WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itatumia shilingi bilioni 55 kuvipatia
umeme vijiji 244 vya mkoa wa Mbeya kupitia Miradi ya
Umeme Vijijini (REA).
Ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Machi
2, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya
waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara yake ya siku saba kwenye mkoa huo.
Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mkapa, jijini Mbeya.
“Nimeambiwa
kuwa katika mwaka 2014/15, jumla ya vijiji 244 vitapatiwa umeme kupitia REA.
Vijiji hivyo ni kama ifuatavyo: Chunya viko 13, Mbeya ni 32, Mbarali (56),
Mbozi (14), Momba (15), Kyela (30), Ileje (18) na Rungwe (66) na jumla ya shilingi
bilioni 55/- zitatumika kwa
madhumuni hayo,” alisema.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza
viongozi wa mkoa huo kwa kusimamia suala la usambazaji wa umeme vijijini na
kukamilisha awamu ya kwanza ya miradi ya umeme vijijini katika
vijiji 17 vya mkoa huo.
“Nimeelezwa kuwa miradi hiyo iliyogharamu ya shilingi
billioni 7.6 katika vijiji 17
imekamilika kwa asilimia 100. Katika Halmashauri
ya Mbeya kuna vijiji vitano, Mbozi vijiji vinne, Chunya vijiji sita na Rungwe vijiji
viwili; na imeweza kuunganisha wateja 650,” alisema.
Alisema taarifa zinaonesha kuwa vijiji
vilivyopangwa kupata umeme wa REA mwaka 2015/2016 ni 51 na kwamba hivi sasa
ujenzi wa njia kubwa ya umeme wa 11Kv na 33Kv unaendelea. “Pia ujenzi wa njia
ndogo ya umeme 400v unaendelea kujengwa na utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia
42.3,” aliongeza.
Aliwahimiza viongozi wa mkoa huo kuongeza jitihada
za kusambaza umeme kwa kuwa mahitaji ya umeme ni makubwa kwa wananchi wengi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
No comments:
Post a Comment