MGOGORO kati ya madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba
walio kwenye harakati za kumg’oa Mstahiki
Meya wa halmashauri ya manispaa hiyo
Anatory Amani hiyo ambao
halmashauri kuu ya mkoa wa Kagera katika kikao chake ilitangaza kuwavua
uanachama umeanza kuwagawa viongozi ndani ya cha hicho kuanzia
ngazi ya mkoa ahadi kitaifa.
Mgawanyiko wa viongozi hao ulianza pale Katibu wa itifaki na uenezi wa wa chama hicho
taifa, Nape Mnauye alipotoa msimamo wa chama hicho kwa kufuta maamuzi yaliyotolewa na halmashauri hiyo kuu
ya mkoa huo ya kuwavua uanachama madiwani 8 wa CCM wanaotaka kumg’oa Meya Amani kwa kusema kuwa hayakuwa sahihi.
Mnauye alitoa msimamo wa chama hicho wakati wa kikao chake
na waandishi wa habari kilichofanyika kwenye ofisi ya chama hicho iliyoko mtaa
wa Lumumba jijini Dar es salaam, agosti 14, mwaka huu.
Katika kikao hicho Nape aliwaambia waandishi wa habari kuwa
kikao kilichowavua madiwani hao uanachama wa chama hicho kuwa kilikuwa sio
kikao rasmi cha halmashauri kuu ya mkoa ya CCM, katika kikao hicho Mnauye
alisema kuwa uamzi ulitolewa na halmashauri kuu ni batili hivyo hauwazuii
kuendelea na shughili zao za kuwatumikia wananchi.
Katika kikao hicho Mnauye alisema kikao kitakachotoa hatima
ya mgogoro kati ya Meya Amani na madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba
ni kile cha halmashauri kuu ya taifa kitakachofanyika Agosti 18, mwaka huu
mjini Dodoma.
Katika hali isiyo ya kawaida umazi ulitolewa na Mnauye wa
kuwanusuru madiwani hao ulipingwa vikali na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho
taifa Philip Mangula ambaye alisema kuwa anaunga mkono maamuzi yaliyotolewa na
halmashauri kuu ya taifa ya kuwavua uanachama madiwani wa CCM walio kwenye
harakati ya kumg’oa meya Anatory Amani.
Mangula alisema maamuzi yaliyotolewa na Nape yalikuwa yake
binafsi na wala sio ya chama, alisema kikao kilichowavua uanachama madiwani hao
kuwa kilichokuwa sahihi, kauli ambayo inapingana na iliyotolewa na Mnauye kuwa
kilikuwa batili.
Kufuatia hali hiyo ya viongozi wa chama hicho kuchanganyana ,
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kagera Bi. Costancia Buhiye jana alikutana na
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa jengo la chama hicho kuelezea maamuzi
sahihi ya chama hicho.
Katika Kikao hicho na waandishi wa habari Bi. Buhiye alisema
maamuzi yanayoheshimiwa ni yale yaliyotolewa na Makamu wa CCM taifa, Mangula na
wala sio yaliyotolewa na Nape Mnauye juu ya sakata la kuwavua baadhi ya
madiwani kupitia katika chama hicho uanachama.
Alisema maamuzi yaliyotolewa na Mnauye ni batili hivyo
wananchi hasa wanachama wa CCM hawapaswi kuyasikiliza kwa kuwa yana lengo la
kukigawa chama hicho, “kikao kilichogtoa maamuzi ya kuwavua uanachama madiwani
kilikuwa sahihi kabisa wale wanaosema mengine wana mambo yao” alisema Bi.
Buhiye kwa msisitizo.
Mwenyekiti huyo alisema CCM haiwezi kuendelea kuwakumbatia
madiwani wanaochangia kukwamisha maendeleo, “madiwani hawa tumewavumilia sana,
wakiitwa kwenye vikao hawaudhurii, kisa eti hawana imani na Meya” alisema.
“Ndugu nawaambia waandishi tume mbalimbali zimeundwa
kuchunguza mgogoro kati ya madiwani na Meya, sasa tunasubili majibu, ziko
nyingi inaonekana madiwani hawa hawana subira” alimaliza.
Kauli hiyi inapingwa na madiwani wanaompinga Meya, kwa
nyakati tofauti walisema kuwa baadhi ya viongozi ndani ya CCM kuwa ndio
wanachangia kukua kwa mgogoro kati ya Meya na Madiwani, walisema baadhi ya
viongozi hao wanamkumbatia meya kwa maslahi yao binafsi.
Bila kutaka majina yao yatajwe walisema Meya ni mmoja wa
viongozi ambao wanataka kuifilisi halmashauri ya manispaa ya Bukoba, walisema
wanachokipinga ni kwamba meya huyo ni mbinafsi sana na miradi yote
inayotekelezwa katika manispaa ya Bukoba anataka kutanguliza maslahi yake mbele
na ndio maana kila mradi anataka mambo yasiwe wazi kwa madiwani.
Walimaliza kwa kutaja miradi ambayo meya huyo ametanguliza
maslahi yake mbele kuwa ni pamoja na mradi wa ujenzi kuu la Bukoba, upimaji wa
viwanja 5,000 na mradi wa ujenzi wa standi kuu ya mabasi ya Kyakailabwa.
No comments:
Post a Comment