Wednesday, August 28, 2013

Watoto hunyanyaswa migodini Tanzania



Maelfu ya watoto wanaofanya kazi katika machimbo ya madini nchini Tanzania wanakabiliwa na tishio kubwa la kupata magonjwa na hatimaye kufa.
Shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch, limefichua ushahidi zaidi kuhusu unyanyazaji wa watoto nchini Tanzania, baadhi yao wenye umri wa miaka minane ambao wanafanya kazi kwa zamu, katika migodi ya madini iliyoko chini ya ardhi, kwa saa ishirini na nne.
Shirika hilo limesema watoto hao wanakabiliwa na tishio la kuvuta hewa ya sumu inayotokana na uchimbaji wa madini ya dhahabu na wakati mwingine kuuawa wakati migodi hiyo, inapoporomoka nyingi zikiwa hazina leseni.
Tanzania ina sheria kali inayozuia watoto kufanya kazi katika machimbo ya madini lakini shirika hilo limesema, serikali ya rais Jakaya Kikwete ni sharti iimarishe juhudi zake za kuhakikisha sheria hizo zimetekelezwa.

No comments:

Post a Comment