Thursday, November 29, 2012

KIKAO CHA MWENYEKITI WA CCM NA WAANDISHI WA HABARI

 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa wa Kagera Peter Mushi, akitoa maelezo ya kikao cha Mwenyekiti wa CCM Bi. Costancia Buhiye na waandishi wa habari.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa na waandishi wa habari.
 Baadhi ya viongozi wa CCM.
 CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera kimeiagiza halmashauri ya manispaa ya Bukoba kutoa taarifa sahihi kwa wananchi juu ya miradi inayotekelezwa na itakayotekelezwa ndani ya manispaa hiyo.

Agizo hilo lilitolewa na mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kagera Bi Costancia Buhiye kwenye taarifa yake aliyoisoma mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Kagera na waandishi wa habari alipokutana nao jana kwenye ukumbi wa chama hicho ulioko katika manispaa ya Bukoba.

Katika taarifa hiyo Bi. Buhiye alisema kuwa Halmashauri ya manispaa ya Bukoba ihakikishe inatoa taarifa sahihi  kwa wananchi juu ya miradi ya upimaji wa viwanja na ugawaji 5,000, mradi wa ujenzi wa soko kuu la kisasa la Bukoba na kituo cha mabasi cha kisasa ili haki itendeke kwa kila mwananchi husika.

Bi. Bihuye kwenye taarifa yake hiyo alisema chama kimefikia uamzi wa kutoa agizo hilo baada ya kupokea kwa mguso wa aina ya kipekee hali ya siasa na kiuongozi iliyojitokeza katika manispaa ya Bukoba inayoashiria uvunjifu wa amani na mshikamano.

Alisema kuwa katika kuimarisha mshikamano na kuhakikisha hali ya uvunjifu wa amani katika halmashauri ya manispaa haijitokezi kamati ya siasa ya mkoa wa Kagera imeuagiza uongozi wa CCM wa wilaya ya Bukoba mjini kukaa vikao vya kikatiba kujadili hali ya malumbano na baadae kiweze kuwasilisha mapendekezo ya malumbano hayo kwa uongozi CCM mkoa ili yapatiwe ufumbuzi wa kudumu mapema iwezekanavyo.

Pia aliviomba vyombo vya habari viwaelimishe wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wavipuuze vipeperushi ma propoganda zenye nia ya kuwagawa.

"Chama cha mapinduzi tunawaomba wananchi kuendelea kuwa wamoja kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na umoja ni ushindi kwani pasipo na umoja hapana amani na pasipo amani hakuna maendeleo" alimaliza taarifa yake mwenyekiti huyo.

Taarifa ilitolewa na chama hicho inahusiana na mgogoro uliopo kati ya mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba Anatory Amani na waziri wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki, Kagasheki kwenye mkutano wake wa hadhara alioufanya kwenye viwanja vya uhuru aliuambia uongozi wa manispaa ya Bukoba kuweka wazi mikataba ya miradi ya maendeleo inayoiibua ili wananchi waielewe na baadae waikubali.

Alisema wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wanapinga miradi ya maendeleo inayoibuliwa katika manispaa hiyo kwa kuwa inafanyika kwa uficho mkubwa hivyo wananchi wanashindwa kuielewa na kusema kuwa ndio maana wananchi baadhi ya miradi wanaipinga, aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja mradi wa ujenzi wa soko kuu la Kisasa la Bukoba na  mradi wa upimaji wa viwanja 5,000.

Kagasheki katika mkutano huo alisema kuwa ubabe katika suala zima la kutekeleza miradi inayogusa wananchi kuwa hautakiwe, alisema hatua ya meya Amani kuwatangazia wananchi kupitia kituo kimoja cha radio kuwa iwe isiwe soko litafunjwa mwezi januari ni ya kibabe.

Utekelezwji wa miradi ya maendeleo katika manispaa ya Bukoba sasa imeanza kukumbana na vizingiti ambapo wafanyabiashara  walioko ndani ya soko wamefungua shauri mahakama kuu kupinga kuondolewa ndani ya soko hilo bila kuelezswa hatima yao, pia baadhi ya watu wamefungua kesi mahakamani kupinga mradi wa upimaji wa viwanja wanadai kuwa walikupunjwa wakati wa kulipwa fidia.

 Mkuu wa mkoa wa Kagera alikuwa miongoni mwa walioudhuria kikao hicho.

Wednesday, November 28, 2012

KIKAO CHA KUPASHANA HABARI JUU YA CHANJO ITAKAYOZINDULIWA JANUARI JUU YA MAGONJWA YA NYUMONIA NA KUHARA

 Baadhi ya washiriki wa kikao.

MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu, Fabian Massawe amewaagiza viongozi wa halmashauri za wilaya na manispaa mkoani humo kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wazazi wanakataa kuwapeleka watoto wao kwenye vituo  vya afya na zahatati kwa ajili ya kupata chanzo.

Massawe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha afya ya msingi mkoani Kagera kilichokuwa kinalenga kueleza mikakati ya chanzo mpya ya kuthibiti ugonjwa wa kuhara na rumonia itakayoanza kutolewa mkoani Kagera hivi karibuni kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu huyo wa mkoa leo, Massawe amesema wanakataa kuwapeleka watoto kwenye vituo vya afya na zahanati wanakuwa wanalenga kuchangia ongezeko la vifo hapa nchini kwa watoto hasa walio na umri wa miaka 5.

Amesema kuwa sheria ndogo ndogo  zikitungwa  zitawabana wale wanaoenda kinyume na mikakati ya serikali ya kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya nzuri, Masaawe amesema kuwa wananchi wanapokuwa na afya nzuri wanachangia sana ukuaji wa kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa  ujumla.

Mkuu huyo wa mkoa amesema taifa linaloundwa na watu wenye afya mbovu linadumaa katika Nyanja zote za maendeleo ya kijamii na kiuchumi, aliendelea kusema kuwa kusema kuwa mwitikio wa wazazi kuwapeleka watoto wao kwa ajili ya chanjo unaridhisha.

Akitoa takwimu hali ya halisi ya kiwango cha chanjo mkoani Kagera amesema kuwa kwa mwaka 2009 kiwango cha chanjo mkoani Kagera kilikuwa asilimia 84, 2010 asilimia 87 na  mwaka 2011 kiwango cha chanjo mkoani Kagera kilikuwa asilimia 88.

Kwa upande wake mratibu wa chanjo wa mkoa wa Kagera, Jackson Minja katika kikao hicho amesema kuwa chanzo kwa ajili ya magonjwa ya kuhara na rumonia itatolewa kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja na chanjo hiyo itaanza kutolewa kuanzia mwaka kesho, mwezi januari.

 Wajumbe wa kikao wakisikiliza Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw. Massawe.
 Washiriki wengine wa kikao cha chanjo.
Baadhi ya waratibu wa masuala ya chanjo mkoani Kagera.

Tuesday, November 27, 2012

WALEMAVU KAGERA WAAHIDIWA KUTAFUTIWA MIKOPO ILI KUPATA MITAJI YA SHUGHULI ZAO

 Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na walemavu wa kikundi cha BUDAP.

Katika kusistiza kauli yake kwa vitendo juu wa walemavu katika mkoa wa Kagera kujitegemea na kujishughulisha pia  kufanya kazi mbalimbali za kujipatia kipato na kuacha kuombaomba mitaani Mkuu wa Mkoa wa Kagera ametembelea kikundi cha Walemavu (BUDAP) Nyamkazi katika mji wa Bukoba ili kujionea jinsi kikundi hicho kinavyojishughulisha.

Kikundi cha BUDAP ni kikundi cha walemavu ambao wanaendesha shughuli zao za kutengeneza bidhaa mbalimbali za mikono na kujipatia kipato kwa kuuza bidhaa hizo hasa kwa wageni mbalimbali wanaofika hapa mkoani katika sekta ya utalii. Bidhaa hizo ni ngoma za asili, vidani mbalimbali pamoja na bidhaa nyinginezo mbalimbali za mikono.

Baada ya Mhe. Massawe kufika katika kituo hicho na kujionea jinsi kikundi hicho kinavyojishughulisha na kazi za mikono amehaidi kuwatafutia mtaalam wa kutengeneza andiko la mradi ili afike katika kituo hicho na kuwatengenezea andiko ambalo atalitumia kuwatafutia wafadhili ili waweze kupata mikopo kupitia andiko hilo.

Pia amewasistiza walemavu hao kubuni miradi zaidi itakayowavutia wafadhili katika kuwasaidia. Vile vile Mhe. Massawe amewahaidi kuwa ataongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ili naye awatembelee na kuona shughuli zao na jinsi ya kuwakwamua katika kupata mtaji wa kujishulisha zaidi.

Changamoto kubwa walionayo walemavu hao ni wenzao kuwakimbia na kutopenda kujishughulisha na kuishia mijini na kuendelea kuombaomba ambapo wanasema kuwa walianza kikundi na watu 20 lakini mpaka sasa wamebakia wanawake wawili na wanaume watano tu.

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kagera alitoa kauli ya walemavua kuacha kuwa wategezi wa kuombaomba barabarani na mijini na kutafuta miradi ya kujishulisha ili wajipatie kipato cha kujiinua wao wenyewe na familia zao waka, kauli hiyo aliitoa wiki jana Alhamisi tarehe 22/11/2012 wakati akikabidhi msaada wa baiskeli mbili kwa walemavu.

Na;         Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa
KAGERA @2012


Shilingi bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini

Shilingi bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini
Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.

Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).

Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.

Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi. Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka TANESCO.

 Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo (installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.

Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1.      Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.

2.      Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.
3.      Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.

Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha

Monday, November 26, 2012

MAFUNZO KWA WAANDISHI MKOANI KAGERA JUU YA MASUALA YA UTAWALA BORA NA HAKI ZA BINADAMU

 Mwandishi wa habari mkongwe Nyaronyo Kicheele akiwapa elimu waandishi wa habari.
Bw. Nyaronyo Kicheele.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo.

Washiriki wa mafunzo.

PHOTOS UZINDUZI WA MKOA WA KATAVI

  Mwanasiasa Mkongwe na Mbunge Mstaafu, Chrisant Majiyatanga Mzindakaya akicheza ngoma ya Uyeye katika sherehe za uzinduzi wa mkoa wa Katavi kwenye uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda Novemba 24, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakizungumza na Mbunge wa Mpanda Mjini,Said Amour Arfi  katika sherehe za uzinduzi wa mkoa wa Katavi zilizofanyika kwenye uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda, Novemba 24,2012. (Picha na Ofis ya Waziri Mkuu)

Michoro ya kampasi ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kinachojengwa Mloganzila

Michoro ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila iliyo kijijini Kwembe  katikati ya Wilaya za Kisarawe Mkoa wa Pwani na Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam. Hii ni sehemu ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
  (MUHAS) inayojengwa kwenye eneo la ekari 3800 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya wapatao 15,000 kwa mwaka, na pia itakua sehemu ya kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na ya kawaida nchini. 

 Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, ujenzi  wa Hospitali hii, ambayo pesa ya ujenzi wake imeshapatikana, unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi kuanza. Kwa maneno mengine Kampasi ya Muhimbili ya Mloganzila inategemewa kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka 2015.

Tayari wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya Mloganzila wameshaanza mafunzo ndani na nje ya nchi. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita (600). 

Sambamba na kampasi ya MUHAS ya Mloganzila pia ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Dodoma  (UDOM)  umeshaanza na kufikia hatua ya juu na ambapo pia hospitali  hiyo inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2015.

Kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba mchakato wa  kufanikisha uanzishaji wa Chuo Hospitali hiyo vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu wakiwemo Madaktari na watumishi wengine wako nchini na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na mafunzo mbalimbali.

Chuo hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi mahitaji ya Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa, ikiwa ni mikakati kabambe ya serikali ya awamu ya nne katika kuhakikisha nchi ina wataalamu wengi na huduma za kisasa za afya ili kuondokana na adha ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Kwa sasa MUHAS inachukua takriban wanafunzi 2442 wa udaktari na huduma za afya kwa mwaka. Hivyo ujio wa kampasi ya Afya Mloganzila na Kampasi ya afya ya UDOM   utaharakisha mpango wa serikali wa kupunguza wastani wa wagonjwa  kwa daktari mmoja kwa kiwango kikubwa. Hivi sasa wastani ni daktari mmoja anahudumia wagonjwa 30,000. 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA MREJEO WA HALI YA EL NIÑO NA LA NIÑA

Taarifa hii inatoa mrejeo wa hali ya joto la bahari (El Niño na La Niña) kwa kipindi cha Julai
hadi Novemba, 2012.


Hali ya sasa na mwelekeo wa Hali ya joto la Bahari:
Katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2012, hali ya joto la bahari ukanda wa tropikali wa
Bahari ya Pasifiki iliongezeka na kuwa juu ya wastani hali iliyoashiria kuwepo kwa El Niño
hafifu, hata hivyo hali ya mifumo ya upepo, mgandamizo wa hewa katika usawa wa bahari na
mawingu vilishindwa kuwiana na ongezeko hilo hafifu la joto la bahari.


Katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni hadi sasa hali ya joto la bahari katika ukanda wa
tropikali wa Bahari ya Pasifiki imekuwa ya wastani, hali hii haiashirii kuwepo kwa aidha El
Niño au La Niña. Aidha katika ukanda wa Bahari ya Hindi unaopakana na nchi yetu pamoja na
joto la bahari kuwa la juu ya wastani, mifumo ya upepo na mgandamizo wa hewa vimeendelea
kusababisha upungufu wa unyevunyevu katika anga. Hali hii ya mabadiliko ya joto la bahari
na mifumo ya hali ya hewa si ya kawaida na haijawahi kutokea katika miaka iliyopita.


Kutokana na hali hii isiyokuwa ya kawaida taasisi zinazohusika na masuala ya hali ya hewa
katika Kanda ya Pembe ya Afrika (ICPAC) na Kanda ya Kusini mwa Afrika (SADC-CSC) kwa
mara ya kwanza zimeandaa warsha ya wataalamu wa hali ya hewa ikiwemo Tanzania, kufanya
uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mrejeo wa mwelekeo wa mvua za msimu katika
ukanda huu. Mikutano hii itafanyika tarehe 29 hadi 30 Novemba, 2012 Nairobi, Kenya na tarehe
5 hadi 13 Disemba, 2012 Lusaka, Zambia. Baada ya taarifa hiyo ya kikanda, Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania itapitia taarifa hiyo na kutoa mrejeo wa utabiri wa msimu wa mvua nchini.
Tathmini ya mvua kuanzia mwezi Oktoba hadi Novemba 2012:


Katika maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka, hususani maeneo ya ukanda wa Ziwa
Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) mvua zinaendelea
kunyesha, wakati maeneo ya nyanda za juu Kaskazini mashariki (mikoa ya Kilimanjaro, Arusha
na Manyara) na pwani ya Kaskazini (mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga na
visiwa vya Unguja na Pemba) kumekuwa na mvua ambazo ni za chini ya wastani.


Aidha, katika maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka, hususani maeneo ya Kigoma,
Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa, Tabora, Katavi na Singida mvua zimeanza na zinaendelea
kunyesha. Mtawanyiko wa mvua hizo si wa kuridhisha katika baadhi ya maeneo.
Ushauri:


Katika maeneo ambayo mvua iliyonyesha mpaka sasa ni chini ya wastani, wananchi
wanashauriwa kutumia maji kwa uangalifu na kuhifadhi malisho kwa ajili ya mifugo.
Pamoja na mabadiliko hayo ambayo si ya kawaida yaliyojitokeza kuna uwezekano wa kuwepo
kwa vipingi vifupi vya mvua kubwa hivyo wananchi wanashauriwa kuendelea kuchukua
tahadhari.


Mamlaka ya hali ya hewa inaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na itaendelea
kutoa taarifa “update” za mara kwa mara.


Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Sunday, November 25, 2012

MAMBO YA KIPAIMARA HAYO!

 Rose Edwin Mwesiga apata kipaimara hapa yuko katika picha ya pamoja na ndugu zake.
Baadhi ya wazazi na ndugu wa Rose.

FAMILY DAY YA BENKI YA CRDB MATAWI YA KARAGWE NA BUKOBA YAFANA

 Watumishi wa CRBD tawi la Bukoba wakitambulishwa wakati wa family day ya benki hiyo iliyofanyika kwenye ufukwe wa ziwa victoria na kupambwa na michezo mbalimbali.
 Familia ya Victor mtumishi wa benki ya CRBD tawi la Bukoba.
 Mchezo wa mpira wa miguu ni moja ya burudani zilizopamba sherehe hiyo.
 Baadhi ya watumishi wa CRDB walioshiriki kwenye mpambano wa mpira wa miguu.
 Bw. Sendwa, Meneja wa CRDB wa tawi la Bukoba akitetra jambo na mmoja wa wadau wa benki ya CRDB.
 Mambo ya vollyball.
 Watumishi wa benki CRDB wa tawi la karagwe wakiwashangilia wanawake walioshinda mchezo wa kuvuta kamba.
Baadhi ya wadau walioudhulia sherehe, wa pili toka kulia ni Mmiliki wa saloon ya kisasa inajukana kwa jina la Nice and beauty.

VOLUNTEES FOR MUSHEMBA FOUNDATION FROM DENMARK

Wanashirikana na watanzania kumenya senene,  walikutwa kwenye ufukwe wa ziwa Victoria eneo la Kiroyera.

Saturday, November 24, 2012

MKUTANO WA HADHARA ULIOANDALIWA NA WAZIRI KAGASHEKI

 Balozi Khamis Kagasheki akipongezwa na wananchi baada ya kumaliza hotuba yake ya mkutano wa hadhara aliouandaa uliofanyika kwenye viwanja vya uwanja wa uhuru.




 


WAZIRI wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki ameutaka uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba kuweka wazi mikataba inayoiingia inayohusu miradi ya maendeleo inayobuniwa na manispaa hiyo  kabla ya kuanza kuteikeleza.



Alisema wakiweka wazi mikataba ya miradi ya maendeleo inayobuniwa na uongozi wa manispaa hiyo kabla ya kuitekeleza watakuwa wanajenga imani kuwa ya wananchi ambao ni sehemu ya miradi inayobuniwa.



Balozi Kagasheki alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye maeneo ya viwanja vya uhuru vilivyoko katika manispaa hiyo.



Alisema baadhi ya miradi ambayo manispaa inataka kuitekeleza ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu jipya la Bukoba na upimaji wa viwanja 5,000 kuwa mikataba yake haileweki na haiku wazi, “mimi kama mbunge na diwani wa manispaa ya Bukoba sijawahi kuonyeshwa mkataba aina yoyote naisikia kama watu wengine” alisema waziri.



“Sioni haja ya uongozi wa manispaa ya kuficha mikataba ya mradi unaotaka kuitekeleza, hali hii inaonyesha ndani ya mikataba hiyo palivyo na ajenda ya siri, haiwezekani mambo ya wananchi yafanyike kwa uficho mkubwa, na mimi sitakubali mambo yafanyike kwa uficho mkubwa nitahakikisha kila kitu kinakuwa wazi” alisema huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu.



Waziri huyo alisema tunaposhindwa kuweka mambo wazi tunakuwa tunawapa wapinzani nafasi ya kutujadili, “sasa natamka kuwa soko halitavinjwa januari 15, mwaka kesho kama uongozi wa manispaa unavyotaka kufanya kupisha ujenzi wa soko kuu jipya la kisasa hadi  tuhakiki mikataba ambayo imefichwa, hapa ,kina kitu”  alisema kwa msisitizo.



Aliuagiza uongozi wa manispaa kabla ya kuwaondoa wafanyabiashara walioko ndani ya soko kuwatafutia sehemu mbadala ambayo wataitumia kufanya biashara wakati ujenzi wa soko ukiendelea.



“Nashangaa kuna baadhi ya viongozi walioko ndani ya manispaa wanaosambaza habari kuwa napinga mambo ya maendeleo ndani ya manispaa ya Bukoba, Naapa sipingi maendeleo ila ninachotaka ni kila  kifanyike kwa kufuata taratibu zilizowekwa za utekelezwaji wa miradi ya maendeleo inayobuniwa, hatutaki watu wabuni miradi na waitekeleze kulingana na matakwa yao” alisema Balozi Kagasheki.



“Ningekuwa napinga mambo ya maendeleo ndani ya manispaa nisingerekebisha soko sehemu wanapouzia ndizi, nisinge jenga vyumba vya madarasa karibu kila kata, nisingeweka taa za barabarani na mambo mengine makubwa, wanaosema ninapinga maendeleo inaonekana wana mazazo mgando” alisema.



Alimaliza kwa kuwaomba wananchi wa manipaa ya Bukoba waimarishe mshikamano ili waweze kupambana na vitendo vya kidharimu vinavyochangia kuvuruga amani ndani ya manispaa hiyo.





 Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba akiondoka kwenye jukwaa baada ya mkutano.
 Viongozi wa dini walikuwa miongoni mwa walioudhuria mkutano huo, anayempongeza balozi Kagasheki ni Padre Projestus Mutungi wa kanisa Katoriki.


 Baadhi ya vijana wakisukuma gari alilokuwemo Balozi Kagasheki, wa.lifanya hivyo baada ya kukunwa na hotuba yake aliyoitoa.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha KAKAU wakifanya vitu vyao.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA SEKTA YA AFYA IKULU, APOKEA CHETI CHAKE CHA UDAKTARI WA MUHAS

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  toka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka  2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini. Sherehe hiyo fupi ilifanyika leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya akisoma risala kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo Desemba mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo Novemba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.

UZINDUZI WA MKOA WA KATAVI Friday, November 23, 2012 5:38 AM

Waziri Mkuu, Mizengoi Pinda  akitazama mtambo wa kuchemsha maji kwa kutumia nguvu ya jua wakati alipokagua banda la CARMATEC Novemba 23, 2012 katika monyesho ya kuadhimisha uzinduzi wa mkoa wa Katavi unaotarajiwakufanyiak Vovemba 24, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Friday, November 23, 2012

SEMINA YA UELIMISHAJI WA MAJUKUMU YA MFUKO NA TARATIBU ZA ULIPAJI WA MAFAO

 Washiriki wa semina.




 Katibu tawala wa mkoa wa Kagera anayeshughulikia masuala ya utumishi Richard Kwitega akifungua semina.
 Afisa mfawidhi wa mkoa wa PSPF, Thadeo Rweyunga (kulia) na kushoto ni Richard Kwitega.
Mkuu wa TAKUKURU Bi. Domina Mukama alikuwa mmoja wa walioudhuria semina ya PSPF.