Marekani imeachana na jitihada
za kutafuta uungwaji mkono wa baraza la usalama la umoja wa mataifa
kuichukulia hatua Syria kwa utumiaji silaha za kemikali.
Hii ni kufuatia kukataa Urusi kwa rasimu ya maazimio yaliowasilishwa kwenye mkutano wa wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo la usalama.
Akilaumu Urusi kwa kile alisema msimamo wake wa
kutobadili maoni kwa chochote, Msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni,
Maria Harf amsema kuwa Marekani haitaruhusu alichotaja kama uzembe wa
kidiplomasia kutumiwa kama ngao ya kutetea Serikali ya Syria. Azimio
lilioandikwa na Uingereza lingaliruhusu hatua za kuwalinda raia wa Syria
lakini likapingwa na Urusi katika kikao cha wanachama watano wa kudumu
katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Hii ni kufuatia kukataa Urusi kwa rasimu ya maazimio yaliowasilishwa kwenye mkutano wa wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo la usalama.
Msemaji huyo alielezea hali ya Marekani ya kutoridhika na hali ya upole inayoendelea katika Umoja wa Mataifa, na akasisitiza kwamba kwa wakati huu Marekani haioni matumaini yoyote ya kuungwa mkono na Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa na kwa sasa itatilia mkazo mashauriano na mataifa mengine washirika kabla ya kuchukua hatua yoyote inayofaa hivi karibuni.
Alisema kuwa hadi kufikia sasa Rais Obama hajafanya uamuzi wowote juu ya hatua inayopaswa kuchukuliwa, lakini akaongeza kuwa ni dhahiri kuwa silaha za kemikali zilitumiwa nchini Syria na kwamba wa kulaumiwa ni utawala wa Rais Assad.
No comments:
Post a Comment