa standi kuu ya mabasi.
No comments:
Post a Comment