JESHI la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwaua watu watano wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali vya uharifu
ambavyo ni pamoja wizi wa kutumia silaha na utekaji wa magari kwenye maeneo mbalimbali
ya mapori yaliyoko mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la
polisi wa mkoa wa Kagera, Philip Kalangi amesema jeshi hilo limewaua watu hao jana baada ya kukutana nao uso kwa uso katika eneo
ya msitu wa Kalenge ulioko wilayani Biharamulo
wakati wakitoroka kuelekea wilaya ya Kakonko iliyoko mkoani Kigoma.
Anasema watuhumiwa hao baada ya kukutana na askari wa jeshi
hilo walianza kurusha risasi ovyo kwa lengo la kujiami, Kalangi amesema pamoja
na kurusha risasi hizo askari hao walifanikiwa
kuwazidi nguvu ambapo watuhumiwa wengine walilazimika kukimbilia maporini,
watuhumiwa hao walikuwa na silaha mbili aina ya SMG, risasi 35, magazine 2 na simu za mkononi nne,
vyote ambavyo viko mikononi mwa jeshi hilo.
Kalangi amesema waliouwawa
walikuwa wakisakwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kuhusika na tukio la
utekaji wa magari manne uliofanyika hivi karibuni kwenye maeneo ya Nyamagala
yaliyoko Rusaunga wilayani Biharamulo, amesema marehemu walipopekuliwa walikutwa
na vitambulisho vinaonyesha kuwa ni raia
wa nchi jirani ya Burundi.
Ametoa wito kwa wananchi waendelee kushirikiana na jeshi hilo ili
liweze kupambana na vitendo vya uharifu ambavyo vinahatarisha amani ndani ya jamii
kwa urahisi zaidi,amewaomba wananchi wamtolee taarifa mtu yoyote wanayemtilia
mashaka.
No comments:
Post a Comment