Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa wa Kagera Peter Mushi, akitoa maelezo ya kikao cha Mwenyekiti wa CCM Bi. Costancia Buhiye na waandishi wa habari.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa na waandishi wa habari.
Baadhi ya viongozi wa CCM.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera kimeiagiza halmashauri ya
manispaa ya Bukoba kutoa taarifa sahihi kwa wananchi juu ya miradi
inayotekelezwa na itakayotekelezwa ndani ya manispaa hiyo.
Agizo
hilo lilitolewa na mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kagera Bi Costancia
Buhiye kwenye taarifa yake aliyoisoma mbele ya wajumbe wa kamati ya
siasa ya mkoa wa Kagera na waandishi wa habari alipokutana nao jana
kwenye ukumbi wa chama hicho ulioko katika manispaa ya Bukoba.
Katika
taarifa hiyo Bi. Buhiye alisema kuwa Halmashauri ya manispaa ya Bukoba
ihakikishe inatoa taarifa sahihi kwa wananchi juu ya miradi ya upimaji
wa viwanja na ugawaji 5,000, mradi wa ujenzi wa soko kuu la kisasa la
Bukoba na kituo cha mabasi cha kisasa ili haki itendeke kwa kila
mwananchi husika.
Bi. Bihuye kwenye taarifa yake hiyo alisema
chama kimefikia uamzi wa kutoa agizo hilo baada ya kupokea kwa mguso wa
aina ya kipekee hali ya siasa na kiuongozi iliyojitokeza katika manispaa
ya Bukoba inayoashiria uvunjifu wa amani na mshikamano.
Alisema
kuwa katika kuimarisha mshikamano na kuhakikisha hali ya uvunjifu wa
amani katika halmashauri ya manispaa haijitokezi kamati ya siasa ya mkoa
wa Kagera imeuagiza uongozi wa CCM wa wilaya ya Bukoba mjini kukaa
vikao vya kikatiba kujadili hali ya malumbano na baadae kiweze
kuwasilisha mapendekezo ya malumbano hayo kwa uongozi CCM mkoa ili
yapatiwe ufumbuzi wa kudumu mapema iwezekanavyo.
Pia aliviomba
vyombo vya habari viwaelimishe wananchi wa halmashauri ya manispaa ya
Bukoba wavipuuze vipeperushi ma propoganda zenye nia ya kuwagawa.
"Chama
cha mapinduzi tunawaomba wananchi kuendelea kuwa wamoja kwani umoja ni
nguvu na utengano ni udhaifu na umoja ni ushindi kwani pasipo na umoja
hapana amani na pasipo amani hakuna maendeleo" alimaliza taarifa yake
mwenyekiti huyo.
Taarifa ilitolewa na chama hicho inahusiana na
mgogoro uliopo kati ya mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani
na waziri wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki, Kagasheki
kwenye mkutano wake wa hadhara alioufanya kwenye viwanja vya uhuru
aliuambia uongozi wa manispaa ya Bukoba kuweka wazi mikataba ya miradi
ya maendeleo inayoiibua ili wananchi waielewe na baadae waikubali.
Alisema
wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wanapinga miradi ya
maendeleo inayoibuliwa katika manispaa hiyo kwa kuwa inafanyika kwa
uficho mkubwa hivyo wananchi wanashindwa kuielewa na kusema kuwa ndio
maana wananchi baadhi ya miradi wanaipinga, aliitaja miradi hiyo kuwa ni
pamoja mradi wa ujenzi wa soko kuu la Kisasa la Bukoba na mradi wa
upimaji wa viwanja 5,000.
Kagasheki katika mkutano huo alisema
kuwa ubabe katika suala zima la kutekeleza miradi inayogusa wananchi
kuwa hautakiwe, alisema hatua ya meya Amani kuwatangazia wananchi
kupitia kituo kimoja cha radio kuwa iwe isiwe soko litafunjwa mwezi
januari ni ya kibabe.
Utekelezwji wa miradi ya maendeleo katika
manispaa ya Bukoba sasa imeanza kukumbana na vizingiti ambapo
wafanyabiashara walioko ndani ya soko wamefungua shauri mahakama kuu
kupinga kuondolewa ndani ya soko hilo bila kuelezswa hatima yao, pia
baadhi ya watu wamefungua kesi mahakamani kupinga mradi wa upimaji wa
viwanja wanadai kuwa walikupunjwa wakati wa kulipwa fidia.
Mkuu wa mkoa wa Kagera alikuwa miongoni mwa walioudhuria kikao hicho.
No comments:
Post a Comment