WAZIRI wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki
ameutaka uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba kuweka wazi mikataba
inayoiingia inayohusu miradi ya maendeleo inayobuniwa na manispaa hiyo kabla ya kuanza kuteikeleza.
Alisema wakiweka wazi mikataba ya miradi ya maendeleo
inayobuniwa na uongozi wa manispaa hiyo kabla ya kuitekeleza watakuwa wanajenga
imani kuwa ya wananchi ambao ni sehemu ya miradi inayobuniwa.
Balozi Kagasheki alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia
wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye maeneo ya viwanja vya uhuru vilivyoko katika manispaa hiyo.
Alisema baadhi ya miradi ambayo manispaa inataka kuitekeleza
ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu jipya la Bukoba na upimaji wa viwanja
5,000 kuwa mikataba yake haileweki na haiku wazi, “mimi kama mbunge na diwani
wa manispaa ya Bukoba sijawahi kuonyeshwa mkataba aina yoyote naisikia kama
watu wengine” alisema waziri.
“Sioni haja ya uongozi wa manispaa ya kuficha mikataba ya
mradi unaotaka kuitekeleza, hali hii inaonyesha ndani ya mikataba hiyo palivyo
na ajenda ya siri, haiwezekani mambo ya wananchi yafanyike kwa uficho mkubwa,
na mimi sitakubali mambo yafanyike kwa uficho mkubwa nitahakikisha kila kitu
kinakuwa wazi” alisema huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu.
Waziri huyo alisema tunaposhindwa kuweka mambo wazi tunakuwa
tunawapa wapinzani nafasi ya kutujadili, “sasa natamka kuwa soko halitavinjwa januari
15, mwaka kesho kama uongozi wa manispaa unavyotaka kufanya kupisha ujenzi wa
soko kuu jipya la kisasa hadi tuhakiki
mikataba ambayo imefichwa, hapa ,kina kitu”
alisema kwa msisitizo.
Aliuagiza uongozi wa manispaa kabla ya kuwaondoa
wafanyabiashara walioko ndani ya soko kuwatafutia sehemu mbadala ambayo
wataitumia kufanya biashara wakati ujenzi wa soko ukiendelea.
“Nashangaa kuna baadhi ya viongozi walioko ndani ya manispaa
wanaosambaza habari kuwa napinga mambo ya maendeleo ndani ya manispaa ya
Bukoba, Naapa sipingi maendeleo ila ninachotaka ni kila kifanyike kwa kufuata taratibu zilizowekwa za
utekelezwaji wa miradi ya maendeleo inayobuniwa, hatutaki watu wabuni miradi na
waitekeleze kulingana na matakwa yao” alisema Balozi Kagasheki.
“Ningekuwa napinga mambo ya maendeleo ndani ya manispaa
nisingerekebisha soko sehemu wanapouzia ndizi, nisinge jenga vyumba vya
madarasa karibu kila kata, nisingeweka taa za barabarani na mambo mengine
makubwa, wanaosema ninapinga maendeleo inaonekana wana mazazo mgando” alisema.
Alimaliza kwa kuwaomba wananchi wa manipaa ya Bukoba waimarishe
mshikamano ili waweze kupambana na vitendo vya kidharimu vinavyochangia
kuvuruga amani ndani ya manispaa hiyo.
Viongozi wa dini walikuwa miongoni mwa walioudhuria mkutano huo, anayempongeza balozi Kagasheki ni Padre Projestus Mutungi wa kanisa Katoriki.
Baadhi ya vijana wakisukuma gari alilokuwemo Balozi Kagasheki, wa.lifanya hivyo baada ya kukunwa na hotuba yake aliyoitoa.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha KAKAU wakifanya vitu vyao.
No comments:
Post a Comment