NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA, TANZANIA +255 784 939586/ 753 844 995
Watanzania wameshauriwa kuzipuuza kauli za ushawishi zinazotolewa na na baadhi ya viongozi wa
vyama vya siasa zenye lengo la
kuikwamisha rasimu ya katiba ya jamhuri
ya muungano iliyopendeklezwa kwa maslahi ya vyama vyao vya siasa badala yake
waisome kwa umakni zaidi katiba hiyo ili waipigie kura kulingana na
namna walivyoielewa.
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wadau mbalimbali ambao ni
pamoja na viongozi wa madhehebu ya dihi, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya
kiserikali na asazi za kiraia wakati wa hafla
fupi ya uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa katiba kwa wananchi uliofanywa na halmashauri ya manispaa ya BUKOBA.
Wamesema wale
wanaojaribu kuwashawishi wananchi waipigie kura ya hapana katiba
iliyopendekezwa kwamba hawana nia njema
na nchi hii, waliahidi kutumia nafasi zao walizonazo kuwahamasisha wanachi
waisome katiba ili wachukue uamzi ulio
sahihi wakati muda kuipigia kura ukifika kama wanavyoeleza.
Lengo la kusambaza rasimu ya katika iliyopendekezwa kwa wananchi
ni kuhakikisha wananchi wanapata fiursa
ya kuisoma na kuielewa kabla ya kuipigia kura .
No comments:
Post a Comment