NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
Wajumbe wa halmashauri
kuu ya taifa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa KAGERA wamehimizwa
kuendelea juhudi zao za kukiimarisha chama hicho kwa kubuni
mikakati ya kuleta ustawi ndani ya jamii bila kuwasikiliza
wale wanaojaribu kuwakatisha tamaa na wakati mwingine kuwabeza.
Kauli hiyo imetolewa na
katibu wa CCM wa mkoa wa KAGERA ALI AME wa hitimisho la zoezi la usambazaji wa
msaada ya majaketi maalumu yatakayowawesha waendesha pikipiki kujiepusha na
ajali wakati wa usiku na kutambuliwa pamoja na vifaa vya michezo.
Msaada huo wenye thamani
ya zaidi ya shilingi zaidi ya MILIONI SITINI na TANO umetolewa mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM taifa, NAZIR KALAMAGI na umesambaza kwa walengwa
katika vijiji TISINI na NNE vilivyoko katika kata ISHIRINI na TISA
zilizoko katika wilaya ya BUKOBA vijijini.
AME amesema mambo
yanayofanywa na wajumbe wa NEC katika mkoa wa KAGERA ya kutoa
misaada mbalimbali yenye lengo la kuleta ustawi ndani ya jamii hayahusiani na
masuala ya kampeni kama baadhi ya watu wanavyodhani ambao ni pamoja na mbunge wa jimbo la bukoba vijijini JASSON RWEIKIZA kwa kuwa muda wa kampeni za
kuwania nafasi mbalimbali za uongozi haujafika, amesema wajumbe hao
wanachokifanya ni kutekeleza wajibu na kisisitiza kwa kusema kwamba hiyo kazi
ya MNEC.
Kwa upande wake, YAHYA
KATEME ambaye ni katibu wa jumuia ya umoja wa vijana katika mkoa wa KAGERA
amesema kazi inayofanywa ya KALAMAGI ya kukiimarisha chama inapaswa
kupongezwa na kila mtu, Naye NAZIR KALAMAGI mjumbe wa halmashauri kuu CCM
taifa anaeleza sababu za kutoa msaada wa majaketi maalumu kwa waendesha
pikipiki na vifaa vya michezo, AMIDA KAGASHEKI mwenyekiti wa UWT na AMIM IBRAHIMU katibu
siasa uenezi na itikadi mkoani KAGERA wanaoelezaa kazi inayofanywa na MNEC huyo
kwamba ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM, huku DENIS ALOYS na PETER
NGEMELLA ambao ni miongoni waendesha pikipiki wakieleza msaada
utakavyowanufaisha.
KALAMAGI ni miongozi mwa wajumbe wa halmashauri ambao wametekeleza wajibu wao vizuri, amekuwa wakitoa misaada mbalimbali ambayo ni pamoja uungaji mkono wa ujenzi wa
vyumba vya maabara, kukiimarisha chama kuanzia ngazi ya kata, hali hii
inampelekea mbunge RWEIKIZA kulalamika kwamba MNEC huyo anayafanya yote hayo kwa lengo la
kuwania nafasi ya ubunge, kauli ambayo wananchi wameitafsiri kuwa ni woga alionao kwa kuwa hakutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2010
No comments:
Post a Comment