YAH:SABABU ZA KUUNGA MKONO UAMUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO NA
VILABU KUKATAA KUSAJILI MAREKEBISHO YA
KATIBA YA TFF KUTOKANA UKIUKWAJI
WA UTARATIBU NA SHERIA ZA MAREKEBISHO YA KATIBA TFF 2013
Katiba ya TFF ya 2012 ilifutwa na msajIli wa vyama
vya michezo na vilabu kwa kuwa ilibadilishwa kinyume cha sheria(BMT) pamoja na Katiba ya TFF ibara ya 30 kwa kutumia njia ya waraka badala ya Mkutano
Mkuu, hivyo katiba halali kisheria
inayotambulika ni ile ya 2006 na mabadiliko yake . FIFA na Serekali kupitia wizara yenye dhamana
na michezo iliiagiza TFF iitishe Mkutano Mkuu ili ifanye mabadiliko
ya katiba stahiki kwa mujibu wa katiba
na kwa kufuata taratibu zilivyoainishwa kwenye katiba ya TFF. Nimelazimika kuendelea
kuiunga mkono Serikali kupitia msajili kwa maamuzi yake ya kukataa kusajili
mabadiliko ya katiba ya TFF kwa kuwa
TFF kwa makusudi imeendelea kuvunja katiba yake katika kufanya
mabadiliko.
Kisheria msajili husajili mabadiliko yoyote ya Chama
kilichosajiliwa chini ya Sheria ya BMT kwa kuzingatia Sheria NA
12 ya 1967 na marekebisho yake NA 6
ya 1971 ya Baraza la Taifa la Michezo pamoja na Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa na Kanuni za Usajili NA
422 za1999.
Chama
chochote kitakacho kwenda kinyume na sheria hizo hikiwezi kupewa usajili au
Katiba yake na marekebisho yake hayawezi kupewa usajili,aidha uamuzi wa
msajili sio tu utaifanya TFF peke yake
itambue sheria bali hata vyama vingine
vitawajibika kufuata utaratibu katika kufanya mabadiliko ya katiba zao,
Katiba ni nyaraka ya kisheria hivyo chombo chenye
mamlaka kisheria hapa Tanzania ya kutafsiri katiba ni Mahakama pale pande mbili
zinapotofautiana juu ya tafssiri ya Katiba, hivyo kwa kufanya hivyo msajili
atakuwa ameepusha suala la Katiba ya TFF kuingia katika mikono ya kimahakama
kwa kuwa utaratibu uliotumika kubadili katiba ya TFF ni dhahiri haukufuata taratibu zilizoainishwa
kwenye katiba ya TFF na sheria na za nchi kama zilivyoaanishwa. Sababu kuu
zinazonipelekea mimi kuunga mkono uamuzi huo ni kama zifuatazo:
1.
UPIGAJI KURA MAREKEBISHO YA KTIBA
Ibara ya 30(4) ya katiba ya TFF 2006 inaelekeza
ya kuwa mapendekezo ya mabadiliko ya katiba ya
yatapitishwa ikiwa yataridhiwa na wajumbe theluthi mbili(2/3) ya wajumbe wenye haki ya kupiga kura.
·
Ibara ya 28(4) maamuzi yote ya mkutano mkuu yatafanywa kwa kuzingatia uwingi wa kura halali zitakazopigwa
na wajumbe halali wa Mkutano Mkuu labda
ikiwa katiba ya TFF inaelekeza vinginevyo. “ Unless otherwise stipulated
in the statutes the decisions of the general assembly shall be taken by simple
majority of the votes validly cast by
the official delegates”.
·
Ibara 28(5) ya katiba ya TFF(MAAMUZ)
Inazungumzia
Maamuzi yanayohusiana na mabadiliko
yoyote ya makao makuu ya TFF, mabadiliko yoyote ya Katiba na Kanuni zake, marekebisho
yoyote ya ajenda kwenye mkutano mkuu wa
kawaida, maamuz iyoyote yanayohusiana na
kusimamishwa au kufukuzwa mjumbe wa vyombo vya TFF au inayohusiana na kuvuliwa
hadhi ya Urais wa heshima au mwanachama
wa TFF au inayohusiana na kutengwa kwa mwanachama au kuvunjika kwa TFF lazima itahitaji zaidi ya 2/3 ya kura halali zililizopigwa na
wajumbe resmi wa Mkutano Mku “ Decision relating to any change
of head office of TFF ,any amendments of
Statutes and regulations, any modification to the agenda of the ordinary general assembly, any
decision relating to suspension or
dismissal of member a member of an organ of TFF or relating to bestowing of the title of
honorary president or member of the TFF or relating to the exclusion of a
member of TFF or dissolution of TFF shall require a majority of 2/3 of the
votes validly cast by the official delegates”.
Kwa kuwa
hakuna kura zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kuhesabiwa kuamua ama kupitisha au kukataa mabadiliko
basi zoezi hilo na marekebisho hayo ni batili kwa mujibu wa Katiba ya TFF.
2.
MKUTANO MKUU WA DHARURA
Ibara ya
25(4) katiba ya TFF ya 2006 inaelekeza kuwa
Agenda na makabrasha ya Mkutano Mkuu
ni lazima yawafikie wajumbe wa mkutano mkuu walau siku 15 kabla ya mkutano Mkuu.
Kwa kuwa wajumbe walipewa agenda na makabrasha
siku moja kabla ya Mkutano Mkuu, huo
ulikuwa uvunjaji mkubwa wa Katiba ya TFF , wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF
hawajiwakilishi wao bali wana wakilisha
Mikoa, Vyama shirikishi na Vilabu
ambavyo vina wanachama wake na
kamati zake za utendaji ambazo zilikuwa na haki ya kujadili na kuwapa
wawakilishi wao mawazo yao kwani maamuzi ya ya TFF yanagusa kuanzia ngazi ya Taifa mpaka wilaya.
3.
KUINGIZA VIFUNGU KWENYE KATIBA BILA KUJADILIWA NA
KUPITISHWA NA MKUTNO MKUU WA TFF
Kwa kuwa
marekebisho ya katiba kwa kutumia waraka
ya 2012 yaliyowasilishwa kwa msajili,
usajili wake ulifutwa hiyo maraekebisho yote yaliyofanyika wakati huo ikiwa ni
pamoja ibara Ibara 52 (1(b),2,3,4,5,6(a,b)
yanayohusu Kamati ya Uchaguzi na
kamati ya Rufaa ya Uchaguzi iliyopelekea
Uteuzi wa Mtinginjola na kamati yake , pamoja na
Ibara ya 64(1,2) ya leseni za vilabu yanakuwa batili, hivyo kama TFF ilikuwa bado inapenda
vifungu hivyo viwemo kwenye marekebesho ya katiba ya 2013, basi njia sahihi
ilikuwa ni kuwasilisha maombi kwenye
mkutano Mkuu wa TFF 13/7/2013 kwa mujibu wa Katiba ya TFF ibara 30 (2006).
Kwakuwa TFF haikupeleka maombi ya mabadiliko haya na kupitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF 2013
hivyo kuyaingiza kwenye katiba ya sasa ya 2013 na kuyaombea usajili kwa msajili
ni kinyume na sheria na Katiba ya TFF, tafsiri rahisi ni kuwa TFF ilitaka kuonyesha kwa Umma wa Watanzania ya kuwa serekali kupita msajili wa vyama vya
michezo haikuifuta na haikuwa na mamlaka
ya kuifuta katiba ya Tff na mabadiliko yake ya Desemba 2012.
4.
UUNDWAJI WA KAMATI KABLA YA MAREKEBISHO YA KATIBA
KUSAJILIWA.
TFF
iliamua kuunda kamati zake hata kabla katiba haijasajiliwa na Msajili wa vyama
vya michezo na vilabu, hii naonyesha jinsi ambavyo mfumo mbovu ulivyozoeleka
huko nyuma ambapo msajili alikuwa akisajili
katiba bila kuzingatia mapungufu hivyo kufanya vyama vya michezo kuwa
kama mali za watu binafsi na hata wakati
mwingine kumuona msajili kama sehemu ya vyama vyao jambo ambalo Wizara imeamua
kulifuta na kuhakikisha taratibu zinafuatwa.
Kwa mujibu
wa katiba ya TFF ibara ya37(3)i (2006) Rais wa TFF anayo mamalaka ya kupendekeza kwa
kamati ya Utendaji majina ya wajumbe wa vyombo vya TFF(TFF
Organs) zilizoko kwenye katiba ya TFF ibara ya 44(a,b)(kamati ya nidhamu na Rufaa),ibara
48(mahakama ya usuluhishi,49(Kamati ya Uchaguzi), pamoja na kamati ndogo ndogo
(standing Committees) zilizoainishwa kwenye
Ibara ya 39(1)a-i, isipokuwa hana mamlaka ya kuteua wajumbe wa kamati za
vyombo ya TFFambavyo havimo kwenye katiba ya TFF (2006) kama kamati
ya Rufaa ya Uchaguzi, kamati ya Maadili na Kamati ya Rufaa ya Maadili.
Uteuzi wa Majaji na Wanasheria waandaamizi kuingia kuongoza kamati ambazo
zina utatata wa kisheria kumeidhalilisha
sana idara ya Mahakama na wanasheria kwa Ujumla hali ambayo huenda kwa siku za
usoni Majaji / Mahakimu na wanasheria waandamizi hawataweza kukubali kushirikiana tena na TFF. Hata hivyo uundwaji wa kamati hizi ni
dhahiri ulikuwa ni wa hila kwa kuwateua majaji ili ionekana haki ingetendeka
huku TFF ikijua wazi maamuzi yao kwa mujibu wa katiba yanazingatia upigaji wa
kura zaidi pale pande mbili zinapopingana kwani ukiachila majaji kwenye kamati
hizi wajumbe wanaobaki ni wale wale
ambao kwa mtindo wa Kura wanakuwa wengi(wengi wape)
TFF inaelekeza
kuwasilisha malalamiko ya uchaguzi
kwenye vyombo vyake ambavyo ndio
hivyo vilivyo haribu mchakato wa Uchaguzi ambao hadi sas haujafanyika.Katika
kuonyesha dhamira isiyo nzuri ya kutaka kuwa na uchaguzi usiokuwa huru na wa
haki TFF imewateua na kuwabadilisha
wajumbe ambao kwa sehemu kubwa walishiriki kuharibu mchakato wa uchaguzi
uliopita kwa kuwapa majukumu ambayo kwa
njia moja au nyingine bado watashiriki katika mchakato wa uchaguzi unatarajia
kufanyika siku za hivi karibuni, mfano ni wajumbe 3 kati ya 5 waliokuwa kwenye kamati ya Rufaa ya chaguzi ya TFF
wamehamishiwa kwenye Kamati ya Maadili
ya TFF(Francis KebweMohamed Mpinga,madundo Mtambo na mmoja( Murtaza Mangungu Kamati ya Rufaa ya Maadili,aidha wajumbe 4 wa kamati ya Uchaguzi Kati ya 5
wamebakishwa kwenye kamati ilie ile na wawili kati yao wamepandishwa vyeo na kuwa mwenyekiti na
Makamu wa Kamati hizo ambao Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti),
Hassan Dyamwale na Kitwana Manara. Katika shauri lilifunguliwa mahakama kuu M.A. Ndolanga & others v National Sports
Council and Other [HCT, 1996,
TLR 325,Bubeshi,J.] lililohusu uchaguzi
mkuu wa FAT ambalo maamuzi yake hayajawahi kutenguliwa na mahakama nyingine ya
juu nchini mpaka sasa, matatizo kama haya yalijitokeza na ambapo
mahakama pamoja na hoja nyingine ilitaka kujua:) (i)
Kama Kamati ya Usaili ya uchaguzi ya BMT iliundwa kwa kufuata misingi ya sheria? (ii) Kama kamati ya usaili ya Uchaguzi ya BMT ilifanya kazi kwa kuzingatia
haki asili za kimsingi (Natural Justice and Fair Play) UAMUZI WA MAHAKAMA ULIMPA USHINDI M.A.
NDOLAGA Mahakama iliamua kuwa Vyombo vya maamuzi vya kiutawala wakati wa
kutekeleza majukumu yake ambayo yanahitaji kutambuliwa kisheria, vinawajbu wa
kutenda kwa kufuata sheria kwa kuzingatia haki za msingi ikwa na maana ya
kufuata utaratibu ambao msingi wake utahitaji Uhuru nje ya maslahi na upendeleo
kutoka upande wa chombo cha maamuzi kiutawala na haki ya uwazi ya kusikilizwa kwa wale ambao wataathiriwa moja
kwa moja na maamuzi. “it is trite to remark that an administrative body exercising functions
that impinge directly on legal recognized interests, owes it as a duty to act
judicially in accordance with the rule of natural justice which basically means the adoption of procedure, which fundamentally demand freedom
from interest and bias on the part of the administrative body and the right to
fair hearing for those who are immediately affected by its decision”(pg 333)
Kwa kuwa
uundwaji na malengo ya kamati hizi zina
walakini kisheria ni wazi uwezekano wa wadau kutafuta msaada wa kisheria
mahakamani unaweza kujitokeza kwa kzingatia ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi
(Natural Justice) na Katiba ya TFF inavyoelekeza
5.
UKOMO WA MADARAKA WA VIONGOZI WA VYAMA
TFF imehusishwa
sana na hila na nia ya kuvuruga uchaguzi ili
waandelee kuliongoza shirikisho kinyume na katibaTFF Ibara ya 33 ya
katiba ya tff inazungumzia Ukomo wa madaraka ni miaka 4 na uongozi wao ulikoma
Desemba 2012 hivyo uongozi huu kuendelea
kuwepo madarakani na kufanya marekebisho ya katiba ni kinyume na katiba ya TFF na sheria ya BMT ibara 15(1)a. “chama cha mchezo wowote kilichojishirikisha na BMT kitakuwa na wajibu
wa kufanya kazi zote za chama kwa msingi wa katiba yake” kwa mujibu wa
Katiba ya na kanuni za usajili wa vyama vya michezo kisheria isinge kuwa halali
kw a msajili kusajili marekebisho ya Katiba ya TFF kwa kuwa yanapingana na
sheria za BMT na Msajili kifungu7(1,2,3,4&5). Vinavyo someka kama
ifuatavyo:
·
7(1). “Kipindi cha Uongozi wa Chama chochote kitamalizika mara kipindi cha
kufanya uchaguzi mwingine kitakapokuwa kimefika kwa mujibu wa katiba ya chama “
ambapo TFFilikuwa Dec 2012
·
7(3) “Viongozi wanaomaliza muda wao
watatakiwa waitisha mkutano mkuu wa Uchaguzi katika Kipindi ha siku 30 kabla ya
siku ya ya mwisho ya kipindi cha Uongozi” Jambo ambalo TFF haikulifanya kwa
makusudi kwa kingizio cha kupisha mabadiliko ya
katiba kwa njia ya waraka ambayo ni kinuyume cha Katiba Ya TFF.
·
7(4). “Endapo siku 30 zitamalizika baada ya kipindi cha uongozi kumalizika
bila ya uchaguzi kufanyika ,na bila ridhaa ya wanachama wa chama husika,
viongozi wanaomaliza muda wao watahesabika kuwa wamejivua Uongozi” kwa kuwa Uongozi wa TFF haujapata ridhaa ya
kuendelea kuongoza TFF kutoka kwa
wanachama wake. kisheria hawakuwa na mamalaka ya kufanya na
kusimamia mabadiliko ya katiba hivyo
msajili kuyakataa ni utekelezaji wa sheria za nchi.
·
7(5). “ Endapo Viongozi wanaomaliza muda wao wamepata ridhaa ya
wanachama kuendelea kuongoza baada ya kipindi cha uongozi kumalizika, wanaweza
kukiongoza chama husika kwa kipindi
kisicho siku 90 tu baada ya siku ya mwisho ya kipindi cha uongozi. Hata hivyo,
ridhaa ya wanachama lazima iwe
imepatikana kabla yatarehe ya mwisho ya kipindi cha Uongozi”.
Kwa
mantiki hii Kamati ya Utendaji ilimalizi muda wake 14/12/2012 na haijaahi
kupatiwa ridhaa na wanachama wake na hata kama ingepata ridhaa, ridhaa hiyo
ilikuwa na ukomo mwezi wa March 2013 , hivyo kamati hii haikuwapo kihalali
wakati wa mchakato wa kubadilisha katiba na hivyo kwenda kinyume kanuni za Usajili
wa vyama vya michezo 11(1)d
“ mabadiliko hayo hayafai kwa kuwa hayakuzingatia Sera ya Michezo ,Sera ya
Utamaduni na sheria ya Baraza la Michezo”
6.
HILA ZA
KUVURUGA MCHAKATO WA UCHAGUZI
TFF imejiongezea muda wa kukaa madarakani
zaidi ya Miezi 7 sio kwa sababu yoyote ya msingi zaidi ya mikakati yenye hila
ya kuwaondoa wagombea wasiowahitaji
tangu wakati wa kurekebisha katiba kwa njia za hila za waraka ili kuunda kamati
zitakazo tekeleza malengo yao na hadi
sasa wanaendelea na mkakati huo ili kuidhalilisha serekali kwa kuwa ilionyesha
msimomo wake wa kutaka wagombea watendewe haki, swali ni vipi watu walioharibu
mchakato wa uchaguzi uliolalamikiwa na Wadau na serekeli wapandishwe vyeo tena
washiriki katika mchakato huo huo wa uchaguzi na ni vipi watu ambao
hawakuwatendea haki wagombea kwa kuwakata na kuwaondoa kwenye mchakato kwa hila
mara ya kwanza watatenda haki tena. Hii
ni kinyume na sheria za BMT na kanuni za
msajili Kifugu 11(3)b.kwa kuwa nia ya TFF ni kuwanufaisha wachache
Kwa kuwa Marekebisho ya Katiba ya Tff
hayakuzingatia katiba ya TFF na sheria za BMT na Kanuni za Msajili wa Vyama
ninaunga mkono uamuzi wa Msajili kukataa kusajili mabadiliko haya kwa kuzingatia kanuni za msajili kama ifuatavyo:
·
11(3)a, Mabadiliko hayo yanaweza
kuhatarisha usalama na kuvuruga amani miongoni mwa
wanachama na jamii kwa ujumla na
hivyo kuathiri maeneleo ya chama”.
·
11(1)b, Mabadiliko hayo
yanalenga kuwanufaisha wachache”.
·
11(1)d, mabadiliko hayo hayafai
kwa kuwa hayakuzingatia Sera ya Michezo
,Sera ya Utamaduni na sheria ya Baraza
la Michezo.
USHAURI: 1. Kwa Kamati ya Utendaji chini ya L.C Tenga
imemaliza muda wake kisheria na imeshindwa
kwa mara nyingine kuandaa katiba ili
kuipeleka TFF katiak Uchaguzi ambao utakuwa wa haki na huri ni vizuri na
busara inaelekeza kwa Bwn Tenga na kamati yake kawajibika
kwa kujiuzulu ili kupisha uundwaji wa kamati ya mpito (normalization Committee)
kama ilivyofanyika nchi za Sieraleon, Gambia, Cameroon na Tanzania(2001)ili
kuandaa njia huru kuelekea uchaguzi mkuu
kupata viongozi wapya. 2. Kwa kuwa Uongozi uliopa madarakani
kwa makusudi umekiuka katiba ya TFF kwa mara ya pili, Msajili atumie kifungu 10(1)a,b
(kukiuka katiba ya Chama) za kanuni ya Usajili kuwawajibisha viongozi hawa wa
TFF waliomaliza muda wao. Kifungu “10(1).b endapo itabainika kuwa
kiongozi au viongozi wnaendesha shughuli za chama bila kufuata katiba iliopo au
kukiuka kwa makusudi vifungu vya katiba ya chama,msajili anaweza kuchukua hatua
ikiwa ni pamoja kufutwa uongozi kwa
kipindi cha uongozi kilichobaki”.
No comments:
Post a Comment