Matokeo ya mwanzoya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta akiwa anaongoza kwa asilimia hamsini na nne dhidi ya Raila Odinga aliye na asilimia arobaini na moja.
Mamilioni ya wakenya wanatumai kuwa matokeo ya uchaguzi huu yatawaunganisha wananchi hasa baada ya ghasia kushuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Watu elfu moja na miambili waliuawa na maelfu ya wengine kuachwa bila makao.
Matokeo ya mwanzo yanaonyesha Uhuru akiongoza kwa zaidi ya asilimia hamsini dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga, 68.
Tume ya uchaguzi inasema kuwa shughuli ya kuhesabu kura huenda ikaendelea hadi Jumatano kwa sababu ya idadi kubwa ya wapiga kura walioshiriki zoezi hilo.
Hatua hii nayo huenda ikachelewesha kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu.
Watu waliendesha shughuli hiyo kwa amani kwani ndiyo ilikuwa kauli mbiu ya uchaguzi huu kwa hofu ya kutokea tena ghasia za kikabila zilizoshuhudiwa mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment