Friday, August 23, 2013

Tsvangirai atuhumiwa kudharau mahakama

Morgan Tsvangirai
Morgan Tsvangirai amekua akisisitiza kwamba uchaguzi mkuu wa Zimbabwe ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe, Morgan Tvangirai anakabiliwa na makosa ya kudharau mahakama kufuatia matamshi aliyoyatoa kuhusiana na idara hiyo.
Jaji wa mahakama kuu Chinembiri Bhunu amesema waendesha mashtaka watafahamishwa kuhusu tuhuma hizo. Haya yanajiri wakati chama cha Tsvangirai cha Movement For Democratic Change kimepoteza kesi mbili kulalamikia uchaguzi mkuu wa Julai 31 mwaka huu.
Mahakama ya kikatiba ilitangaza kwamba Rais Robert Mugabe alishinda uchaguzi kwa njiya huru na haki. Mugabe alipata asili mia 61 ya kura dhidi ya asili mia 34 alizopata Bw. Tsvangirai.
Viongozi hao wamekuwa katika utawala wa kugawana madaraka ulioafikiwa mwaka 2009 kufuatia uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata. Chama cha MDC kiliondoa kesi yake mbele ya mahakama ya kikatiba kikisema hakikua imani ya kupata haki.

No comments:

Post a Comment