Wakazi wa Kisiwa cha Goziba
Kilichoko Wilayani Muleba wamekombolewa na kampuni ya mawasIliano ya Vodacom
Tanzania baada ya kampuni hiyo kuzindua mnara wake wa mawasiliano katika kisiwa hicho ambapo wananchi sasa wanaweza kuwasiliana popote
Tanzania na duniani kwa kutumia mtandao wa mawasiliano wa Vodacom.
Mnara wa Vodacom Kisiwani Goziba ulizinduliwa jana
tarehe 30/10/2012 na Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe aliyembatana na Mkuu
wa Wilaya ya Muleba Mhe. Lembrisi Kipuyo. Pia Katika uzinduzi huo Kampuni ya
Vodacom iliwakilishwa na Salum Mwalimu ambaye ni Meneja Mahusiano ya nje wa
Kampuni hiyo.
Katika Uzinduzi huo Meneja Mahusiano ya nje wa
Vodacom Salum Mwalimu aliwaomba wananchi wa kisiwa cha Goziba kuulinda na
kuutunza mnara huo kwani alisema kuwa mnara huo umejengwa kwa gharama kubwa, ni
zaidi ya mara mbili ya gharama ya kujenga mnara mmoja katika eneo la nchi kavu.
Pia aliwahakikishia wananchi wa Goziba kuwa huduma nyingine mbalimbali kama M- Pesa zitapelekwa kwao.
Wananchi wa Kisiwa cha Goziba ambao ni 6000 pamoja na kuchangia asilimia 25 ya pato la
wilaya ya Muleba, walisema kuwa kabla ya mnara huo hawakuwa na aina yoyote ya
mtandao wa simu, pia bado wanakabiliwa na changamoto katika huduma za kijamii
kama shule, Zahanati, na maji safi na slaama. Vilevile usafiri wa
kuaminika na kukumbwa na ujambazi wa
mara kwa mara na kunyanganywa mali zao.
Wananchi hao waliishukuru Kampuni ya Vodacom
Tanzania kwa kuwakumbuka kupitia mbunge wao Charles Mwijage wa Jimbo la Muleba
Kasikazini kuwawekea mnara huo ambao utawatatulia baadhi ya kero zao kama kero
ya ulinzi kwani itakuwa rahisi kutoa taarifa za uharifu kwa haraka sana pale
unapotokea.
Mkuu wa Mkoa alisistiza sana wananchi hao kuutumia
mtandao huo kwa manufaa yao na taifa lakini siyo kutumia simu zao kwa mambo ya
uhasherati kwani UKWIMWI bado unatisha sehemu za visiwani. Aliwasistiza
wananchi hao kuwa waaminifu walioko kwenye ndoa, kutumia kinga na vijana
kusubiri muda wao wa kuoa ndiyo waoane. Pia Mhe. Massawe alitumia muda huo
kuwagawia kinga (kondomu) wananchi hao na kuwashauri kuzitumia ili kupanga
uzazi na kujikinga na virusi vya UKWIMWI.
Vodacom Tanzania tayari pia imetoa Tshs.
4,200,000/= kwa ajili ya ujenzi wa zahanati, pia Mkuu wa Mkoa naye alitoa Tshs
500,000/= ili kuendeleza jengo la zahati ya Goziba ambalo limefikia hatua ya
Msingi. Changamoto ni vifaa vyote vya ujenzi kupatika na nje ya kisiwa hicho
hata matofari ya kujengea yafyatuliwa Mwanza
na kuletwa kisiwani humo isipokuwa mawe tu.
Mnara wa Vodacom siyo tu ni faida ya wakazi wa
Goziba na visiwa vya jirani isipokuwa imekuwa mkombozi kwa Manahodha wa
mitumbwi iliyokuwa inapotea mara kwa mara na kujikuta sehemu nyingine kwasababu
ya kisiwa hicho kutoonekana kwa mbali. Mnara huo umekuwa ndiyo dira ya nahodha
wanaokwenda huko kwasasa.
Wilaya ya Muleba inavyo visiwa 36 na 24 tu ndivyo
vinakaliwa na wananchi. Pia serikali ianaendelea na juhudi za kuhakikisha
huduma za kijamii zinapatikana katika kisiwa hicho ambapo inatarajia katika
miaka miwili ijayo itakuwa tayari imeanzisha kituo cha Polisi kisiwani humo.
Imeandikwa na : Sylvester
Raphael
Afisa
Habari Mkoa
KAGERA
@2012
No comments:
Post a Comment