Sunday, March 10, 2013

MAMBO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE

 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akikagua batik katika  tamasha la maonyesho  ya batik ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwenye ukumbi wa Hellenic Club jijini Dar es salaam Machi 9, 2013.Tamasha hilo liliandaliwa kwa pamoja na Kamati ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (MOWE) na Shirika la kazi Duniani ILO. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda  akizungumza katika  katika Tamasha la Moanyesho ya batik ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye ukmbi wa Hellenic Club jijini Dar es salaam Machi 9, 2013. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani ILO nchini, Bw, Alexio Musindo na Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (MOWE), Egaika Mrema. Tamasha hilo liliandaliwa kwa pamoja na MOWE na ILO. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza na mke wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Sophia Mukama katika Tamasha la Maonyesho ya batik la kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani  kwenye ukumbi wa Hellenic Club jijini Dar es salaam Machi  9,2013.  Tamasha  hilo liliandaliwa kwa pamoja na Kamati  ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania  MOWE na Shirika la Kazi Duniani ILO.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment