1.)
Kutokana na kutokuwepo na taarifa sahihi kuhusu deni la Taifa kuna
umuhimu wa kukutanisha wadau wakuu wanaohusika hususani BOT, HAZINA,
Kamati za Bunge na CAG ili kuweza kujua kwa usahihi zaidi ukubwa wa deni
hilo. Vile vile imeamuliwa kuwa Serikali ishauriwe kuunda chombo huru
kitakachosimamia deni la taifa.
2.)
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma haiweki uwazi wa kutangaza
umiliki wa mali za viongozi. Hii inapelekea viongozi kutoweka wazi mali
wanazomiliki na ni rahisi mtu kuzushiwa umiliki usio wa ukweli. Ni
vyema Sekretarieti wakafanya utafiti wa umiliki wa mali kwa viongozi wa
Umma na kuweka taarifa hizo katika tovuti ya Sekretariati ili
kuwawezesha wananchi kuweza kuona mali zinazomilikiwa na viongozi wao;
na pale ambapo kiongozi hatakuwa ametoa taarifa ya umiliki huo basi
taarifa hiyo itolewe kwa Tume.
3.)
Kwa kuwa leseni za udereva za sasa zinaweza kuweka kumbukumbu za makosa
ya usalama barabarani, basi TRA ikishirikiana na Wizara ya Mambo ya
Ndani zihakikishe ya kuwa Askari wa Usalama Barabarani wanatumia
utaratibu huu wa kisasa wa kutoa “notification” na kutoa risiti za
malipo za elektroniki.
4.)
Maduhuli ya Serikali sasa yakusanywe kwa kutumia risiti za
elektroniki. Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma
yaanze kutumia risiti za eletroniki mara moja ili kudhibiti upotevu wa
mapato ya serikali yanayotokea hivi sasa katika kutumia risiti
zinazoandikwa kwa mkono. Pia ofisi za serikali zifanye manunuzi yake kwa
wafanyabiashara wanaotumia mashine za kielektroniki.
5.)
“The Proceeds of Crime Act, 1991” ifanyiwe marekebisho na kuweka
kifungu kinachomwezesha AG/DPP kuwa na mamlaka ya kuomba mahakama
kufungua kesi ya madai (Civil Forfeiture) kwa watu wanaotuhumiwa kwa
ufisadi.
No comments:
Post a Comment