NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
Vitendo vya mauaji vinavyofanywa
na watu wasiojulikana katika kata ya
KITENDAGURO iliyoko katika halmashauri
ya manispaa ya BUKOBA wavimeendelea kukithiri , kukithiri kwa vitendo hivyo
kunafuatia kuuawa kwa watu wengine wawili
kwa nyakati tofauti katika maeneo
ya kata hiyo waliokatwa kukatwa katwa na
mapanga kichwani.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la
polisi mkoani KAGERA, kamishina msaidizi wa jeshi hilo, HENRY MWAIBAMBE amewataja
watu waliuwawa kuwa ni
pamoja na EMANI DILIDI aliyekuwa akiiishi katika mkazi wa
mtaa wa KANAZI na EVALIST MALISELI aliyekuwa akiishi mtaa wa KAGEMU.
Kufuatia kwa mauaji hayo MWAIBAMBE amesema jeshi la polisi
mkoani KAGERA linawashikilia watu KUMI na WAWILI kwa tuhuma ya kuhusika na
mauaji hayo, amewaomba wananchi kulipa ushirikiano keshi hilo ili liweze
kuwabainiwanaojihusisha na matukio hayo ya mauaji pamojana kueleza kwamba jeshi
hilo kwamba linayafanyia uchunguzi wa
kina matukio hayo.
Vitendo vya mauaji ya
watu katika kata ya KITENDAGULO iliyoko
katika manispaa ya BUKOBA vilianza tangu
mwaka jana, hadi sasa zaidi ya watu KUMI
wameishauwawa kwa kukatwa katwa na
mapanga na watu wasiojulikana, mauaji hayo yamewajenga hofu kubwa wananchi
katika kata hiyo hadi kufikia hatua ya kutotembea wakati wa usiku.
No comments:
Post a Comment