TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI
Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko wa wawakilishi
wa matawi 189 ya chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa mwanza. Umoja huu wa
matawi unawajumuisha wajumbe kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.
Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30.nov 2013
kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine
tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi wetu
wanaotuwakilisha kwenye vikao vya maamuzi kama
vile wilaya, mkoa na taifa wamekuwa waoga na wameshindwa kuwakilisha
mawazo yetu tuliyowatuma badala yake wengi wao wamekubali kuwa vibaraka wa kile
kinachoitwa CHADEMA KASKAZ
Kutokana na ukweli kwamba msingi wa chama chetu na chama
kingine chochote kile cha siasa, uimara na uhai wake unatokana na uwepo wa
misingi na matawi ya chama, hivyo sisi wanachama wa matawi haya 189 tumeamua
kuunganisha nguvu zetu kutetea chama chetu na kuhakikisha haki, heshima, katiba
na maadili ya chama vinafuatwa bila ya kuogopana wala kuoneana haya.
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania
na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
Chadema ni chama cha siasa kinachopaswa kuendeshwa kwa
misingi ya kufuata taratibu, kanuni na katiba yake na si vinginevyo. Lakini
badala yake kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa viongozi wetu wa juu kujitwalia
mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya katiba ya chama chetu hususan katika
kutoa haki sawa kwa viongozi na wanachama wa chama chetu. Kumekuwepo na upendeleo
wa hali ya juu sana kwa wale wanao amini kuwa ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo
kupelekea kuwaadhibu kama ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza bila kuhojiwa au
kukosolewa.
Sababu zilizotolewa na
kamati kuu hazikubaliki
Maamuzi
ya kamati kuu ya tarehe 20-21 /11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Ndg Samson Mwigamba, kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali ni
unafki na Uzandiki wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa Demokrasia kwa
kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama. Katiba yetu imeweka wazi
Ibara ya 6 Kifungu cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za nidhamu na
uwajibishaji ndani ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi bila
kufuata taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo sisi baadhi ya wanachama huo
ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi wetu
waliotumia nguvu zao na akili nyingi sana kukijenga chama.
Sababu kubwa ya kuandamwa
kwa viongozi hawa ni
1. Kutaka
kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za
serikali.
2. Michango
ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
3. Harambee za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
4. Kutaka
kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana
wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo
ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
5. Kutaka
kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia
ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama
ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.
Kushamiri
kwa migogoro
Mwenyekiti
na katibu mkuu wameshindwa kutatua migogoro ya viongozi na wanachama kutoka
mikoani kwa njia sahihi za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa viongozi
na wanachama kutumia njia ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na katibu mkuu
mwenyewe, kujitokeza mara kwa mara kwenye mitandao hiyo hiyo kwa madai ya
kutolea ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya husuyo maswala ya chama ilihali akijua
kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya vikao
ilipelekea migogoro mikubwa sana hususan mkoa wetu wa Mwanza na kupelekea kupoteza
Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa kwa baadhi ya madiwani,
kuvunjwa uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya chama na kutumia nafasi zao
kuopanga safu za uongozi wanao uwona watawatumikia wao na si chama, hivyo
kusababisha mifarakano mikubwa ndani ya chama na kupelekea kuvuliwa uongozi kwa
viongozi mbalimbali katika mkoa wetu kwa maamuzi yasiyo zingatia utafiti na
uhalisia wa kweli ndani ya chama.
Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja
katiba Mfano:
·
Kitendo cha kutoa muongozo nje na matakwa ya
katiba juu ya kuwapata wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi kama wabunge
kwamba wanaohitaji kugombea 2015 waandike barua makao makuu na wao ndio watatoa
wagombea kinyume na katiba ya chama Ibara 7.2.13 inayotoa taratibu ya kuwapata
wagombea, huwo ni uvunjaji wa katiba na ubakaji wa demekrasia ndani ya chama,
sizani kama kuna uhaini zaidi ya huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama leo sisi
Chadema hatuheshimu katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje siku
tukikabidhiwa nchi yenye watu wenye mawazo na mtizamo tofauti na sisi?.
Hatutaki kuamini kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja wa maopambano ya kivita.
Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa dhidi ya
Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lema
kumkashfu kiongozi wa chama Mh: Zitto
Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na Mzandiki kwendye mitandao ya kijamii pia
tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi ya Bw Henry Kilewo kwa kuweka waraka unaoitwa ripoti ya siri inayomhusu
Zitto mbao chama makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi wa
chama kukana mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo chama hakiusiki nao na
hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw
Kilewo ambaye pia ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama,
waraka huo ambao chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali akijua
kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu maadili ya
viongozi kanuni ya 10.
Pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa kwa
waandaaji wa tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti ya siri kuhusu Zitto
kwasababu tayari makada na viongozi wetu wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni
mwa waandaaji wa tamthilia hii.
Lakini cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia macho na
kupelekea kwetu baadhi ya wanachama kuamini zengwe hili la kumchafua Zitto Lina
Baraka zote za viongozi wa chama ngazi ya juu.
Tunataka
kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa waraka
ujulikanao kama mkakati wa mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo itumike kwa hawa
waliotumia njia chafu ya kuandaa waraka wa kumchafua zitto ambao chama
kinawajua na baadhi yao tumewaweka humu kwenye tamko letu.
Kingine
tunataka kwa mara nyingine kwa viongozi wa chama makao makuu kuwaambia umma wa
watanzania ni kwanini waraka huo huo uinaoitwa warajka wa siri kuhusu Zitto leo
viongozi na wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka huo uangawiwa kwa
wanachama na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si ubaguzi ni nini?.
Tunaonya na kulaani kitendo cha viongozi wetu kuendeleza
utawala wa kibabe na kupelekea kuhatarisha maisha ya baadhi ya wanachama na
viongozi wanaotofautiana nao kimtizamo mfano: kumezuka tabia ya baadhi ya
viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja jukwaani
hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia maneno ya uchochezi dhidi ya wanachama na
viongozi wanaokinzana nao kifikra na kimtizamo na kuhamasisha wanachama wasiojua
itikadi vizuri ya chama kuwa wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa
hadharani kwenye mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli
kubaki na maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali kuhusiana na
jambo hili.
Hitimisho
Mwekiti
na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi
ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii, M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya
kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza
uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.
Mwisho tunataka maamuzi haya HARAMU kamati kuu
yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate taratibu
na kanuni kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo tarehe 4/12/2013 tutaungana na
wapigania Demokrasia kote nchini kufanya maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka
uongozi uliopo utoke madarakani.
Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha
wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie
jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya
kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo
tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.
Tunamuagiza mbowe na slaa wasithubutu kukanyaga ardhi hii
ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiudhuru ama kubadili maamuzi yao HARAMU
haraka iwezekanavyo
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani
ya chama chetu,
Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha,
tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye
chama hiki vya kutosha,
Sasa sisi wanachadema wa matawi ya mwanza na kanda ya
ziwa kwa ujumla, tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi watupo chadema kwa
bahati mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi wakuu wa chama hiki,
tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob Nyanga Makani, Marehemu
Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe, kamanda Zitto Kabwe na sisi
wengine wengi.
Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina
yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA
CHADEMA.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA
ROBERT E.
GWANCHELE
Mwenyekiti wa umoja
wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA
ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA
No comments:
Post a Comment