MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu, Fabian Massawe
amewaagiza viongozi wa halmashauri za wilaya na manispaa mkoani humo kutunga
sheria ndogo ndogo zitakazowabana wazazi wanakataa kuwapeleka watoto wao kwenye
vituo vya afya na zahatati kwa ajili ya
kupata chanzo.
Massawe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha afya ya msingi
mkoani Kagera kilichokuwa kinalenga kueleza mikakati ya chanzo mpya ya
kuthibiti ugonjwa wa kuhara na rumonia itakayoanza kutolewa mkoani Kagera hivi
karibuni kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja.
Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu huyo
wa mkoa leo, Massawe amesema wanakataa kuwapeleka watoto kwenye vituo vya afya
na zahanati wanakuwa wanalenga kuchangia ongezeko la vifo hapa nchini kwa
watoto hasa walio na umri wa miaka 5.
Amesema kuwa sheria ndogo ndogo zikitungwa zitawabana wale wanaoenda kinyume na mikakati
ya serikali ya kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya nzuri, Masaawe
amesema kuwa wananchi wanapokuwa na afya nzuri wanachangia sana ukuaji wa
kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa
ujumla.
Mkuu huyo wa mkoa amesema taifa linaloundwa na watu wenye
afya mbovu linadumaa katika Nyanja zote za maendeleo ya kijamii na kiuchumi,
aliendelea kusema kuwa kusema kuwa mwitikio wa wazazi kuwapeleka watoto wao kwa
ajili ya chanjo unaridhisha.
Akitoa takwimu hali ya halisi ya
kiwango cha chanjo mkoani Kagera amesema kuwa kwa mwaka 2009 kiwango cha chanjo
mkoani Kagera kilikuwa asilimia 84, 2010 asilimia 87 na mwaka 2011 kiwango cha chanjo mkoani Kagera
kilikuwa asilimia 88.
Kwa upande wake mratibu wa chanjo
wa mkoa wa Kagera, Jackson Minja katika kikao hicho amesema kuwa chanzo kwa
ajili ya magonjwa ya kuhara na rumonia itatolewa kwa watoto chini ya umri wa
mwaka mmoja na chanjo hiyo itaanza kutolewa kuanzia mwaka kesho, mwezi januari.
Washiriki wengine wa kikao cha chanjo.
Baadhi ya waratibu wa masuala ya chanjo mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment