Askofu wa kanisa la kiinjili la Kirutheri diosisi ya kaskazini magharibi Elisa Buberwa.
Viongozi wa dini Mkoani
Kagera waweka mikakati ya pamoja ya
kudumisha amani upendo na ushirikiano pia kuhakikisha wanawahubiria
waamini wa dini zao kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga na kuhatarisha amani ya Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla.
Mikakati hiyo iafikiwa
katika kikao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliyeitisha kikao hicho leo
tarehe 5/11/20212 ili kujadili na kuweka
mikakat i ya kuendeleza amani katika mkoa wa Kagera
kutokana na viashiria vya uvunjifu wa amani vilivyoanza kuonekana katika baadhi
ya maeneo mbalimbali Tanzania.
Mkuu wa Mkoa akiongea na viongozi
hao aliwasistiza kuwa serikali na dini ni vyombo ambavyo vinategemeana katika
kudumisha amani ya nchi. Viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuhakikisha
inchi inakuwa na amani.
Mhe. Massawe alisistiza juu
ya baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini kuacha kufanya miadhara ya kukashifu
madhehebu na dini za wenzao ambapo kila dhehebu au dini imetakiwa kuhubiri na
kutoa mafundisho yanayoihusu dini hiyo yenyewe.
Wakitoa maoni yao juu ya
kudumisha amani na upendo katika mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla viongozi
hao walipendekeza serikali kutafuta vyanzo vya machafuko ya dini kuliko
kushughulika na matokeo, pia serikali kuhakikisha inavisajili vikundi vyote
ambavyo vipo chini ya dini husika.
Aidha viongozi hao
wametoa wito kwa serikali kuwa wananchi wanaofanya vitendo vya kukashifu
vitabu vitakatifu wachukuliwe hatua za kisheria kama wao wenyewe na siyo kuwa
dini zao zinawatuma kutekeleza uhalifu huo kwa baadhi ya dini za wenzao.
Pia viongozi wa dini mkoa
wa Kagera wamesistiza kuwa dini isiwe kichaka cha kuficha maovu ya watu
wanaopenda kuficha uovu wao kwa mgongo wa dini. “Baadhi ya watu wanaofanya
maovu ya kuchoma nyumba za ibada
wachuliwe hatua na serikali mara moja na wasizifanye dini kuwa vichaka vya
kuficha uovu wao.” Alisistiza Askofu Method Kilaini Jimbo Katoliki la Bukoba.
Katika Kufunga kikao hicho
Mkuu wa Mkoa amewaomba viongozi hao wa dini kushirikiana na serikali
kulitafutia ufumbuzi suala la ajira za vijana ambapo amewahimiza viongozi hao
kuanzisha vyuo mbalimbali vya ufundi vya kuwafunza vijana kujitegemea na siyo kuisubiri serikali kuwaajili. Aidha amewahimiza
viongozi hao kuwahubiri wananchi wa Kagera kufanya kazi na kuacha uvivu ili
kujipatia kipato.
No comments:
Post a Comment