Wednesday, August 14, 2013

Wafuasi wa Morsi tayari kwa maandamano


Wafuasi wa Morsi tayari kwa maandamano mapya Misri
Wafuasi wa rais aliyeondolewa mamlakani nchini Misri, Mohammed Morsi, wameanza kukusanyika mjini Cairo kutaka arejeshwe mamlakani.
Maelfu walikiuka onyo la maafisa wa usalama kusitisha maandamano yao na kutoka katika kambi walizokaa nje ya msikiti wa Rabaa al-Adawiya na medani ya Nahda.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu waliitaka serikali kujaribu kukomesha waandamanaji kuendelea kupiga kambi ili kuzuia vurugu na ghasia zengine.
Mamia ya wafuasi wa Morsi wameuawa kwenye makabiliano tangu aondolewe mamlakani na jeshi tarehe 3 mwezi Julai.
Zaidi ya watu 80 waliuawa kwa kupigwa risasi katika tukio moja karibu na msikiti wa Rabaa al-Adawiya wiki jana.
Mnamo siku ya Jumatano, serikali ilielezea hofu na wasiwasi ya kuzuka tena ghasia wakati ilipowaonya waandamanaji na kuwataka kusitisha harakati zao la sivyo serikali itumie nguvu kukabiliana nao.
Ilisema kuwa inasababisha hofu na tisho kubwa kwa usalama wa Misri.

No comments:

Post a Comment