NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
Kufuatia matukio yanayofanywa na watu wasiojulikana katika kata
ya KITENDAGULO iliyoko manispaa ya
BUKOBA ya kuwauna watu kwa kuwakata kata
na mapanga yanayohusishwa na imani za kishirikina, serikali imewaomba wananchi
kuwafichua wale wote wanaowahisi wanaojihusisha na matukio hayo badala ya
kuwaonea aibu ili waendelee kuishi kwa amani na kwa usalama zaidi.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya BUKOBA, JACKON
MSOME ambaye amekutana na na wananchi wa
mtaa ya KAGEMU ulioko katika kata ya KITENDAGULO kwa lengo la kuwapa pole ndugu
na jamaa wa marehemu WAWILI waliouwawa kwa siku moja katika kata hiyo kwa
kukatwa katwa na mapanga.
MSOME amewaambia wananchi kuwafichua wale wote wanawatilia
mashaka kwa kutoa taarifa juu yao kwa
kiongozi yoyote bila bla kuwaonea aibu
na bila kujali nafasi yao wallizonazo ndani ya jamii ili serikali iweze
kuwachukulia hatua za kisheria.
Kwa upande wake,Mkuu wa kituo cha polisi cha kati Bukoba,
FRANK UTONGO amewahakikishia wananchi kuwa jeshi hilo litafanya doria endelevu
katika kata hiyo, nao baadhi ya wananchi katika kata hiyo ambao
n FRANCIS RWEGASIRA na DEOGRATIAS
RUSIZOKA ni miongoni mwa wananchi katika mkoa wa KAGERA wanaotoa ushauri wa
namna ya kudhibiti vitendo hivyo.
Kata ya KITENGAGURO ni kata ziliko mkoani KAGERA ambayo
imekubwa na wimbi la mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana, mauaji katika
kata hiyo yalianza tangu mwishoni mwa mwaka jana, hadi sasa zaidi ya watu NANE
wameishauwawa.
No comments:
Post a Comment